joto la jiwe
JF-Expert Member
- Sep 4, 2017
- 26,117
- 46,617
China donates 30,000 bags of rice to Kenya, Twitter users outraged | Africanews
A number of Kenyans are, however, not enthused by the news of donation. Most of them slammed the government for failing citizens so badly that Kenyans have to depend on food donations.
Wakati Waziri wa Ugatuzi akichekelea kupokea mchele wa msaada toka China ili kuokoa maisha ya mamilioni ya wakenya walio katika hatari ya kufa kutokana na njaa kubwa inayoikumba Kenya, wananchi wengi wa Kenya wamelichukulia kama ni kitendo cha aibu kwa taifa Lao kuendeleza tabia ya kuomba na kupokea misaada ya chakula.
Kwa mujibu wa Waziri huyo ni kwamba, nusu ya nchi ya Kenya inakabiliwa na njaa hivyo kuhitaji msaada wa chakula haraka. Tangu Kenya ijipatie Uhuru wake, janga la njaa ni sehemu ya maisha ya wakenya, na wengi wamepoteza maisha kwa sababu ya njaa.
Rais Uhuru Kenyatta alikiri kwamba, Kenya haina uwezo wa kujilisha hivyo kutegemea misaada ya chakula, na kwamba haki hiyo itaendelea kuikumba Kenya kwasababu idadi ya watu inazidi kuongezeka na ardhi iliyopo inazidi kupoteza uwezo wa uzalishaji chakula.