Haya bei hizo kwa wale wasafiri wa ATCL

Haya bei hizo kwa wale wasafiri wa ATCL

Uchumi wa Kati tutaufikia, Usafiri wa muda mfupi kwenda mwanza na Arusha unafanya biashara na kurudi Dar siku hiyo hiyo.

Hapa kazi tu .

yani kama tungenunu
Hiyo nauli ya 30,000 hata Canada hizi ndege zilikotoka hakuna!
kwanini isiwe hivyo? Mafuta yameshuka kwenye soko la dunia. Pia serekali haitatoza kodi hayo mafuta. Viwanja vya ndege ni mali ya serikali. Inawezekana iwapo tu tutakuwa wazalendo
 
Muache uongo na wengine msidanganyike kirahisi jamani. ATCL ni shirika, haliwezi kutoa tangazo la kihuni kama tangazo la muvi kwenye vibanda umiza vya uswahilini.
 
Uchumi wa Kati tutaufikia, Usafiri wa muda mfupi kwenda mwanza na Arusha unafanya biashara na kurudi Dar siku hiyo hiyo.

Hapa kazi tu .

Unatupigia kelele hapa kumbe kitu chenyewe ofa!!!!? Weka bei halisi badala kutuwekea ofa hapa.
 
dadeq. akat fast jet ukiwah kukata unapata had tiket za 40,000/=. 2 weeks bfore unapata tiket za 70,000/=. laki na sitini wapande wenyewe
 
Hiyo ni kwenda na kurudi au kwenda tu?
Hiyo ni kwenda na kurudi. Kumbuka gharama ya mafuta kwenda na kurudi Mwanza ni shs million 2 tu. ATCL wamekodisha hizo ndege bure toka serikalini, hakuna walichowekeza kwenye hizo ndege.ATCL linamilikiwa 100% na serikali hata mishahara yao serikali inaweza kuwalipa ikiamua ila kwa sasa itatokana na faida wataoipata baada ya kutoa running cost.

Ndege ni brand new hivyo running cost ni ndogo sana. Ni bei ya mafuta tu na service ya kawaida. Kama Fast jet waliweza kutoza shs 70,000/ Dar - MZA return ticket tena kwa jet engine, kwa nini ATCL ishindwe kutoza Shs 160,000/ Dar- Mza Return tena kwa bombardia engines?

Hivyo bei ya Shs 80,000/ kwa one way Dar Mwanza ni very reasonable. Ni mara mbili tu ya nauli ya basi, hivyo mwananchi wa kawaida ataweza kuimudu. Wa mabasi nao wanaweza wakapunguza kidogo nauli au angalao watasita kuipandisha. Mambo yatanoga zaidi treni zetu zitakapokuwa za umeme baada ya standard gauge kumalizika maana safari ya Dar -Mza itachukua masaa matatu tu. Hadi raha.
 
yani kama tungenunu
kwanini isiwe hivyo? Mafuta yameshuka kwenye soko la dunia. Pia serekali haitatoza kodi hayo mafuta. Viwanja vya ndege ni mali ya serikali. Inawezekana iwapo tu tutakuwa wazalendo
Pole.
 
Hizo bei kma ni kweli hazina tofauti na PW pia fastjet bado wko chini kuna mpka 120,000 oneway dar to mwz
 
Go and return za ndege haziko hivyo mkuu, ikiwa one way ni 160,000, kwenda na kurudi inaweza kuwa 270,000
160, 000 kama siwahi sanaa nitapanda Yutong Tu Luxury ... Haya mapanga boy hata Raha hutoona kwa hela hiyo yoteee bora upande ya 45000 na TV unaona
 
Back
Top Bottom