Haya makundi ya Bongo Fleva yalitupa raha sana sisi Wahenga

Haya makundi ya Bongo Fleva yalitupa raha sana sisi Wahenga

Enzi hizo niko A-Town (Siku hizi A-CITY aka R-CHUGA aka Chugastan aka Chugamaica) bongo flava naipata redioni tu na kwenye TV 😀 😀 . Niliendaga kwenye Fiesta moja tu, nakumbuka msanii wa nje alikuwa 2face Idibia (2baba) na tulikuwa na vijana wa Arusha wanajiita 'Wana Apolo' kwenye stage walivyopanda walifunika sana na style yao kama ya TMK Wanaume 'mapanga shaaa' 😀😀
Jcb na chindoman walikuwaga waanangu sana....
Nakumbuka kuna siku tulikuwa block41 alikuja chindo nlikuwa kwa mwana mmja anaitwa chis,sasa chindo akawa anasema
Anawaza sana ....anawaza
Ahh baada ya siku kadhaa nkasikia katoa goma linaitwa nawaza haha
Jamaa alikuwa gifted sana

Ova
 
Wale jamaa walikuwa vizuri sana, ila niliwahi kusikia Fanani alijiingiza kwenye ngada hadi akawa Teja.....sijui kama alirecover
Fanani alijiingiza kwenye madawa ila kna wakati alikuwa anapigana kutoka ila muda sana hajaonekana
Hata kwanza unit kna mmoja wao sjui ni y thang yule au nani naye aliijingizaga kwenye madawa yaani nomaa

Ova
 
Job na chindoman walikuwaga waanangu sana....
Nakumbuka kuna siku tulikuwa block41 alikuja chindo nlikuwa kwa mwana mmja anaitwa chis,sasa chindo akawa anasema
Anawaza sana ....anawaza
Ahh baada ya siku kadhaa nkasikia katoa goma linaitwa nawaza haha
Jamaa alikuwa gifted sana

Ova
Bonge la track lilikuwa aisee
 
Fanani alijiingiza kwenye madawa ila kna wakati alikuwa anapigana kutoka ila muda sana hajaonekana
Hata kwanza unit kna mmoja wao sjui ni y thang yule au nani naye aliijingizaga kwenye madawa yaani nomaa

Ova
Fanani alikuwa Magomeni kama sijakosea
 
Siku hzi mziki hKuna kitu makelele tu

Ova
Nashukuru siku hizi vijana kwenye sanaa wanaonesha kujitambua na kupiga hela na kujitahidi kufanya ya maana na pesa wakizipata. Diamond, Harmonize, Rayvanny, Mesen Selekta, Nahreel na wengine wengine wanamiliki studio zao wenyewe na wanaishi kwa kujitegemea na zaidi ya hapo wamekuwa wakutegemewa. Tofauti na zamani.
 
Nashukuru siku hizi vijana kwenye sanaa wanaonesha kujitambua na kupiga hela na kujitahidi kufanya ya maana na pesa wakizipata. Diamond, Harmonize, Rayvanny, Mesen Selekta, Nahreel na wengine wengine wanamiliki studio zao wenyewe na wanaishi kwa kujitegemea na zaidi ya hapo wamekuwa wakutegemewa. Tofauti na zamani.
Zamani waliimba vzr sema wasani walipata pesa kdg,wengine walishindwa kutunza pesa
Mr 2 naona ndy alikomaa

Ova
 
Nakumbuka hizi nyimbo tulikuwa tunazisikia sana kupitia Radio One na Clouds FM... Tukiwa Form One... Iyunga Tech. Mbeya.. Mwanzoni mwa miaka ya 2000....

List ya misongi unaipata katika gazeti la Ijumaa... La mtalaam Eric Shigongo...

Kweli siku zinasonga....
 
Tunataabika ya Mabaga fresh [emoji91][emoji91][emoji91]
 
Bush part by solid ground family [emoji91][emoji91][emoji91]
 
Kamanda kama kamanda by Daz Nundaz [emoji91][emoji91][emoji91]
 
Barua kama barua by Daz Nundaz [emoji91][emoji91][emoji91]
 
Mwengine sajo [emoji2][emoji2]
ila hawa jamaa nyimbo zao hazijawahi kuchuja...

Kamanda
Barua
Boss
nyie watu walikua wanaimba vitu vina make sense Wallah
Nimekumbuka nyimbo za dully na
Leah
Salome izi nyimbo zilikuwa nzuri
 
AY (Mzee wa Commercial) na COMPLEX (Field Marshall) - Hawa hawakuwa kundi rasmi ila walikuwa na tabia ya kupiga collabo kali kama ilivyokuwa AY na FA au na GK. Iwe wao wawili (RAHA TU rmx, Hakuna Hatari, Muda ndiyo huu, etc) au wakiwa na msanii mwingine (Zay B kwenye 'Njoo kati', GK kwenye 'mchanga wa macho')

Naona tulipoteza msanii mkali sana kwa COMPLEX maana niliona ukimuweka na AY combo ilikuwa kali. Kuna wimbo Complex aliimba na Mturuki sijui aliitwa Bharish, unaitwa 'taifa la Bongo'. Nimeutafuta sana bila mafanikio.
 
Zamani waliimba vzr sema wasani walipata pesa kdg,wengine walishindwa kutunza pesa
Mr 2 naona ndy alikomaa

Ova
Soko halikuwa tayari aisee. Vijana wengi waliopenda muziki huu hawakuweza kuununua walitegemea redio na TV au waende kwenye shows. Digital platforms zilizopo saivi zingekuepo enzi zile nahisi wangetoboa.
Kwa kipindi cha miaka ya 90’s mpaka 20’s ilikuwa ili msanii uweze kutoboa lazima ujiunge kwenye kundi lolote la muziki na ndio maana kwa kipindi hicho idadi ya makundi ilikuwa kubwa na yalidumu kwa muda mrefu,walikusudia kuifanya Tanzania kuwa "Taifa la hip hop’’, vijana kuondokana na maisha ya mtaani.

Haya ni baadhi makundi ambayo yalifanikiwa kwa kiasi kikubwa kuukuza muziki wetu na kuacha alama mpaka sasa.

1. Kwanza Unit (KU Creaw).

Kwanza Unit lilikuwa kundi la mwanzo kabisa la muziki wa hip hop na lilianzishwa mwaka 1990, liliundwa kutokana na muunganiko wa makundi matatu, KBC, Eazy-B, Fresh-G na D-Rob ni baadhi ya wasanii wa KUC ambapo awali walikuwa wana-rap kwa kiingereza lakini baadae walibadilika na kutumia Kiswahili.

2. Gangwe Mobb.

Temeke Mikoroshini ndiko maskani ya kundi hili yalipatikana na lilianzishwa mwishoni mwa miaka ya 90 punde baada ya Kwanza Unit, Mr. II na wengineo kuchangia muziki wa hip hop wa Kiswahili nchini kujipatia umaarufu, huku Inspector Haroun na Luteni Karama ndio walikuwa wanakikundi.

3. Hard Blasters.

Ujumbe wao kupitia muziki ulibadilisha mtazamo wa jamii na kuamini kuwa kufanya muziki sio uhuni ni ajira/kazi.
Fanani, Crazy One, Professor Jay, KC1, Trigger F na Tuff Jam waliunda kundi hilo na waliachia album kadhaa “Funga kazi, Tuko nyuma kimaendeleo nakadhalika

4. TMK Wanaume Family.

Ni moja ya kundi lililoleta mapinduzi makubwa kwenye muziki wa kizazi kipya tangu kuanzishwa kwake Septemba 16, 2002 mjini Mwanza, wakati wa uzinduzi wa album ya Juma Nature ‘’Ugali’’ mpaka sasa limejijengea umaarufu mkubwa kutokana na mtindo wao wa kucheza ujulikanao ‘Mapanga’.

5. Chemba Squard.

Hili ni miongoni mwa makundi yaliyokuwa na wasanii wenye vipaji na uwezo wa hali ya juu sana tangu walipoingia rasmi sokoni mwaka 2000, liliundwa na Noorah (Baba Stylz), Dark Master, The late Mez B na Mangwair, wote walikuta shule ya Sekondari Mazengo Dodoma.

6. East Coast Team.

Linaundwa na wasanii Ay, Mwana FA na Crazy GK ambao walifanikiwa kwa kiasi kikubwa kuleta mabadiliko kwenye game kuwa ya kisasa zaidi, makazi yake ni Upanga mashariki.

Yapo mengi sana wahenga wenzangu mnaweza kuendelea kuyataja karibuni sana wahenga.
Nadhani East Coast Team kulikuja kuwa na O-Ten na Imam Abbas. Baadae wakajaongezeka madogo wengine kama Snare na wengine sikuwajua vizuri wakajiita East Coast Army
 
Back
Top Bottom