Haya mawe yanawasha umeme pamoja na Generator!

Haya mawe yanawasha umeme pamoja na Generator!

Poker

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2016
Posts
5,445
Reaction score
14,828
Haya ni mawe ambayo yanauwezo wa kuwasha umeme na hata generator. Yanapatikana nchini DRC na ndio sababu vita vya wenyewe kwa wenyewe haviishi.
Swali kwa wataalamu je ni kweli mawe yanaweza kuwasha umeme hii imekaaje?
 
Wataalamu wa hayo mawe wapo humu? Like seriously 😂😂

Ila kuna vimtu vimesoma Electrical vitakuja kujibu kutokana na hearsay na vi fizikia vya mchongo.
 
Alafu ili uzungumzie kitu ni lazima uwe unakifahamu, aliyegundua hayo, wanaoyatumia na wanaoishi eneo hilo huko congo ndio pekee wanaweza zungumzia
 
Kwahyo hiyo bulb imewashwa na nini Chief-Mkwawa
Ukiingia hio link wameelezea. Kuna video ni za zamani nyengine za Zimbabwe, Morocco etc

Hata mimi naweza fake hivyo kwa ganda la sigara ama chochote kifananiacho

Unaconect battery na bulb kwa + na - halafu waya mmoja unaukata, then kuunganisha vipande ulivyokata unaweka kipitisha umeme, kinaweza kuwa jiwe kama hilo, kipande cha fhahabu, shaba, chuma etc
 
Kwa elimu ya Geology ni kwamba, miamba moto mingi (Igneous rocky) Ina uwezo wa kupitisha umeme but siyo Kwa kiwango hicho mkuu. Composition na nature of deposition ndiyo itaufanya mwamba husika kuwa electrically charged au la.
 
Hyo ni kweli na hayo mawe inavosemekana yanapatikana Congo tuu kwa kiasi kikubwa, haya makundi ya waasi ndio hufanya biashara ya kuwauzia mabeberu na ndio sababu kuu vita Congo hasa sehemu zenye madini haitoisha Leo.
 
Wataalamu wa hayo mawe wapo humu? Like seriously 😂😂

Ila kuna vimtu vimesoma Electrical vitakuja kujibu kutokana na hearsay na vi fizikia vya mchongo.
Usidanganywe.Physics ni ile ile dunia nzima.
Static charges/ electricity vs current electicity
There is is no current if there is no complete circuit.
How does the charge flow out there? Hskuna anode wala cathode( Unajua kinachoweza kutokea iwapo charge zitakosa muelekeo sahihi?
Conventional science vs non conventional /pseudo science ndio kinachoendelea pale.
Ule ni ujinga wa waafrika na utaungwa mkono na wajinga wengi wa Aftica.
Uvumbuzi wowote huongozwa na misingi ya kisaysnsi.

Uvumbuzi mkubwa kama ule hauwezi wekwa you tube.
High energy battery storage kitu kinapiganiwa na kampuni kubwa duniani na reseach nyingi zinaendelea duniani.
Kiki za viewer mmeingia kingi.Watu wanataja viewer kwa scamming.
 
Kwa elimu ya Geology ni kwamba, miamba moto mingi (Igneous rocky) Ina uwezo wa kupitisha umeme but siyo Kwa kiwango hicho mkuu. Composition na nature of deposition ndiyo itaufanya mwamba husika kuwa electrically charged au la.
Ukisoma electromagnatism. Tunaambiwa Dunia ina miolions of charges but they are stable.Mili yetu ina chaji,wadudu wanachaji,.miti ina chaji.
If atom ndio ina electron proton na neutron kwa nini tushangae mawe kutoa nwanga.Static charge ziipo sehemu nyingi sana. Ila current charge inahitajika akili ya ziada ndio kina faradays, ohms, einstein(Photo electric effect) ,
Maxwell wakaja na nadharia za kuvuna hizo chaji.
Yale nawe kutoa mwanga ni sawa na radi hakuna maana yoyote.
 
Watu wanapenda kukuza mambo ambayo hayapo
Usiamini kila video unayo iona YouTube

DRC ni wazalishaji wakubwa wa madini yanayotumika kutengeneza betrii za lithium katika simu laptop nk nk na sio mawe yanayozalisha umeme kama ilivyo andikwa
 
Haya ni mawe ambayo yanauwezo wa kuwasha umeme na hata generator. Yanapatikana nchini DRC na ndio sababu vita vya wenyewe kwa wenyewe haviishi.
Swali kwa wataalamu je ni kweli mawe yanaweza kuwasha umeme hii imekaaje?
View attachment 2502434
Way unaungwaje kupata (-) na (+)

Nisaidie hapo , Ili niweze kukuamini
 
Back
Top Bottom