The Icebreaker
JF-Expert Member
- Feb 11, 2018
- 22,278
- 65,817
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sure,Nakumbuka hizi nyimbo tulikuwa tunazisikia sana kupitia Radio One na Clouds FM... Tukiwa Form One... Iyunga Tech. Mbeya.. Mwanzoni mwa miaka ya 2000....
List ya misongi unaipata katika gazeti la Ijumaa... La mtalaam Eric Shigongo...
Kweli siku zinasonga....
School mate Wangu daz baba popote ulipo Mungu akuinue kwa kweli una kipaji sana tuBarua kama barua by Daz Nundaz [emoji91][emoji91][emoji91]View attachment 1782466
Bon cruz waloimba Jamaa (Wanamwita kaka poa huyu jamaa, wanamwita mambo safi huyu jamaa, wanamwita mtoto wa watu huyu jamaa, sijui si riziki au ni laana huyu jamaa twakuomba tusamehe maulana)[emoji122][emoji122]
GWM - Gangstaz With Matatizo
CBM - Check Bob Maarifa
BDP - Big Dogg Posse (Hili 'posse' inatamkwa 'pasi' kwa kiingereza, likimaanaisha kikundi)
SGF- Solid Ground Family
TNG -nilihisi linaamanisha Tanga Squad
Dolphin sikuwajua na Bon Cruz sidhani kama nawakumbuka 😀😀
Wazamani wengine nawakumbuka ni DEPLOWMATZ -Kina Balozi Dolasoul na Kwanza Unit, Hard Blasters na XPLASTAZ
Chief ni Wakilisha bana!Mmewasahau WAKILUSHA iliundwa na Langa Kileo, Sarah Kaisu na Witnes
Unawakumbuka Manyema Family kina Temba, Daz baba hiyo ni kipindi kabla ya Daz Nundaz!Wachuja nafaka
Kina Suma GHot pot family.
Kali P alitoka miaka ya 2000's nahisi ni 2006Usinione mimi mwembamba ukadhani mi mgonjwa...nilikuwa bwanyenye..
Huyo alikuwa kundi gani kipindi ile...
Kuna kundi walikuwepo Suma Lee na marehemu CPwaa linaitwa Pack Lane.Kwa kipindi cha miaka ya 90’s mpaka 20’s ilikuwa ili msanii uweze kutoboa lazima ujiunge kwenye kundi lolote la muziki na ndio maana kwa kipindi hicho idadi ya makundi ilikuwa kubwa na yalidumu kwa muda mrefu,walikusudia kuifanya Tanzania kuwa "Taifa la hip hop’’, vijana kuondokana na maisha ya mtaani.
Haya ni baadhi makundi ambayo yalifanikiwa kwa kiasi kikubwa kuukuza muziki wetu na kuacha alama mpaka sasa.
1. Kwanza Unit (KU Creaw).
Kwanza Unit lilikuwa kundi la mwanzo kabisa la muziki wa hip hop na lilianzishwa mwaka 1990, liliundwa kutokana na muunganiko wa makundi matatu, KBC, Eazy-B, Fresh-G na D-Rob ni baadhi ya wasanii wa KUC ambapo awali walikuwa wana-rap kwa kiingereza lakini baadae walibadilika na kutumia Kiswahili.
2. Gangwe Mobb.
Temeke Mikoroshini ndiko maskani ya kundi hili yalipatikana na lilianzishwa mwishoni mwa miaka ya 90 punde baada ya Kwanza Unit, Mr. II na wengineo kuchangia muziki wa hip hop wa Kiswahili nchini kujipatia umaarufu, huku Inspector Haroun na Luteni Karama ndio walikuwa wanakikundi.
3. Hard Blasters.
Ujumbe wao kupitia muziki ulibadilisha mtazamo wa jamii na kuamini kuwa kufanya muziki sio uhuni ni ajira/kazi.
Fanani, Crazy One, Professor Jay, KC1, Trigger F na Tuff Jam waliunda kundi hilo na waliachia album kadhaa “Funga kazi, Tuko nyuma kimaendeleo nakadhalika
4. TMK Wanaume Family.
Ni moja ya kundi lililoleta mapinduzi makubwa kwenye muziki wa kizazi kipya tangu kuanzishwa kwake Septemba 16, 2002 mjini Mwanza, wakati wa uzinduzi wa album ya Juma Nature ‘’Ugali’’ mpaka sasa limejijengea umaarufu mkubwa kutokana na mtindo wao wa kucheza ujulikanao ‘Mapanga’.
5. Chemba Squard.
Hili ni miongoni mwa makundi yaliyokuwa na wasanii wenye vipaji na uwezo wa hali ya juu sana tangu walipoingia rasmi sokoni mwaka 2000, liliundwa na Noorah (Baba Stylz), Dark Master, The late Mez B na Mangwair, wote walikuta shule ya Sekondari Mazengo Dodoma.
6. East Coast Team.
Linaundwa na wasanii Ay, Mwana FA na Crazy GK ambao walifanikiwa kwa kiasi kikubwa kuleta mabadiliko kwenye game kuwa ya kisasa zaidi, makazi yake ni Upanga mashariki.
Yapo mengi sana wahenga wenzangu mnaweza kuendelea kuyataja karibuni sana wahenga.
Ilianza ikiwa NUTA Jazz band ikakaja kuwa JUWATA Jazz band (Msondo ngoma ukiwa ni mtindo wao) baadaye ikivyokuwa bendi huru kutoka Jumuiya ya Wafanyakazi ndipo ikwa bendi ya Msondo.Msondo show zao nlikuwa naenda sana
Ova
Waliokuwa consistent na focused walifanikiwa, hata kidogo upatacho ukiwa na malengo unasonga mbele.Soko halikuwa tayari aisee. Vijana wengi waliopenda muziki huu hawakuweza kuununua walitegemea redio na TV au waende kwenye shows. Digital platforms zilizopo saivi zingekuepo enzi zile nahisi wangetoboa.
Nadhani East Coast Team kulikuja kuwa na O-Ten na Imam Abbas. Baadae wakajaongezeka madogo wengine kama Snare na wengine sikuwajua vizuri wakajiita East Coast Army
Yamenikutaaaaa yamenikutaa,yamenikuta mzee mwenzangu mpaka nayavalia bukta.Yamenikuta mzee mwenzangu sina changu
Wanga wengi anga zangu
Kiama Chao au Kiama changu
Hawakawii kusema flan una HIV wanapakaza hivi hivi
Goma la hiphop kali la wakati wote hiloGwm ft Mr 2...yamenikuta
Ova
Unao wa LWP waliomshirikisha Inspecta unaitwa Jela. Nalikubaligi sana lile libiti.
ahaaaa naukumbuka huu wimbo 🙏Bon cruz waloimba Jamaa (Wanamwita kaka poa huyu jamaa, wanamwita mambo safi huyu jamaa, wanamwita mtoto wa watu huyu jamaa, sijui si riziki au ni laana huyu jamaa twakuomba tusamehe maulana)
Na Dolphin pose walikuwa wakijiita machalii wawili heat song yao Ni rafiki tu.
Nimeupata saivi tu, sikuwa naoUnao wa LWP waliomshirikisha Inspecta unaitwa Jela. Nalikubaligi sana lile libiti.
Yamenikutaaaaa yamenikuta mzee mwenzanguGwm ft Mr 2...yamenikuta
Ova