Hawa: Wimbo wa 'Nitarejea' wa Diamond nauchukia sana, Umeniharibia maisha yangu

Hawa: Wimbo wa 'Nitarejea' wa Diamond nauchukia sana, Umeniharibia maisha yangu

Diamond alitambulishwa na wimbo wa Nenda Kamwambie na baadae Mbagala kwahiyo si kweli hata kidogo kusema kwamba NItarejea ndio ulimtoa! Nenda Kamwambie ilitoka mwaka 2009 na huo wimbo ulimpatia tuzo tatu za Kilimanjaro na kuwa msanii wa kwanza kuzoa tuzo nyingi kwa wakati mmoja ambapo alichukua tuzo ya Best Upcoming Artist, Wimbo Bora wa R & B pamoja na Wimbo Bora wa Mwaka!

Fanya utafiti kidogo tu uulize watu kumi wangapi wanaujua nenda kamwambie na wangapi wanaujua nitarejea ndio uje kucomment hapa. Halafu hiyo si hoja ya msingi. Hoja ni Diamond ku-consider contribution ya huyu Hawa. Unfortunately both of us hatujui mkataba wake na huyu Hawa ila inavyoonekana alimlipa peanut. Hivyo hoja ni kuwa afanye consideration ya kum-boost kama anavyowafadhili watu wengine ambao huenda hawana mchango wowote kwenye muziki wake bali ni kurudisha part ya income yake kwa jamii basi mwanajamii mmiojawapo ni Hawa ambaye angalau kuna hata justification.
 
Huyu dada inabidi apate watu wa kumshauri kuhusu masuala ya mikataba. Mikataba haina mambo ya kujuana ni mnalipana kwa mujibu wa mkataba na mabo yanaishia hapo. Suala la yeye kuwa na maisha ya dhiki si majukumu ya Diamond. Hapa angeleta kesi kwamba Diamond kaenda kinyume na mkataba wao hapo angeeleweka, lakini kama hakuna kipengele chochote cha mkataba kilichovunjwa basi ajilaumu mwenyewe kwa kushindwa kuendeleza kipaji chake.
 
nyimbo zilizomtoa diamond ni kwamwambie na mbagala, sio nitarejea. Anyway Diamond hujafanya fair kutompa chochote hata kama hakukuwa na mkataba, ni ubinadam tu. Nawewe Hawa hicho hakiwez kuwa kigezo cha kufail maisha, tafuta kingine
 
Mm ni napenda kazi anazo fanya diamond na kila kitu kuhusu mzk wake lakini kwa hili hapa diamond amkumbuke huyo Hawa! Hayo malalamiko hayajaanza leo toka kipindi kile diamond ameenda "zizu fashion" kununua nguo na ana mkuta hawa akiwa anauza nguo huku akiimba,siku ya pili tena diamond anarudi anamkuta tena Hawa

ndipo anampenda na kuomba kufanya nae kazi Hawa bila hiyana anakubali na kufanya nae wimbo wa nitarejea wakaenda mbali zaidi wakaingia kwenye mauhusiano( kipindi kile haikuvuma coz diamond alikuwa bado hajawa diamond wa sahizi) ndipo diamond anafanya nae ngono huyu dada

,wakawa na show sikumbuki ni show gani kama sio kil.awards bas BSS kwenye mazoezi diamond alikuwa hata hampi nauli huyo dada ya kufikia mazoezini kila kitu Hawa alifanya kwa gharama zake katika maandalizi yote ya show kwenda na kurudi! Wakafanya bonge moja la show lakini Hawa hakuambulia hata sent ya malipo ya show! Ikawa kama kafanya bure hivi sijui kwann diamond alimfanyia hivyo sijui kwa vile dada alikuwa underground bado sijajua....

ikafika kpindi diamond akamuacha Hawa kimapenzi na kimziki na sahizi venyewe yupo na Zari sijui kama atakua ana mkumbuka Hawa lakini diamond kwa hili akumbuke aliko toka amkumbuke hawa tuache unafiki basi hata bila hvyo amlipe kwa kazi walio fanya hata kama ni elfu hamsini maana hawa hajaambulia chochote zaidi ya kuwa nae kimahusiano!

Nonsense.... 😱😱😯
 
Hebu wadau tupieni picha yake tumuone muonekano wake wa sasa.Simpatii picha kama mnasema kwasasa kachoka atakuwa anaonekanaje maana wakati hajachoka tu wakati wa video ya wimbo huo alikuwa anaonekana kachoka mbaya
 
asimlaumu mtu hapo kwani diamond ndiye aliyemtia mimba na kumkimbia?...ajipange kufanya collabo siyo iwe kigezo cha kumpa mtu lawama kuwa hakusaidii.
 
Dimondi mlipe dada hawa mkwanja wake,ungemlipa hela hiyo asingebabaika na wanaume mpaka wamempa mimba,mlipe fedha zake za kolabo,ni kama Nelly na Kelly Dillema ule wimbo wote wanafaidika ila wewe unafaidika peke yako tu.

msaidie muende mahakamani akadai haki yake. humu mitandaoni hata pata kitu.
 
Mlikubaliana nini wakati anakuambia ufanye kazi hiyo?
 
Kumbe walioharibiwa si kina wema tu, ila dango domo rudisha fadhila bwana kabla mungu unaemtumikia hajakukana maana ulishamkataa MUNGU wa Ibrahim
 
Khah!!!!!!!!!!! kumbe tangia alivyoenda mjini hajarejea tena kijijini??????????kweli mjini shule
 
Hebu wadau tupieni picha yake tumuone muonekano wake wa sasa.Simpatii picha kama mnasema kwasasa kachoka atakuwa anaonekanaje maana wakati hajachoka tu wakati wa video ya wimbo huo alikuwa anaonekana kachoka mbaya
5715307542ce4b3ca6d94014dcaea4d1.jpg
 
Nahisi mleta mada yupo ile timu ya Tembo...diamond hahusiki kwa lolote hapo kama anamdai aseme maan alipewa chake...sasa kuharibikiwa na maisha vinahusiana nin na wimbo..mwenye akili ataelewa huyo mdada hayupo sawa psychologically .
 
Back
Top Bottom