DELETED ACCOUNT
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 9,805
- 15,476
Nimeangalia kwa umakini haya marekebisho ya ratiba naona siyo rafiki kabisa kwa Simba. Sijajua ushirikishwaji wa wadau wa hizi timu upoje kabla ratiba haijatolewa au kufanyiwa marekebisho ila naona kuna mapungufu makubwa.
Tukianzia, nimeshangaa kuona game ya KMC vs Simba ya tarehe 11/05 bado ipo pale pale. Hii mechi ilistahili iahirishwe hasa baada ya KMC kuipeleka Tabora, sehemu ambapo hamna hata uwanja wa ndege na hapo hapo Simba ina mechi ya fainali Morocco baada ya siku 6. Tukumbuke kule nchi za Kaskazini ni kipindi cha ubaridi kwa hiyo ningetegemea Simba ingeenda siku kadhaa kabla ili kuzoea hali ya hewa.
Tukija mechi ya Singida imepangwa siku 3 tu baada ya fainali ya pili kwa Mkapa. Aliyepanga hivi alikuwa anawaza nini? Hapa Simba ilistahili ipewe walau siku 3 za mapumziko, hata kwa heshima tu ya kile ambacho imeifanyia nchi msimu huu.
Tena baada ya siku 3, Simba na Singida inabidi zikutane tena katika nusu fainali ya CRDB huko Manyara, mji mwingine ambao hauna uwanja wa ndege.
Simba ingeweza kukubali kucheza hizo mechi walau mbili bila uwepo wa wachezaji wake walio timu ya taifa na pia Singida na KMC hawana wachezaji kwenye timu za taifa. Hizi mechi mbili za ligi na ile ya CRDB zingepewa gape zikachezwa hata wakati wa international break kama utaratibu unaruhusu.