Upo sahihi sana hapo kwa wafuasi wa Magufulism, ila huyo Tundu Lissu ana mambo ambayo binafsi yananifanya nisimkubali tena kamwe na naamini wapo wengine wengi wasioweza kumpigia kura kwasababu ya mambo hayo;
i. Alihusika kumpokea na kumsafisha Lowassa kipindi Mbowe anabadilisha gia angani 2015 na alishindwa kujibu hoja za Slaa akaishia kumu attack personally.
Kwangu binafsi ule unasimama kama uhuni mkubwa kabisa wa kisiasa niliwahi kushuhudia kwenye maisha yangu na kuanzia hapo simuamini tena huyo Tundu Lissu na cream yote ya Chadema especially ya wakati huo ispokua dr. Slaa,
ii. Kuendelea kumshambulia Magufuli ambae alishalala kitambo.
Hii anajifunga magoli mwenyewe aidha kwa kujua ama kwa kutojua kwasababu;
-Pana vitu vingi sana vya kuongea kwa sasa ambavyo vinaweza kumpa kuaminika kwa watanzania ila humsikii akiviongelea, tazama hata wakati wa ishu ya bandari, yupo Chato halafu anaendelea kumsema vibaya Magufuli tena mbele ya watu wake badala aelezee ubaya wa huo mkataba, sasa unajiuliza kama hajalipwa na watawala kufifisha hiyo hoja basi huenda atakua sio mzima kichwani kwasababu whatever it is he was doing was accomplishing the opposite,
-Watanzania wengi hawataki kabisa kusikia Magufuli anasemwa ama kutendewa vibaya na mtu yeyote, unaweza usione nguvu yao kwa sasa kwasababu hawajapata mtu wa kuwasemea ambae wanaona anaweza kuvaa viatu vya Magufuli vizuri, wakimpata tutashangaa,
-Lakini hata anayomtuhumu nayo yangekua kweli, inasaidia nini kuendelea kumsema wakati sio anaeshindana nae kugombea uongozi??
Pia mwisho, kama nipo sahihi hana mtoto hata mmoja ambae ni raia wa Tanzania, hata mke wake nakumbuka kuna interview moja alisema aidha ameshapata uraia wa Belgium ama amepata permanent residence permit ya huko, sasa hii unawaelezeaje watanzania kwamba upo nao na utawapigania mpaka mwisho kama mfano hatuuoni kuanzia kwa familia yako?
Kwa haya na mengine mengi naona hata yeye hafai tena hafai kwa mbali kabisa.