Haya ndio magari chaguo langu

Kwa list hiyo ya hayo magari panda panda baiskeli kwanza hamna gari hapo
 
Sio kweli mkuu. Gari zinazozingua zimejaa tele. Haijalishi mmiliki ana pesa au la.

Unafikiri sababu ya serikali kutotumia Range Rover kama magari ya viongozi ni kwamba haiwezi kuzinunua?
 
Mimi Discovery 4 knob gear au 5 ya 2022 Mungu ajaalie Mwaka huu nimiliki moja
 
Yan me nikiiona Nissan Dualis moyo wangu unaenda mbio mbio
 
CX-5 shikamoo.

Ile Sky Active 2.2 Wajapan walitulia.

Matunzo…, nchi zetu hizi diesel inayokuja mtihani. Usipotoa DPF lazima kuna muda itaanza kukufurahisha. Naihusudu pia ila nikiipata nitafanya dof delete kwanza, then model za nyuma natoa coolant junction ya plastic na kuweka ya metal, mafuta nitaweka PUMA na TOTAL na Engen, service kila baada ya KM 5000 - 6000, Oul ni yake recommended tu.
Hapa unaenjoy Mazda power na fuel economy ya ajabu
 
Nashukuru sana. Ila plan yangu ni kununua showroom moja kwa moja au kuagiza Japan au Singapore moja kwa moja.

Asante sana
kuwa makini sana na chuma za kutoka Singapore mkuu, kule nahisi kuna wahuni wengi kama wa hapa bongo tu... niliwahi agiza chuma huko hakuna rangi niliacha kuona. ilikuwa subaru forester
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…