Haya mambo jamii ikiendelea kuyachekea tutapoteza nguvu kazi za taifa

Haya mambo jamii ikiendelea kuyachekea tutapoteza nguvu kazi za taifa

kiss ov love

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2025
Posts
9,388
Reaction score
16,188
Wana jukwaa habari za wakati huu, ni matumaini yangu mu wazima. Huwa nashea mambo yanayotokea kwenye jamii yangu kama ilivyo ada.

Hapa ninapoishi kuna mmama jirani yangu ana watoto watatu wakike mmoja na wakiume wawili, sasa huyu mtoto wa kike ni binti wa karibu miaka 22 hadi 23 hivi..

Alivyomaliza kidato cha 4, aliolewa akazaa mtoto mmoja ambaye kwasasa ana miaka miwili kuelekea mitatu, lakini walishindwana na mwanaume wake hivyo yupo tu anakaa zake huko kapanga mbali na kwao kabisa.

Sasa kuna siku moja hapo nyumbani kwao kulikuwa na sherehe huyu mama jirani kuna ndugu yake alikuwa anaolewa hivyo shughuli ilikuwa hapo kwao. Sasa wakati wa kwenda kumpamba bibi harusi, yule binti akawa ameongozana na kijana mmoja hivi kwa maelezo ya mama yake huyo kijana ni rafiki yake.

Walivyorudi kutoka huko saluni mimi nikawa nimekaa hapo nje na mama shughuli pamoja na wamama wengine maana shughuli ilikuwa bado haijaanza hivyo watu hawakuwa wengi pembeni kulikuwa kuna ndugu za huyo mama jirani na watu wengine baadhi wa kiume.

Wakawa wamekuja hapo kwenye kundi la wamama sasa yule kijana akaanza kuropoka na kutukana hayo maelezo yake na muonekano wake huhitaji hata D moja kutambua kuwa kipa katoka golini, binafsi nilikuwa naona aibu maana anaongea hayo mbele ya wamama watu wazima wa kumzaa na wanamchekea tu.

Kilichonisikitisha ni kwamba huyo msichana ambaye anadai ni rafiki yake akawa anacheka anaona ni kitu cha kawaida tu na anasema ndiyo alivyo huyu akilewa huwa anatukanaga hivi, akawa anasema yaani huyu mara ana bwana Zanzibar akiendaga huko akirudi na hela za maana ananitoaga ndiyo maana nampenda, vile vile anasema amesoma nae O-level, na ni kwamba tangu wanasoma walikuwa hadi wanalala wote hapo kwao kashazoeleka.

Huyu mama jirani yeye hana shida kabisa na mwanae kuwa na mazoea na urafiki na mtu wa namna hii, sasa hizi tabia zikichekewa na kukumbatiwa si ndivyo vijana wengi wataona ni vitu vya kawaida na watashawishika kufanya hayo mambo, tutakuwa na kizazi cha namna gani.... binafsi niliumizwa sana na hivi vitendo maana nimewaza mengi sana, Mungu atusaidie kwenye hiki kizazi chenye kila mambo mabaya, wazazi mjitahidi kuwa makini na malezi ya watoto wenu wakike kwa wakiume
 
Back
Top Bottom