Haya matamasha na marathons kwanini yanafanyika nyumbani kwa viongozi wakubwa tu?

Haya matamasha na marathons kwanini yanafanyika nyumbani kwa viongozi wakubwa tu?

fazili

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2011
Posts
16,427
Reaction score
22,418
Nimeona matamasha na marathons nyingi zikifanyika kwenye majimbo na mikoa walipotokea viongozi wakubwa wa nchi hii.

Mfano ni Tamasha la Kizimkazi lililomalizika hivi majuzi na lilifanyika kijijini alipotokea Rais Samia. Pia hivi majuzi tulishuhudia Tulia Marathon huko Mbeya alipotokea Spika Tulia Akson.

Na leo nimeona Ruangwa Marathon ikifanyika huko Ruangwa alipotokea waziri mkuu Kassim Majaliwa. Nini kinafanya matukio haya yafanyike wanapotokea viongozi wakubwa tu? Je maeneo mengine hawastahili kuwa na matukio haya?

Je sports complex kubwa ya kimataifa na uwanja wa mpira wa miguu mkubwa kuliko ule wa Amani Zanzibar unaojengwa huko kijijini Kizmkaz ni kwa ushawishi wa nani? Je campus mbili za University of Dar es Salaam zinazojengwa kwa wakati mmoja Ruangwa ni upendeleo au kuna kitu gani?
 
Back
Top Bottom