Haya maneno ya mtangazaji wa Uhuru FM kwa wanafunzi wa Jangwani mnayaonaje?

Andrew Tate

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2020
Posts
4,503
Reaction score
6,861
Lengo la uzi halipo kisiasa wala kuegemea au kushambulia upande wa chama chochote cha kisiasa.

Leo nilikuwa nasikiliza redio stesheni ya Uhuru FM.

Walikuwa wanahoji wanafunzi wa kidato cha 5 na 6 shule ya Secondary Jangwani kuhusu "kwanini Magufuli miaka mitano mingine"

Ila kuna mwanafunzi mmoja alionesha kaupinzani kidogo.
Kwamba mhe. Rais Magufuli mambo mengi ya construction au wanaita maendeleo ameyafanya Dar na sio sehemu nyingine za Tanzania.
Pia mhe. Amefocus zaidi kwenye vitu kuliko watu.

Ila nilishangaa kuona yule mtangazaji akionyesha kutofurahishwa na maoni yale.

Then akasema "Ukiwa sehemu yenye kundi la watu uchague maneno ya kuongea"
Nadhani alimaanisha usitoe maoni yoyote yanayokwenda against na anavyotaka.

Cha kushangaza zaidi ni pale alipoowambia hao wanafunzi kwamba "hutakiwi kufanya makosa kwani ukikosea leo umejikosea miaka mitano,

Nyie si mnaona alichofanya kwenye elimu hapa?
Sasa hamtakiwi kukosea.

Sasa kwa hali hiyo mbona inaonesha wamewanyima Uhuru wa maoni hao wanafunzi?

Nao kwa uoga imewabidi waseme vitu kama robots walioprogramiwa kusema kitu fulani tu.

Hawaoni kama wanatengeneza watu ambao ni waoga.
Watu ambao hawatoweza kupigania haki zao pale inapobidi.
Wanatengeneza watu ambao bila shaka hawatoweza kufikiria nje ya box na kufuata waliyowekewa kama mnyama aliye tofauti na binadamu.

Mna maoni gani wana JamiiForums?
Au mimi nimeelewa vibaya? Pia kukosoa na kurekebisha itakuwa vizuri zaidi.
 
Kwani Uhuru fm mali ya nani, chombo cha habari cha CCM unakuja unaanza kumponda mwenyekiti wa chama, mtangazaji alikua sahihi kumfunza adabu huyo mwanafunzi.
 
Zamu hii Magu kawafanya waunde kwaya za kumsifia ,kila sehemu wachumia tumbo wanamsifia.

Nimeshangaa kuona kampeni mbeya kwaya ya kanisa kuhudhuria kampeni na kuimba wimbo wa kumsifu magu.

Yaani hata kwaya za makanisa yanatumika kisiasa
 
Ila kuna mwanafunzi mmoja alionesha kaupinzani kidogo.
Kwamba mhe. Rais Magufuli mambo mengi ya construction au wanaita maendeleo ameyafanya Dar na sio sehemu nyingine za Tanzania.
Pia mhe. Amefocus zaidi kwenye vitu kuliko watu.

Ila nilishangaa kuona yule mtangazaji akionyesha kutofurahishwa na maoni yale.

Then akasema "Ukiwa sehemu yenye kundi la watu uchague maneno ya kuongea"
Nadhani alimaanisha usitoe maoni yoyote yanayokwenda against na anavyotaka.
dogo kamfanya jamaa apanic

asiwafokee watoto
 
Huyo dent ametembelea maeneo gani nchini zaidi ya Dar ili kutathmini uwepo wa miradi ya maendeleo? Kwa uelewa wake kama anamaanisha flyover sawa. Je anafahamu kuhusu SGR, bwawa la Nyerere, Viwanja vya ndege, Hospitali na vituo vya afya, barabara zinazounganisha mikoa?
 
Kwani Uhuru fm mali ya nani, chombo cha habari cha CCM unakuja unaanza kumponda mwenyekiti wa chama, mtangazaji alikua sahihi kumfunza adabu huyo mwanafunzi.
Technically hajamponda mhe. Bali ametoa maoni.
Kufanya hivyo ni kumnyima mtu uhuru wa kutoa maoni haijarishi chombo ni cha nani.
Kama hawataki kukosolewa basi wasihoji watu.
 
Huyo dent ametembelea maeneo gani nchini zaidi ya Dar ili kutathmini uwepo wa miradi ya maendeleo? Kwa uelewa wake kama anamaanisha flyover sawa. Je anafahamu kuhusu SGR, bwawa la Nyerere, Viwanja vya ndege, Hospitali na vituo vya afya, barabara zinazounganisha mikoa?
Lakini still rais amefocus kwenye vitu zaidi ya watu na hata hivyo vitu sio kila mahali.

Watu ndio kila kitu kwenye taifa.
 
Huyo dent ametembelea maeneo gani nchini zaidi ya Dar ili kutathmini uwepo wa miradi ya maendeleo? Kwa uelewa wake kama anamaanisha flyover sawa. Je anafahamu kuhusu SGR, bwawa la Nyerere, Viwanja vya ndege, Hospitali na vituo vya afya, barabara zinazounganisha mikoa?
Ni mwanafunzi wa advanced level, maana yake yawezekana alimaliza shule ya kata huko Uvinza/wilaya yoyote iliyo nyuma kimaendeleo, akapangiwa shule iliyopo katikati ya jiji, kutoka huko Uvinza/wilaya yoyote iliyo nyuma kimaendeleo akasafiri hadi Dar, anashituka anapokelewa na daraja la Kibamba na libarabara lipana, mara paap ngazi mbili za Ubungo hizi hapa...
Nafsi yake ikasononeka sana.
 
Technically hajamponda mhe. Bali ametoa maoni.
Kufanya hivyo ni kumnyima mtu uhuru wa kutoa maoni haijarishi chombo ni cha nani.
Kama hawataki kukosolewa basi wasihoji watu.
Anatoa maoni hasi nyakati hizi za uchaguzi, kwa kiongozi wa CCM, kwenye radio inayomilikiwa na CCM, huyo dogo hana common sense.

Maoni hayakatazwi, tatizo lazima uangalie uanayatolea maoni yako wapi sio kila sehemu kushare mtazamo wako, sehemu nyingine wasome wahusika kwanza.
 
Back
Top Bottom