Haya mambo ya ndoa hapana aisee anakununia siku nzima afu asubuhi unatakiwa umuachie matumizi

Haya mambo ya ndoa hapana aisee anakununia siku nzima afu asubuhi unatakiwa umuachie matumizi

Kuna wakati unajiuliza, what's all this for? Yaani mtu ananuna tu, umetoka huko ukijua narudi kupumzisha akili unakutana na mdomo umefura na huambiwi nini shida.

Kuna wakati nawaelewa senior bachelors sema kuishi mwenyewe nao mtihani sana.
 
Kawaida sana mkuu, hata sisi pia huwa tunanuna lakini bado asubuhi tunawahi kuamka, tunaandaa nguo za kazini, tunaandaa breakfast na kupack lunch box yenye chakula chake pendwa juu. Vyote hivyo tunafanya huku tumenuna.
 
Hizi aina za vijana wa siku hizi ni challenge sana, ukiangalia nyuzi zao humu za malalamiko dhidi ya mabinti/wanawake unagundua kuwa jamii ina upungufu wa wanaume.

Sijui ndio matokeo ya malezi toka kwa baba dhaifu wa zama hizi au ndio tunaanza kushuhudia matokeo ya malezi ya ‘singo maza’?!

By the way, naona dada ako ‘chura’ anachanja mbuga tu 😎😎
Kuna tabia ni purely za kike, huwezi kumtenganisha ke na kununa. Tunatofautiana viwango tu.

Ikiwa mtu amejiandaa kuishi na ke lazima ajiandae na kuhandle tabia za kike.

Ndugu yangu chura amebadilika kama zuwena.
 
Mi alinnunia tangu juzi kwasbb nliingia na viatu ndani kabla hapajakauka alipodeki
 
Unakuta janajike limevuta domo kama mimba ya panya bila sababu zozote za msingi.
 
Mke anakununia siku nzima yaani hataki kuongea na wewe kabisa afu asubuhi niache matumizi wakati ameninunia
Kabla asubuhi kufika, mgeuze bila kumuandaa ichape kama ataendelea kununa bila ushirikiano
 
Back
Top Bottom