HAYA, mambo yanazidi kuwa vinyo vinyo, dhidi ya Chalamila, wamiliki wa Mabasi nao wamgomea

HAYA, mambo yanazidi kuwa vinyo vinyo, dhidi ya Chalamila, wamiliki wa Mabasi nao wamgomea

Kupitia Kitenge TV, Nnkya, mmoja wa wamiliki wa ofisi hizo, amesema Mkuu wa Mkoa anakurupuka kutoa matamko kuhusu ofisi hizo, wakati yeye mwenyewe alikuwa Mkuu wa Mkoa kipindi ambacho ofisi hizo zilipokuwa zikijengwa. Amehoji, iweje leo anataka ziamishwe?
Shida ya mtu kuwa mwongo- mwongo na kuwa miongoni mwa wahalifu credibility inaondoka. Hata siku ukiwa na agenda ya maana watu hawakuamini tena
 
Hii amri ya Chalamila natamani Rais Samia akazie ili upigiliwe msumari wa mwisho, Chalamila yupo sahihi apongezwe
Mtu na mzigo chanika/Kigamboni kiloo 100 tu, atafikaje Mbezi kimara na gharama zitakuwaje? Watu wa mabasi wanawasaidia waananchi, lakini wananchi wenyewe wana akili mavi kama wewe
Nakazia
Mwilapwa ni jina la huko anakotoka Chalamila
Usemalo ni sahihi kabisa 100%
 
Aisee leo ume comment, pokea like yangu Mkuu sana
Mkuu 'raraa reree' huwa hasomi; kazi yake ni kuweka tu alama za 'like' kwa kila kilichoandikwa'

Ni mtu wa kipekee sana.

Sijui hili huwa linampa raha gani; anafahamu mwenyewe!

Nashawishika kusema mkuu 'raraa reree' anacho kipaji cha kuweka 'like' kwenye michango mbalimbali kwenye Jukwaa la Siasa.
 
Watu wa Dar acheni ubishi stendi haiwezi kuwa karibu na kila mtu. Mikoani stend zipo centre za wilaya, hivyo ukiwa mbali na hiyo stend inabidi usafiri na hivyo utalala karibu na stend au utasafiri siku hiyo hiyo. Sasa mtu anakuambia sijui chanika mbali kwenda stend Mbezi. Toka mapema huko chanika wahi gari Mbezi au kalale lodge karibu na stend. Maendeleo ya ustraabu yanatuhitaji tubadilike.
Dar es Salaam ina wilaya 5 kwanini Mabasi yasifike wilayani yanalazishwa yaishie stendi ya mkoa tu?
 
Mtu na mzigo chanika/Kigamboni kiloo 100 tu, atafikaje Mbezi kimara na gharama zitakuwaje? Watu wa mabasi wanawasaidia waananchi, lakini wananchi wenyewe wana akili mavi kama wewe
Lakini vipi kuhusu mikoani magari yanakotoka? Si abiria wakiwa na mizigo yao wanayafuata mabasi stendi bila kujali umbali uliopo kati ya majumbani kwao mpaka stendi? Hizo kilo 100 zinafikaje stendi? Au basi linamfuata abiria nyumbani? Mfano, mtu aliyepo Mbalizi - Mbeya, anasafiri kwenda Mwanza, stendi ipo nanenane, anafuata basi huko. Iweje kwa Dar isiwezekane?
 
Watu wengi wanaomsapoti chalamila ni matofali yaan hua hayasafiri hata yakisafiri mpaka yapakiwe ndo maana hayajui ni kiasi gani sisi tunao safiri kira mara. Hao wenye mabasi wanatusaidia kutufikisha mjini..Kwanj basi likinishusha shekilango kuna shida gani au tunafanyiana roho mbaya tu
 
Mtu ana mzigo chanika/Kigamboni kilo 100 tu, atafikaje Mbezi kimara na gharama zitakuwaje? Matajiri wa mabasi wanawasaidia waananchi, lakini wananchi wenyewe wana akili mavi kama wewe
Mbona SGR mnaenda na vifurushi vyenu?
Kwanini kwenye usafiri wa mabasi mje na conditions zenu ?
 
Watu wa Dar acheni ubishi stendi haiwezi kuwa karibu na kila mtu. Mikoani stend zipo centre za wilaya, hivyo ukiwa mbali na hiyo stend inabidi usafiri na hivyo utalala karibu na stend au utasafiri siku hiyo hiyo. Sasa mtu anakuambia sijui chanika mbali kwenda stend Mbezi. Toka mapema huko chanika wahi gari Mbezi au kalale lodge karibu na stend. Maendeleo ya ustraabu yanatuhitaji tubadilike.
Wanadeka sana
Mbona hawajawahi kulalamika kwamba Airport ipo mbali?
 
Dar es Salaam ina wilaya 5 kwanini Mabasi yasifike wilayani yanalazishwa yaishie stendi ya mkoa tu?

Dar kieneo ni dogo, stend ya mkoa iko karibu na wilaya zote na inafikika kirahisi. Mabasi hayawezi kufika kila wilaya ya Dar sababu itakuwa ni vurugu kila bus kufika kila wilaya. Stendi za kuongezeka ni za kikanda , za mabasi kwenda kusini(Lindi,Mtwara) , kaskazini (Kmj,Arusha, Tanga).
 
Wewe hujali ustaarabu umejaa ubinafsi hutaki miji ya nchi yako ipangiliwe vizuri.
Ipangwe kwenye kipi?
Yard za makontena kila kona, kila mtaa, kila barabara kila siku zinafunguliwa mpya,
Dar maeneo ya wazi yote wamejimilikisha
ikifika saa 7 mchana mandela road haipitiki, foleni ya maroli toka tazara hadi ubungo.
Bara bara za mijini zimejaa mashimo,
Mwendo Kasi inafanys kazi kwa
Asilimia only 20.
Huu ndio upangaji wa mji?
Wamiliki wa mabasi wamekuwa msaada sana wa abiria wa pembezoni.
Ukifika hapo magufuli stend usipo kuwa makini utaibiwa na kupandishwa gari bovu, mawinga wanakuvamia km unadaiwa vile... kwa mvutano na mawinga unaweza kuchaniwa nguo.
Huo ndio ustaarabu?
 
Tuwe na stand angalau nne za mabasi ya mikoani.

Tujenge mbagala stand kubwa na ya kisasa.

Chanika inahitajika haraka au ikiwezekana ianzie mvuti. Kuondoa tatizo la miaka 20 ijayo

Mbande hapa itakuwa umesolve pakubwa.

Kigamboni hili lipo wazi

Tegeta/bunju

Tengeneza Ring road ya kuunganisha mbagala na gongo la mboto kwa kuapugrade hii njia kwenda njia nne(hii ndio ring road ya dar es salaam)

Boresha njia ya Kutokea magufuli.

Boresha magufuli tegeta

Hii itasaidia mabasi kuizunguka pembezoni mwa dar kwa vitongoji vyote bila kuingia mjini.

Tuwaze maboresho
Huu mji ulishakosewa plan miaka mingi sana.
Yaani hii plan ilitakiwa iwepo kabla hata ya mwaka 1990.
Imagine leo hii wakiitumia hii plan ya kujenga barabara mpya kutoka Mbagala to Gongolamboto watabomoa nyumba ngapi na watalipa fidia kiasi gani kuwahamisha watu ambao wanaishi kwenye hiyo zone.
Yaani shida ilipoanzia ni kwamba barabara alizotuachia mkoloni ndio hadi leo zinatumika hizohizo wanazitanua tu lakini hawaongezi mainroads mpya.
Bado tuna safari ndefu sana
 
Kuna kitu hakipo sawa hasa mifumo yetu ya uongozi na aina ya matamko na maamuzi yanayofikiwa, kunakuwa na mkanganyiko fulani , huyu atasema hili na ataruhusu kitu fulani kifanyike then mwingine atakuja kuongea kitu tofauti
 
Watu wa Dar acheni ubishi stendi haiwezi kuwa karibu na kila mtu. Mikoani stend zipo centre za wilaya, hivyo ukiwa mbali na hiyo stend inabidi usafiri na hivyo utalala karibu na stend au utasafiri siku hiyo hiyo. Sasa mtu anakuambia sijui chanika mbali kwenda stend Mbezi. Toka mapema huko chanika wahi gari Mbezi au kalale lodge karibu na stend. Maendeleo ya ustraabu yanatuhitaji tubadilike.

Kwa hiyo mtu wa Mafinga akapandie Bus Iringa mjini?
Au mtu wa kahama akapandie Basi Shinyanga?
Au mtu wa Tarangire akapandie Basi Arusha Mjini?
Au mtu wa Ruvu au Makanya Akapandie Bus Same au Moshi mjini?

Au mtu wa Tukuyu au Matema Beach akapandie Gari Mbeya Mjini?
Au Mtu wa Mvomero au Turiani akapandie Basi Msamvu Stendi kuu ya Morogoro?

Hujui hata kwa nini serikali zipo nafikiri.
Kazi ya serikali ni kuhudumia wananchi. Na kuhudumia wananchi ni kuwarahisishia wananchi maisha.

Dar es salaam ni jiji Kubwa, kuwa na Stendi moja ya mabasi lazima iwe changamoto kwenye connectivity.

Ni aidha kuwepo na stendi ndogo ndogo au kuwepo na shuttle za kupeleka wananchi(abiria) stendi. Na hizo shuttle zitumie gharama zilizopo kwenye nauli halisi.

Kuna wengine wanasema mbona zamani sijui stendi ilikuwa Ubungo na hapakuwa na malalamiko.
Mtu wa hivyo lazima awe ni chizi au upeo mdogo wa kufikiri.

Ndio wale wazazi wapumbavu kisa yenyewe yalipata shida utotoni yanaambia watoto waende shule umbali mrefu au wale uji wa chumvi kisa wao walikunywa
 
Back
Top Bottom