Haya makundi ya Bongo Fleva yalitupa raha sana sisi Wahenga

Haya makundi ya Bongo Fleva yalitupa raha sana sisi Wahenga

Nakumbuka hizi nyimbo tulikuwa tunazisikia sana kupitia Radio One na Clouds FM... Tukiwa Form One... Iyunga Tech. Mbeya.. Mwanzoni mwa miaka ya 2000....

List ya misongi unaipata katika gazeti la Ijumaa... La mtalaam Eric Shigongo...

Kweli siku zinasonga....
Sure,
 
[emoji122][emoji122]
GWM - Gangstaz With Matatizo
CBM - Check Bob Maarifa
BDP - Big Dogg Posse (Hili 'posse' inatamkwa 'pasi' kwa kiingereza, likimaanaisha kikundi)
SGF- Solid Ground Family
TNG -nilihisi linaamanisha Tanga Squad

Dolphin sikuwajua na Bon Cruz sidhani kama nawakumbuka 😀😀

Wazamani wengine nawakumbuka ni DEPLOWMATZ -Kina Balozi Dolasoul na Kwanza Unit, Hard Blasters na XPLASTAZ
Bon cruz waloimba Jamaa (Wanamwita kaka poa huyu jamaa, wanamwita mambo safi huyu jamaa, wanamwita mtoto wa watu huyu jamaa, sijui si riziki au ni laana huyu jamaa twakuomba tusamehe maulana)
Na Dolphin pose walikuwa wakijiita machalii wawili heat song yao Ni rafiki tu.
 
Kwa kipindi cha miaka ya 90’s mpaka 20’s ilikuwa ili msanii uweze kutoboa lazima ujiunge kwenye kundi lolote la muziki na ndio maana kwa kipindi hicho idadi ya makundi ilikuwa kubwa na yalidumu kwa muda mrefu,walikusudia kuifanya Tanzania kuwa "Taifa la hip hop’’, vijana kuondokana na maisha ya mtaani.

Haya ni baadhi makundi ambayo yalifanikiwa kwa kiasi kikubwa kuukuza muziki wetu na kuacha alama mpaka sasa.

1. Kwanza Unit (KU Creaw).

Kwanza Unit lilikuwa kundi la mwanzo kabisa la muziki wa hip hop na lilianzishwa mwaka 1990, liliundwa kutokana na muunganiko wa makundi matatu, KBC, Eazy-B, Fresh-G na D-Rob ni baadhi ya wasanii wa KUC ambapo awali walikuwa wana-rap kwa kiingereza lakini baadae walibadilika na kutumia Kiswahili.

2. Gangwe Mobb.

Temeke Mikoroshini ndiko maskani ya kundi hili yalipatikana na lilianzishwa mwishoni mwa miaka ya 90 punde baada ya Kwanza Unit, Mr. II na wengineo kuchangia muziki wa hip hop wa Kiswahili nchini kujipatia umaarufu, huku Inspector Haroun na Luteni Karama ndio walikuwa wanakikundi.

3. Hard Blasters.

Ujumbe wao kupitia muziki ulibadilisha mtazamo wa jamii na kuamini kuwa kufanya muziki sio uhuni ni ajira/kazi.
Fanani, Crazy One, Professor Jay, KC1, Trigger F na Tuff Jam waliunda kundi hilo na waliachia album kadhaa “Funga kazi, Tuko nyuma kimaendeleo nakadhalika

4. TMK Wanaume Family.

Ni moja ya kundi lililoleta mapinduzi makubwa kwenye muziki wa kizazi kipya tangu kuanzishwa kwake Septemba 16, 2002 mjini Mwanza, wakati wa uzinduzi wa album ya Juma Nature ‘’Ugali’’ mpaka sasa limejijengea umaarufu mkubwa kutokana na mtindo wao wa kucheza ujulikanao ‘Mapanga’.

5. Chemba Squard.

Hili ni miongoni mwa makundi yaliyokuwa na wasanii wenye vipaji na uwezo wa hali ya juu sana tangu walipoingia rasmi sokoni mwaka 2000, liliundwa na Noorah (Baba Stylz), Dark Master, The late Mez B na Mangwair, wote walikuta shule ya Sekondari Mazengo Dodoma.

6. East Coast Team.

Linaundwa na wasanii Ay, Mwana FA na Crazy GK ambao walifanikiwa kwa kiasi kikubwa kuleta mabadiliko kwenye game kuwa ya kisasa zaidi, makazi yake ni Upanga mashariki.

Yapo mengi sana wahenga wenzangu mnaweza kuendelea kuyataja karibuni sana wahenga.
Kuna kundi walikuwepo Suma Lee na marehemu CPwaa linaitwa Pack Lane.

2Berry wale wapemba wa Chakechake
 
Msondo show zao nlikuwa naenda sana

Ova
Ilianza ikiwa NUTA Jazz band ikakaja kuwa JUWATA Jazz band (Msondo ngoma ukiwa ni mtindo wao) baadaye ikivyokuwa bendi huru kutoka Jumuiya ya Wafanyakazi ndipo ikwa bendi ya Msondo.
 
Soko halikuwa tayari aisee. Vijana wengi waliopenda muziki huu hawakuweza kuununua walitegemea redio na TV au waende kwenye shows. Digital platforms zilizopo saivi zingekuepo enzi zile nahisi wangetoboa.

Nadhani East Coast Team kulikuja kuwa na O-Ten na Imam Abbas. Baadae wakajaongezeka madogo wengine kama Snare na wengine sikuwajua vizuri wakajiita East Coast Army
Waliokuwa consistent na focused walifanikiwa, hata kidogo upatacho ukiwa na malengo unasonga mbele.
Ukiachilia waliokwenda overseas kwa hapa bongo mifano ya Sugu, AY, Mwana FA, Professor J na Lady JD unaweza kuona maana halisi ya kuwa focused, uwezo wa kuwekeza au kutumia brand-name kupenya kwenye siasa ni mifano iliyo wazi. Wapo waliochanganyikiwa na fame na vipesa kidogo walivyokuwa wakipata wakazama kwenye maisha ya parting through and through, drugs, ulevi uliopindukia na vurugu nyingine nyingi sasa watu sampuli hizo imagine wangepata pesa kama wapatazo Bongo flavors wa sasa nadhani wengi wao tungeshazika.
 
Wale wajaruo VP ," mpenzi ungejua moyoni mwangu jinsi ninavyokuthamini"
 
Bon cruz waloimba Jamaa (Wanamwita kaka poa huyu jamaa, wanamwita mambo safi huyu jamaa, wanamwita mtoto wa watu huyu jamaa, sijui si riziki au ni laana huyu jamaa twakuomba tusamehe maulana)
Na Dolphin pose walikuwa wakijiita machalii wawili heat song yao Ni rafiki tu.
ahaaaa naukumbuka huu wimbo 🙏
 
Back
Top Bottom