Refa akiwa Mwanamke yule Dada wa Singida ( ambaye ni mwana Simba SC lia lia ) kwa 100% Simba SC anashinda.
Refa akiwa Mwanaume ( hasa Aragija ) ambaye pia Kiuhalisia ni mwana Yanga SC lia lia kwa 100% Yanga SC inashinda.
Refa akiwa ni Mwanaume ( hasa Eli Sasi ) Mechi itaisha Sare kwakuwa huyu huchukua Mlungula kote kote na hupenda Kubalansi Derby kwa kuona Aibu japo kiuhalisia ni mwana Simba SC ila ni muoga muoga.
Refa akiwa ni tofauti na hawa Watatu niliowataja hapa kwa Majina ila Fourth Official akawa ni Mwanamke basi kwa 100% Simba SC itashinda.
Hata hivyo pamoja na GENTAMYCINE kuwaletea yote haya ila wana Simba SC Wenzangu mtanisamehe na msichukie ila ukweli ni kwamba Kindumba ( Kiuchawi ) kuna mahala Yanga SC wametukamata na hadi muda huu naandika huu Uzi matokeo niliyonayo ni kwamba Simba SC itafungwa Goli 1 kwa 0 au Magoli 2 kwa 1.
Hata hivyo Juhudi za Kiutamaduni ( Kindumba ) zinaendelea ili kubadili matokeo ila tatizo Kubwa ni muda wa Saa 11 Jioni ambapo Jini la Yanga SC ndiyo huwa Hatari na Kali na la Simba SC huanza kuwa Imara kuanzia Saa 12 Jioni na hasa Saa 1 Usiku.
Na kwa Yanga SC wana Wataalam ( Waganga ) wengi ila kwa Mechi zote za Simba SC humtumia Mganga wao Hatari ambaye ni Mjomba wake na Kiongozi wa Simba SC Murtaza Mangungu ambaye pia ndiyo Mganga Mkuu wa Kiongozi Mmoja mkubwa, Mawaziri Watatu na Wabunge Tisa.
Kwa Simba SC Kesho Mzigo ( Ndumba ) ataibeba John Boko au Kibu Denis na kwa Yanga SC Ndumba ( Mzigo ) atabeba Mudathir Yahya au Bakari Mwamnyeto.
Jamiiforums Captain GENTAMYCINE I'm back. Na Mimi ndiyo GENTAMYCINE The King!!!!!