Kuna jamaa yg mmoja yeye anampenda sana mke wake ,kiukweli upendo ule sijawai kukuona
Cha kwanza jamaa hana kazi maalumu Kila dili ngumu ye anapiga tu , ila anahakikisha mkewe anapata mahitaji yote muhimu
Jamaa humnunulia mkewe nguo za thamani na kumpa vitu vyote vizuri
, Cha ajabu mkewe ni kicheche sana
Tukio la ajabu Kuna siku mke aliondoka ghafla pasipo mume kujua , Sasa tulimtafuta sanaaa hakupatikana baada ya wiki tukapata taalifa Yuko salasala benako Kuna mchizi anabiga mbupu kafungia ndani
Akatuchukua ili tumpe kampani ya kwenda kufanya Fuji ili kumuonesha mshikaji ubabe , kama vipi timsaule Kila kitu [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Aisee tukatoka na hasira tukiwa na silaha mbalimbali za jadi huku njiani tukijiapiza haiwezekani fala mmoja kuja kuchukua mke wa swahiba wetu na kwenda kumfungia ndani
Ebwanaaa kufika eneo la tukio ohoooo
Ile tunataka kulianzisha , huyu jamaa wetu mwenye mke akapoa tunaona mtu anapiga magoti huku anaelekea alipokaa mke wake Tena huku anaomba msamaha[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Aisee tulipata hasira sana Tena jamaa alitefedhehesha mno , ye ndio kwanza anatuambua jamani acheni fujo ngoja niongee na mke wg , mke akawa anagoma kuondoka , ikabidi amwambie mgoni wake bana niachie mke wg siku zote umekaa nae hujatosheka tu
Jamaa akamjibu ongea na mkeo mi kosa lg lipi , kuongea na mkewe mke akamwambia niachie nauli ya boda nakuja kesho
Swahiba wetu akachomoa 10000 akamuachia tukaondoka , kesho yke asubui mke akaja wakaendelea na maisha
Mimi binafsi nasema ,unaweza jua umeona na kusikia vitu vingi , kumbe ni mengi hatujayajua Duniani tuvijuavyo ni theruthi tu