Haya maneno ya mtangazaji wa Uhuru FM kwa wanafunzi wa Jangwani mnayaonaje?

Haya maneno ya mtangazaji wa Uhuru FM kwa wanafunzi wa Jangwani mnayaonaje?

Huyo dent ametembelea maeneo gani nchini zaidi ya Dar ili kutathmini uwepo wa miradi ya maendeleo? Kwa uelewa wake kama anamaanisha flyover sawa. Je anafahamu kuhusu SGR, bwawa la Nyerere, Viwanja vya ndege, Hospitali na vituo vya afya, barabara zinazounganisha mikoa?
Labda ametembelea Arusha.Bukoba na Babati akaona stendi za mabasi zilivyo mbovu
 
Anatoa maoni hasi nyakati hizi za uchaguzi, kwa kiongozi wa CCM, kwenye radio inayomilikiwa na CCM, huyo dogo hana common sense.

Maoni hayakatazwi, tatizo lazima uangalie uanayatolea maoni yako wapi sio kila sehemu kushare mtazamo wako, sehemu nyingine wasome wahusika kwanza.
Na hapo ndipo unapovunja haki ya uhuru wa kutoa maoni.

Kukosolewa ni lazima ili ajirekebishe sababu wao ndio watakaoumia.
Sasa kama rais anafanya yasiokidhi mahitaji ya wananchi kwanini asikosolewe?
Yaani niendelee kukaa na mambo yasiyo kidhi sababu unaogopa kumkosoa rais?
Hapo ndipo unapotengeneza watu waoga waoga wasioweza kupigania haki zao kama hao wanafunzi wengine.
Rais ni kiongozi wa wananchi na sio vinginevyo hivyo ni wajibu wake kufanya kile wananchi wanataka.

Huyo mwanafunzi anayo common sense sababu anajua kipi sahihi na nini anataka sio hao wengine waoga.

Uoga ni umasikini.

Na ukumbuke rais yupo kwa ajili ya wananchi na sio wananchi wapo kwa ajiri ya rais.
 
Kutishana tishana tu

Upuuzi mtupu

Huwezi lazimisha wote tuwe sawa kimawazo na kifikra

Inakera sana

Ila yatapita haya na itabaki historia iko siku
 
Kwa maneno hayo huyo mwanafunzi hata form six akifaulu vipi na kupata nafasi ya chuo asahau tu habari ya mkopo. Maana kwa hali ilivyo kwa sasa jinamizi la kauli yake litaendelea kumwandama mgongoni.
 
Magufuli for life
Magufuli for life![emoji316][emoji316][emoji316]
1583234011_1583234011-picsay.jpg
 
Kwani hiyo ni redio ya nani kwanza?!
Haijalishi radio ni ya nani.
Kufanya hivyo ni kuwanyima haki yao hao wanafunzi.

Africans niwaoga sana na ndio maana ni masikini.
Sasa huyo mwanafunzi asitoe maoni yake ya kweli kisa ni radio ya fulani na atoe tu maoni feki kisa radio ni ya fulani.
Huo ni uoga na ujinga.

Rais yupo kwa ajili ya wananchi na sio wananchi wapo kwa ajili ya rais.

Uoga ni umasikini.
 
Na wewe una moyo.
Redio zoote hizi wewe ukaona UHURU ndio inanasa... Au labda redio yako haiwezi kusachi?
 
Kwa maneno hayo huyo mwanafunzi hata form six akifaulu vipi na kupata nafasi ya chuo asahau tu habari ya mkopo. Maana kwa hali ilivyo kwa sasa jinamizi la kauli yake litaendelea kumwandama mgongoni.
Kivipi mkuu kwanini wamnyime mkopo?
Au kukosoa serikali ndio wamnyime mkopo?

Kama ni hivyo basi hakuna haki.
 
Huyo dent ametembelea maeneo gani nchini zaidi ya Dar ili kutathmini uwepo wa miradi ya maendeleo? Kwa uelewa wake kama anamaanisha flyover sawa. Je anafahamu kuhusu SGR, bwawa la Nyerere, Viwanja vya ndege, Hospitali na vituo vya afya, barabara zinazounganisha mikoa?
Kwani ayo yote si kazi ya serikali?Kwanini sifa ziende kwake,labda anatoa mfukoni mwake🙏
 
Huyo mtangazaji zwazwa sana,ili mdahalo unoge lazima kuwe na msigano wa pande mbili,vinginevyo huo haukuwa mdahalo bali kipindi cha kusifu na kumuabudu jiwe
 
Huyo dent ametembelea maeneo gani nchini zaidi ya Dar ili kutathmini uwepo wa miradi ya maendeleo? Kwa uelewa wake kama anamaanisha flyover sawa. Je anafahamu kuhusu SGR, bwawa la Nyerere, Viwanja vya ndege, Hospitali na vituo vya afya, barabara zinazounganisha mikoa?
Usimfundishe kijana ujinga.
 
Lengo la uzi halipo kisiasa wala kuegemea au kushambulia upande wa chama chochote cha kisiasa.

Leo nilikuwa nasikiliza redio stesheni ya Uhuru FM.

Walikuwa wanahoji wanafunzi wa kidato cha 5 na 6 shule ya Secondary Jangwani kuhusu "kwanini Magufuli miaka mitano mingine"

Ila kuna mwanafunzi mmoja alionesha kaupinzani kidogo.
Kwamba mhe. Rais Magufuli mambo mengi ya construction au wanaita maendeleo ameyafanya Dar na sio sehemu nyingine za Tanzania.
Pia mhe. Amefocus zaidi kwenye vitu kuliko watu.

Ila nilishangaa kuona yule mtangazaji akionyesha kutofurahishwa na maoni yale.

Then akasema "Ukiwa sehemu yenye kundi la watu uchague maneno ya kuongea"
Nadhani alimaanisha usitoe maoni yoyote yanayokwenda against na anavyotaka.

Cha kushangaza zaidi ni pale alipoowambia hao wanafunzi kwamba "hutakiwi kufanya makosa kwani ukikosea leo umejikosea miaka mitano,

Nyie si mnaona alichofanya kwenye elimu hapa?
Sasa hamtakiwi kukosea.

Sasa kwa hali hiyo mbona inaonesha wamewanyima Uhuru wa maoni hao wanafunzi?

Nao kwa uoga imewabidi waseme vitu kama robots walioprogramiwa kusema kitu fulani tu.

Hawaoni kama wanatengeneza watu ambao ni waoga.
Watu ambao hawatoweza kupigania haki zao pale inapobidi.
Wanatengeneza watu ambao bila shaka hawatoweza kufikiria nje ya box na kufuata waliyowekewa kama mnyama aliye tofauti na binadamu.

Mna maoni gani wana JamiiForums?
Au mimi nimeelewa vibaya? Pia kukosoa na kurekebisha itakuwa vizuri zaidi.
Akili za kuambiwq achanganye na za kwake
 
Back
Top Bottom