Hawa wazee omba omba huku mjini imekuwa huzuni sana

Hawa wazee omba omba huku mjini imekuwa huzuni sana

The ice breaker

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2023
Posts
1,119
Reaction score
2,441
Hivi hawa wazee vikongwe ninao waona huku mjini posta, na mitaa ya upanga wakiwa wanaomba omba, huwa najiuliza walikosea wapi enzi za ujana wao,

Kwanini kipindi cha ujana wao hawakuandaa maisha yao ya uzeeni,

Je, hawana watoto wa kuwasaidia?

Unakuta kibibi au kibabu kinapigwa na baridi na mbu kwa kulala nje, kula ya tabu, yani wana tabu sana.

Bora kijana atabeba gunia la viazi , ata savaivu
 
mi huwa nawasaidia tu,

Wanasemaga baba ni kama Trekta la kutengeneza barabara likimaliza kazi linatelekezwa , hutumia nguvu sana kutunza familia lakini watoto wengi wakiwa wakubwa wanamsahau baba.

Kuna wazee wameuza mashamba kusomesha watoto, kuna wazee walikopa pesa nyingi kununulia kazi watoto, kuna wazee waliuza viwanja vyao kuhonga mawakili watoto wasiende jela, n.k. lakini watoto utawasikia "nani kama mama"

Ewe kijana pambana sana uwe na savings zako za kutosha, uzeeni kuwategemea watoto wakutunze ni kwa neema tu
 
Back
Top Bottom