Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 18,653
- 31,010
Wafanyabiashara kwa sasa wanaiendesha serikali.Kupitia Kitenge TV, Nnkya, mmoja wa wamiliki wa ofisi hizo, amesema Mkuu wa Mkoa anakurupuka kutoa matamko kuhusu ofisi hizo, wakati yeye mwenyewe alikuwa Mkuu wa Mkoa kipindi ambacho ofisi hizo zilipokuwa zikijengwa. Amehoji, iweje leo anataka ziamishwe?
Watu wa Dar acheni ubishi stendi haiwezi kuwa karibu na kila mtu. Mikoani stend zipo centre za wilaya, hivyo ukiwa mbali na hiyo stend inabidi usafiri na hivyo utalala karibu na stend au utasafiri siku hiyo hiyo. Sasa mtu anakuambia sijui chanika mbali kwenda stend Mbezi. Toka mapema huko chanika wahi gari Mbezi au kalale lodge karibu na stend. Maendeleo ya ustraabu yanatuhitaji tubadilike.
Wewe jamaa una akili nyingi sana ubarikiwe na muumba wetuUnapojenga, ofisi na yard ya mabasi kuna kibali kutoka ofisi ya Ardhi ya halmashauri husika au Wizara ya Ardhi.
Utaamatanisha michoro ya majengo pia. Tuanzie hapo, je halmashauri husika au Wizara ya Ardhi ilitoa vibali vya ujenzi wa hizo yards?
Kazi za yards hizo ni kuhifadhi na kuwa kama karakana au kupakia mizigo na abiria?
Kuna mambo mengi ya kuangalia kabla ya kuropoka nani amekosea.
Nimeona comment ya jamaa nikacheka sanaInafikika kutoka wapi?. Mbezi ipo mpakani na wilaya Kibaha halafu unadai inafikika kutoka Kutoka Dar. Punguza uongo
Soma vizuri ,nimeandika mikoani kila wilaya ina stend yake, sasa wa kahama kupandia shinyanga umeitoa wapi?Kwa hiyo mtu wa Mafinga akapandie Bus Iringa mjini?
Au mtu wa kahama akapandie Basi Shinyanga?
Au mtu wa Tarangire akapandie Basi Arusha Mjini?
Au mtu wa Ruvu au Makanya Akapandie Bus Same au Moshi mjini?
Au mtu wa Tukuyu au Matema Beach akapandie Gari Mbeya Mjini?
Au Mtu wa Mvomero au Turiani akapandie Basi Msamvu Stendi kuu ya Morogoro?
Hujui hata kwa nini serikali zipo nafikiri.
Kazi ya serikali ni kuhudumia wananchi. Na kuhudumia wananchi ni kuwarahisishia wananchi maisha.
Dar es salaam ni jiji Kubwa, kuwa na Stendi moja ya mabasi lazima iwe changamoto kwenye connectivity.
Ni aidha kuwepo na stendi ndogo ndogo au kuwepo na shuttle za kupeleka wananchi(abiria) stendi. Na hizo shuttle zitumie gharama zilizopo kwenye nauli halisi.
Kuna wengine wanasema mbona zamani sijui stendi ilikuwa Ubungo na hapakuwa na malalamiko.
Mtu wa hivyo lazima awe ni chizi au upeo mdogo wa kufikiri.
Ndio wale wazazi wapumbavu kisa yenyewe yalipata shida utotoni yanaambia watoto waende shule umbali mrefu au wale uji wa chumvi kisa wao walikunywa
Soma vizuri ,nimeandika mikoani kila wilaya ina stend yake, sasa wa kahama kupandia shinyanga umeitoa wapi?
Kwa Dar stend ndogo ndogo unamaanisha kila wilaya kuwe na stendi yake ambapo kwa miundo mbinu iliyopo itakuwa ni vurugu sana sababu kila kampuni kwa route ya Dar-Mwanza italazimika waweke bus la Temeke-Mwanza, Kinondoni-Mwanza, Ilala-Mwanza au kama ni bus moja basi lizungukie stend zote za wilaya ili kuchukua abiria wake.Huoni hiyo vurugu?
Stend za kuongezeka ni za kikanda (za mabus kuelekea kusini na kaskazini) lakini sio kutaka eti kila stend utakayo enda ukute gari la kila route huko ni kuchafua mji.
Pia suala la shuttle ni kuchafua mji.Usafiri wa uhakika na rafiki wa kutoka na kuelekea kila pembe ya Dar upo na cha muhimu ni maboresho ya huo usafiri.
Kurahisha maisha inatakiwa iwe ya kiustaarabu la sivyo miji ndio hiyo inakuwa michafu.
Dar ni ndogo na iko connected vizuri na wilaya zake tofauti na mikoa mingine ambayo ni mikubwa kieneo na haiko connected vizuri na wilaya zake hivyo kwa mikoani kila wilaya kuwa na stand yake ni sawa.Hoja yako ya mikoani kila wilaya ina stendi ungekuwa ni hoja kuu. Basi automatically Kulazimisha Dar iwe na stendi moja, kwamba magari yote yaende magufuli bus stend inakufa kifo cha mended.
Alafu hiyohiyo DSM ndio mkoa wenye watu wengi kuliko mikoa mingine. Tena mikoa mingjne imezidiwa hata mara Tatu.
Uchafu ni kukosa mpangilio tuu.
Hapo Shekilango ndio kuna vituo mpaka Magomeni.