Mm ni napenda kazi anazo fanya diamond na kila kitu kuhusu mzk wake lakini kwa hili hapa diamond amkumbuke huyo Hawa! Hayo malalamiko hayajaanza leo toka kipindi kile diamond ameenda "zizu fashion" kununua nguo na ana mkuta hawa akiwa anauza nguo huku akiimba,siku ya pili tena diamond anarudi anamkuta tena Hawa
ndipo anampenda na kuomba kufanya nae kazi Hawa bila hiyana anakubali na kufanya nae wimbo wa nitarejea wakaenda mbali zaidi wakaingia kwenye mauhusiano( kipindi kile haikuvuma coz diamond alikuwa bado hajawa diamond wa sahizi) ndipo diamond anafanya nae ngono huyu dada
,wakawa na show sikumbuki ni show gani kama sio kil.awards bas BSS kwenye mazoezi diamond alikuwa hata hampi nauli huyo dada ya kufikia mazoezini kila kitu Hawa alifanya kwa gharama zake katika maandalizi yote ya show kwenda na kurudi! Wakafanya bonge moja la show lakini Hawa hakuambulia hata sent ya malipo ya show! Ikawa kama kafanya bure hivi sijui kwann diamond alimfanyia hivyo sijui kwa vile dada alikuwa underground bado sijajua....
ikafika kpindi diamond akamuacha Hawa kimapenzi na kimziki na sahizi venyewe yupo na Zari sijui kama atakua ana mkumbuka Hawa lakini diamond kwa hili akumbuke aliko toka amkumbuke hawa tuache unafiki basi hata bila hvyo amlipe kwa kazi walio fanya hata kama ni elfu hamsini maana hawa hajaambulia chochote zaidi ya kuwa nae kimahusiano!
Kwa hakika unayonena Danya Kunaitajika support ili mwenzie waliyetoboza nae pia apate nafasi ya kusimama japo kiuchumi kwa namna ya kawaida kabisa...sio lazima afike kiwango cha juu sana lakini anaweza kumfanya ajitegemee katika level nyingine kiuchumi.
Mungu uwa anamakusidi yake pale anapo yaleta mafanikio mikononi mwetu, wakati mwingine utufanya pia ni njia ya watu wengine kusimama kupitia mlango wako....lakini unapoufunga wakati msaada wa kufungua mlango aliufanya huyu Dada pia kwa namna fulani upunguza bahati, na kama kweli upande wa Diamond ukawa unahusika kutokutoa Support ambayo ilihitajika kwa nguvu na mali kumfanya Hawa nae awe na kijishughuli chake ambacho Diamond akisimama pembeni anajiona ni muhusika wa mafanikio yake kama yeye Hawa anavyojiona ni muhusika wa KUTOBOZA kwa Diamond.
Kwa aibu na masikitiko level aliyofika Diamond kama Nationa Icon eti hana Manager Mahusiano [PR]kama team.Manake mfano kwa jambo kama hili aliitajika mtu toka pande ya Diamond kulielezea hili kwa ufasaha mfano kuwa Diamond uenda alishachukua hatua za kumwinua mwenzie huyo wa mtobozo wa maisha yake kimafanikio akiwa ni Mpenzi wake pia wakati wa kuhussle.Kupitia PR uenda Diamond angetueleza bidii ambazo alishafanya katika kumpigania Hawa kusimama.mfano
1: Labda alishapata kumsaidia kwa namna moja au nyingine,
2: Au alishamsaidia kuingia studio na kurekodi Wimbo
Diamond msaidie Hawa kesho na kesho kutwa utajiwekea nafasi njema wakati wa Rise & Fall when you in way down, watu wakikumbuka ulivyomsaidia Hawa basi wanakuweka kwenye kundi la Legandary....Ni vyema kumuiga Dully Skyes japo sipendi haiba yake [Personality] lakini napenda sana Matendo yake kwa Wanamziki Chipukizi. Dully skyes amewainua wengi na leo hii ni wasanii wakubwa sana kama Mr Blue, Young D na wengineo wengi tuu...Na ndio maana anaonekana kuwa bado ni Legendary wa Uhakika na anakubalika pia.Lakini uenda kwake hisani anayowatendea walio mzunguka ndio inamjenga kumweka hapo alipo dully skyes.
Leo Diamond unaweza kuwa ndiye Top Iconn wa Taifa hili kwenye nyanja ya Muziki, lakini kumbuka kesho na kesho kutwa Taifa litapata Sauti nyingine Mpya toka labda Sangamwalugesha [wewe ulitoka Mbagala] mkoani Shinyanga akaibuka na Sauti ya ajabu kama chiruku na ikavuta Watanzania kwa ajabu, kisha kwa asili ya ulimwengu [Nature] itabidi umkabidhi kijiti bila kupenda.Hiyo ndio inaitwa RISE AND FALL -Craig Davi kwamba kuna kipindi ufika aliye namba moja inabidi atelemke apishe wengine...walikuwapo kina Pelle,leo kuna kuna kina Mess, Kulikuwa na kina Tyson leo kuna wakina Maywether.Yote hiyo ni maumbile ya kanuni Mungu alizo tuwekea kibinadamu cha msingi ni kujua jinsi ya kuishi nazo na kujianda kwa POSITIVE side.
Ukisimama ukambeba HAWA toka aliko na kumwinua kwa kumpa mradi wowote na Watanzania wakaona umempa mradi, iwe ni Saloon ya Kisasa, au Duka la Nguo, basi kesho na kesho kutwa Hawa akilinywa Duka ilo au Saloon hiyo basi watanzania watasimama kukumbuka fadhira zako kwake kuwa mtobozo wako wakati unatokelezea kwa mara ya kwanza ulikusupport nawe pia uliusupport pale ulipokuwa unataka kudondoka lakini umeshindwa kusimama wenyewe kwa kuendekeza mapombe na starehe zilizo mwangusha mara ya kwanza kufikia kupewa ujauzito na bwana aliyekimbia.
Diamond mfanye Hawa ni Dada from anaother Mother, itakujengea Heshima sana,, na kwa heshima hiyo itakujenga sana pale yeye atapakokuwa anastawi umma unajua kuna mkono wa Diamond nao ulishiriki kumludisha Binti kwenye msimo Mwema wa kimaisha [Binadamu wanakosea, uenda alichagua watu wasio sahihi kwenye maisha yake, mpe nafasi asahihishe kosa lake].
Ni kwanini umsaidie Hawa!!! ukweli unajulikana nyimbo uliyoimba nae ndio iliyowainua na kuwavuta Watanzania kwa udhati kabisa na kwa huruma ya ujumbe uliobebwa ndani ya wimbo ule ulivuta Hisia za wengi na kuwainua hsa wewe kukuweka kwenye RAMANI kuwa kuna kijana wa KItanzania anitwa Diamond ana wimbo wenye maudhui yanayovuta hisia za maisha kwenye kutafuta.Na kama pia alikuwa ni ka kipozea ni vyema pia kukumbuka kuwa kwenye maisha ya wanaume wengi mwanzoni wakati wanatafuta maisha upita mikononi mwa baadhi ya mabinti ambao kwa namna fulani walikuwa supportive sana kwenye mafanikio yao japo hawa kuwaoa mabinti hao, kwa hiyo Diamond kwa swala hilo hatakuwa wa kwanza kutomuoa Hawa, lakini anapaswa kutambua mchango wake, wanasema kwenye mafaniko ya mwanaume pembeni yake kuna mwanamke shujaa.Ndio kusema HAWA kwa Diamond hakuwa na GUNDU na ndio maana Diamond alitoka.
Sasa enzi zile za kuhussle Hawa alikuwa ni Mwanamke pembeni yetu, TUSIMTUPE , japo inajulikana kwa wanaume wote kuwa uwa tunapenda wanawake warembo ilo ni dunia nzima linatambulika sana tu.Sasa kwa kuwa HAWA hatoshi kwenye viwango vile vya Warembo wa hadhi tuliyofika basi awekwe kando lakini apewe heshima na kusaidiwa pale anapoitaji Msaada.
Inawezekana alipotoka na uwenda alimchafua kwa wimbo wake wake wa majibu ya kuludi kuona wana kwa kuwa anakula Starehe na Wanawake Warembo hiyo ilikuwa ni sanaa na uenda alilubuniwa au shawishika kuimba vile akitegemea atatoka nae...Lakini kwa kuwa wema aulipwi kwa ubaya msaidie asimame one day uko mbeleni utajipima kuwa ulipata kufanya jambo jema kwa mtu mmoja wa karibu.Manake life is full of Surprise...!!! Maisha yanastajabisha sana LOVE EACH OTHER.
Ombi langu kwa Diamond ni kuwaagiza wasaidizi wake wamtafute na kuanza kumsiaidia kumluisha kwanza kwenye hali ya kawaida toka kwenye msongo [desperate] na kumfanya aludi kwenye uhalisia, kwa kumpa mahitaji ya msingi na kuanza kumuexpose kwenye kwenye Ulimwengu mpya ambao ataonekana kushabiana nao na kuacha ULEVI ambao ulikuwa ni ESCAPING GOAT [MASK] ya ukweli wa kushindwa kwake na kuona njia ya kufanikiwa ni kuwa mlevi.Hivyo bidii za kumludisha kwenye uhalisia kwa kumjali na kumpa maitaji ya msingi ya yeye na mwanae kutamfungua akili...
Kisha atafutiwe kijikazi cha kumweka bussy uku Diamond akimpima na kutathimini nini cha kumfanyia kumsaidia yeye na Mwanawe...akijilizisha kuwa katosha kujisimamia basi ampe hicho kitakacho msimamisha kama HAWA.Kama ni Saloon ya ususi au ni Duka la Nguo [Botique] basi amkabidhi mbele ya Watanzania kisha watanzania watamuhukumu HAWA kwa hatua zikazofuata kama ataamua kuludi kwenye Pombe na Kulinywa Duka au Saloon au atatia bidii na kujikuta anafungua jingine na jingine zaidi na kuwa ametusua kama ndoto zake zilivyomtuma enzi izo kuwa Diamond akitoboza basi na yeye ametoboza zitakuwa zimetia kiana.