Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 18,653
- 31,010
Wafanyabiashara kwa sasa wanaiendesha serikali.Kupitia Kitenge TV, Nnkya, mmoja wa wamiliki wa ofisi hizo, amesema Mkuu wa Mkoa anakurupuka kutoa matamko kuhusu ofisi hizo, wakati yeye mwenyewe alikuwa Mkuu wa Mkoa kipindi ambacho ofisi hizo zilipokuwa zikijengwa. Amehoji, iweje leo anataka ziamishwe?
Wanaona wako juu ya sheria na wanajifanyia kama wanavyoona.
Jiji la Dar es salaam ahlitawaliki kutokana na wafanyabiashara wengi kutaka kufanya kama wanavyoona wao na kwa faida yao.
Kuanzia Bajaji, bodaboda, malori, mabasi na hata machinga barabarani kila mtu anajiona ana haki ya kufanya kama anavyotaka.
Jiji hili linahitaji mkono wa chuma na si vinginevyo.