Haya makundi ya Bongo Fleva yalitupa raha sana sisi Wahenga

Haya makundi ya Bongo Fleva yalitupa raha sana sisi Wahenga

Planet 2000 - Bab' Kubwa



Hard Blasters Crew - Mamsap. Mashairi ya Nigga Jay ( Siku hizi Profesa Jay) humu angeimba msanii wa kizazi hiki tungesema hana maadili 😀 kumbe wahenga pia hatukuwa mbali



Big Dog Posse - Majobless

 
Kulikuwa radio presenters waliupigania sana mziki wakina Mike mhagama,taji liundi, soso b,Sebastian maganga

Ova
SOS B - Kukuru Kakara Zako... Huu ndo wimbo ulionishawishi rasmi niikubali Hip Hop yetu. Kama sikosei hii ilitoka kabla ya Chemsha Bongo ya Nigga Jay na nafikiri huyu jamaa aliwashawishi hawa wengine wengi wa enzi zile waingie kwenye game. Kila kitu kipo humu, ujumbe wa kutofanya ngono bila condom, kuwa na msanii mwingine kuitikia na kurudia maneno (ad libs) na kutamka neno kwa herufi syle ya 'A to the... (R nenda A nenda P (RAP)). Kifupi huu wimbo niliukubali sana

 
Planet 2000 - Bab' Kubwa

View attachment 1782313

Hard Blasters Crew - Mamsap. Mashairi ya Nigga Jay ( Siku hizi Profesa Jay) humu angeimba msanii wa kizazi hiki tungesema hana maadili 😀 kumbe wahenga pia hatukuwa mbali
View attachment 1782347


Big Dog Posse - Majobless

View attachment 1782317
Bdp kuna kipindi nlikutana na drez chief
Anakunywa mipombe ya kienyeji yaani
Hali yake ilikuwa syo kabisa
Drezchief alifanyaga sana production na mixing pale sound crafters
Tatizo bdp maisha fulani ya kisela walizidisha sana

Ova
 
Bdp kuna kipindi nlikutana na drez chief
Anakunywa mipombe ya kienyeji yaani
Hali yake ilikuwa syo kabisa
Drezchief alifanyaga sana production na mixing pale sound crafters
Tatizo bdp maisha fulani ya kisela walizidisha sana

Ova
Sad sana
 
Hizo ni bendi sio bongofleva
Nilikuwa nazungumzia nyimbo za enzi za Wahenga, kama ulinisoma vizuri nililiweka wazi hilo.
Hata studio za Mawingu wakati zinaanza hazikuwa enzi za Wahenga, that's what I was clarifying.
 
Nilikuwa nazungumzia nyimbo za enzi za Wahenga, kama ulinisoma vizuri nililiweka wazi hilo.
Hata studio za Mawingu wakati zinaanza hazikuwa enzi za Wahenga, that's what I was clarifying.
Msondo show zao nlikuwa naenda sana

Ova
 
Kwa kipindi cha miaka ya 90’s mpaka 20’s ilikuwa ili msanii uweze kutoboa lazima ujiunge kwenye kundi lolote la muziki na ndio maana kwa kipindi hicho idadi ya makundi ilikuwa kubwa na yalidumu kwa muda mrefu,walikusudia kuifanya Tanzania kuwa "Taifa la hip hop’’, vijana kuondokana na maisha ya mtaani.

Haya ni baadhi makundi ambayo yalifanikiwa kwa kiasi kikubwa kuukuza muziki wetu na kuacha alama mpaka sasa.

1. Kwanza Unit (KU Creaw).

Kwanza Unit lilikuwa kundi la mwanzo kabisa la muziki wa hip hop na lilianzishwa mwaka 1990, liliundwa kutokana na muunganiko wa makundi matatu, KBC, Eazy-B, Fresh-G na D-Rob ni baadhi ya wasanii wa KUC ambapo awali walikuwa wana-rap kwa kiingereza lakini baadae walibadilika na kutumia Kiswahili.

2. Gangwe Mobb.

Temeke Mikoroshini ndiko maskani ya kundi hili yalipatikana na lilianzishwa mwishoni mwa miaka ya 90 punde baada ya Kwanza Unit, Mr. II na wengineo kuchangia muziki wa hip hop wa Kiswahili nchini kujipatia umaarufu, huku Inspector Haroun na Luteni Karama ndio walikuwa wanakikundi.

3. Hard Blasters.

Ujumbe wao kupitia muziki ulibadilisha mtazamo wa jamii na kuamini kuwa kufanya muziki sio uhuni ni ajira/kazi.
Fanani, Crazy One, Professor Jay, KC1, Trigger F na Tuff Jam waliunda kundi hilo na waliachia album kadhaa “Funga kazi, Tuko nyuma kimaendeleo nakadhalika

4. TMK Wanaume Family.

Ni moja ya kundi lililoleta mapinduzi makubwa kwenye muziki wa kizazi kipya tangu kuanzishwa kwake Septemba 16, 2002 mjini Mwanza, wakati wa uzinduzi wa album ya Juma Nature ‘’Ugali’’ mpaka sasa limejijengea umaarufu mkubwa kutokana na mtindo wao wa kucheza ujulikanao ‘Mapanga’.

5. Chemba Squard.

Hili ni miongoni mwa makundi yaliyokuwa na wasanii wenye vipaji na uwezo wa hali ya juu sana tangu walipoingia rasmi sokoni mwaka 2000, liliundwa na Noorah (Baba Stylz), Dark Master, The late Mez B na Mangwair, wote walikuta shule ya Sekondari Mazengo Dodoma.

6. East Coast Team.

Linaundwa na wasanii Ay, Mwana FA na Crazy GK ambao walifanikiwa kwa kiasi kikubwa kuleta mabadiliko kwenye game kuwa ya kisasa zaidi, makazi yake ni Upanga mashariki.

Yapo mengi sana wahenga wenzangu mnaweza kuendelea kuyataja karibuni sana wahenga.
Hao HARD BLASTERS walitisha sana.....vibao vyao kama

Tuko nyuma
Mwokozi
Fanani
Mamsap
Eee Mola

Mwenye hizi ngoma naomba, you tube naona wimbo wa Fanani na Mamsap tu
 
Alicopy nyimbo ya vanilla ice
Aise mzee unaelekea una collection
Za zamani

Ova
aaahaaaa...

'kuna kitu kimenikaa moyoni sasa nimeamua kukitoa mdomoni...'

nadhani ndiye huyu mwamba iliimba kwa tune ya 'ICE ICE BABY'
 
Hao HARD BLASTERS walitisha sana.....vibao vyao kama

Tuko nyuma
Mwokozi
Fanani
Mamsap
Eee Mola

Mwenye hizi ngoma naomba, you tube naona wimbo wa Fanani na Mamsap tu
Kuna show yao moja walipiga sleep way enzi za summer jam ilikuwa balaaa
Kwanza hilo nyomi

Ova
 
aaahaaaa...

'kuna kitu kimenikaa moyoni sasa nimeamua kukitoa mdomoni...'

nadhani ndiye huyu mwamba iliimba kwa tune ya 'ICE ICE BABY'
Yah
Na pia wakina kolumba mwingira,othman njaidi Hahaha

Ova
 
Bdp walikuwa watoto wa kinondoni shamba
Enzi zile shw zao lazima watuinvite

Ova
Enzi hizo niko A-Town (Siku hizi A-CITY aka R-CHUGA aka Chugastan aka Chugamaica) bongo flava naipata redioni tu na kwenye TV 😀 😀 . Niliendaga kwenye Fiesta moja tu, nakumbuka msanii wa nje alikuwa 2face Idibia (2baba) na tulikuwa na vijana wa Arusha wanajiita 'Wana Apolo' kwenye stage walivyopanda walifunika sana na style yao kama ya TMK Wanaume 'mapanga shaaa' 😀😀
 
Kuna show yao moja walipiga sleep way enzi za summer jam ilikuwa balaaa
Kwanza hilo nyomi

Ova
Wale jamaa walikuwa vizuri sana, ila niliwahi kusikia Fanani alijiingiza kwenye ngada hadi akawa Teja.....sijui kama alirecover
 
Back
Top Bottom