Haya ndio Mapinduzi ya Zanzibar, yamerikodiwa live na waitaliano 1964

Hivi huyu okello alipewa chochote na serikali ya mapinduzi ya zanzibar au nd'o alichinjiwa baharini?
 
mwanangu jamii forum nimekubaki kisima cha great thinkers ila tu vijana magamba wanataka kutuharibia, kweli hii ya Z'bar ni shule tosha kwetu vijana wa kileo.

Labda tuuchukulie ule msemo usmao

UKUPIGAO NDIO UKUFUNZAO

labda kuna somo ndnai ya haya, na wao watasoma
 

Babou; Baada ya salaam.
Nikushuru sana kwa fikra zilizozama. Ni wachache wenye kukaa na kuleta fikra kama unavyofanya. Japokuwa nasikitika na waliopoteza watu wao, binafsi NAAMINI kabisa kuwa ile video ya kwanza; RANGI ya makaburini ni ya KUGHUSHI (kisa ni kutokuwapo quality color videography 1964, na uwezekano eti waitalia waje zenj na color equipment kupigia picha huku BBC wakimnasa Okello kwenye black and White SIUONI; Kwenye You-tube utaona hata hao maiti wamevaa vibandiko-kofia vyao humo kaburini!!!

Lakini hayo na tuyaache. Tulie na kisa, nani kasababisha huu mkasa? Huyu ndiye wa KUBEBA LAWAMA sio yale MATOKEO. Mbona ASP wapo? Ugumu uko wapi kuwauliza kwanini mlimpindua sultani? Waliopoteza watu wao kwenye hili walitakiwa kwanza kujiuliza HII chuki ya kuja KUUANA ilianzia wapi na vipi? Nani aliyehisi kadhulumiwa kimaisha na kisiasa? ni yupi ALIYEACHIA HII HALI HADI KUFIKIA KUUANA? Jina tuu ASP linawakilisha hisia za watu fulani. Kwanini ni watu wa aina hiyo (waafrika na Washirazi?) WHY? lazima kuna sababu.

Wao warudi kwenye chanzo ndipo WAOMBANE MSAMAHA STAHIKI bila hivyo bado hiyo You Tube itajaa mambo yao huku wanazeekea nchi za watu wengine na hao Viongozi wanaowalaumu wote hakuna aliye hai hivi sasa.
 
Kauliwa karume ijekuwa okello?chezea mzee kifimbo cheza!

Waingereza wakamuondosha ukelo kama ndio zawadi yake, otherwise na yeye angufungwa mawe akarushwa bandarini kama walivowafanya akina Kassim Hanga.
 
Wickama


ikiwa wewe unafurahia mauwaji haya sawa,

ikiwa video kuwa ya rangi ndio isiwe ya zamani? inafaa nikuulive unaishi dunia ipi mjomba? hujui leo hapa tunavo video za vita vya kwanza vya dunia na zina rangi? au huamini kwamba hao walioweza kuunda video zikarikodi black and white wanao uwezo wa kuunda technology ya kuzitia rangi video hizo?

maiti wenye kofia kichwani ndio hao walizikwa hai

hoja yako ya kwamba jamaa hajakimbia kuhami nmaisha yao....unajuwa geography ya siwani? wakimbilie wapi, au hujuwi kwamba znz ni visiwa kla kona kona bahari?

Una na video hii basi uone wale ambao wazungu walitaka kuwaondosha znz


 
Last edited by a moderator:

babou

kitachosikitisha ni kitu kimoja tu nacho ni kwamba watu wasomi wanashindwa kutafautisha baina ya mapinduzi na massacre. 1964 kulifanyika mambo mawili

1. mapinduzi

2. massacre.

Tatizo la pili nanialiyefanya mapinduzi hayo.

1. Mipango yote ilitoka Ulaya na USA tunawajuwa kwa majina walioshiriki katika kupanga mapinduzi lakini siwataji humu.

2. Aloshika bunduki ni MTANGANYIKA. Hili ndio linalotukera sisi wazanizbari. Walituulia jama zetu wapatao 17,000 kwa usiku mmoja tu. Jesgi la tanganyika lilipewa mazoezi maalum huko Tanga na likapitia Bagamoyo kidogo kidogo kwenda kujipanga.

3. Ufunguo wa ghala za silaha alikuwa Kakabidhiwa Bwana Mohammed suleiman Mohammed Al Mfadhil, wiki moja hivi kabla ya mapinduzi akapokonywa na kamanda wake muingereza na kupewa mznzibara ambae alitakiwa awabidhi ufungu huo majeshi ya tanganyik amuda ukifika na alifanya hivo. Bwana huyo Mohammed ndie wakanza alouliwa

Sasa nadhani unafamu kwamba jitendo baya walilolifanya ni kuwatarget watu kwa kabila zao na rangi zao.

Nakwa hilo hatuwasamehe watanganyika maisha na musituone kimya lakini litasemewa hilo wakati wake ukifika
 
Nakubaliana na wewe kiongozi,pia kuna clip moja nafikiri ya pili kuna rafudhi ya kiswahili cha kubumba, ONDOKA WEWE TUTAKUUA
 
Sasa mnalia nini kwani hayo si ndio mapinduzi, mlitaka hao waarabu waendelee kuwazuluma na kuwatia utumwani waafrika milele? Kama nyie hodari wa tape mbona hamna tape za maauaji na mateso waliopewa waafrika na hao waarabu kwa karne tele. Uhai wa kila mtu una thamani sio kuwalilia hao waarabu waliokua watawala dhalimu. Wacheni fitna nyie mna lenu.
 

Wewe kweli huwa mnafiki hizi video si ndiyo wewe ulikuwa unazitumia kama ushahidi.

CC; gombesugu, Boko haram,
 
Last edited by a moderator:

Faza; Baada ya Salaam.

Nakushukuru kwa maneno mazuri. Mashaka yangu na ile video ya kwanza ni kuwa zipo kama aina 3 kwenye You-Tube. Kuna moja ni bubu kabisa. Hiyo ambayo ni bubu, inaanzia ndege kujaribu kutua airport ikashindwa na kuondoka na kulikuwa na zogo na ndege ndogo inaungua. Lakini Quality ya Rangi na Photography ya ile video sio ya kuingiza rangi kwenye mkanda wa zamani (panchoromatic to color).

Then Faza mimi nasikitika juu ya hata mtu mmoja kupoteza maisha. Nachosema na ambacho si cha KAWAIDA huwezi kuwakusanya watu 500 chini ya mti wa kivuli ukaanza fyatua bunduki zako bila kutokea mparaganyiko wa HAO WALENGWA. Hayo ndiyo mashaka yangu.

Sina tatizo kabisa na documentary za kina Okello. They look Real.
 
Last edited by a moderator:
Wewe kweli huwa mnafiki hizi video si ndiyo wewe ulikuwa unazitumia kama ushahidi.

CC; gombesugu, Boko haram,

Bosi wako umemuaga?

Nilisema tangu awali hiyo ya RANGI NINA MASHAKA NAYO. NA saabau ni hizi pia nazotoa, hukusoma kiundani post yote kwa vile ulishughulishwa na kutukana watu kwa niaba ya bosi wako (poleni naona uzi wenu umefungwa niliwaonya kuwa hamkujiandaa mkanipuuza!!!!)

Nimesema sina tatizo na documentary ya BBC ya Okello. Na hata Okello mwenyewe kwenye kitabu chake kataja ARABS kama 13,000 waliuliwa, na katika ile post pia nilisema, memory yako vipi?

Na hata hapa nimerudia kumwambia Faza sina tatizo na documentary ya Okello, wewe tatizo liko wapi?
 
Last edited by a moderator:
Wackima


Wa Alaykum salaam,

Kwanza ujuwe kaka, wazungu wanaujuwa ukweli wote wa mapinduzi lakini hawana sababu ya kufanya mchezo wa kuigiza ili kuwapa nguvu waarabu. kwahivo video hizo ni kweli tu

Pili, unahisi kwanini watu wasikimbie, labda hujui kwamba znz ilivamiwa kijeshi na tanganyika ka muelekezo wa mzungu majeshi yalikuwa kila sehemu

Tatu...mpaka hivi majuzi huko znz polisi mmoja anawashika watu 20, na kuwaambia tangulieni kituoni mimi ninapata chai kidogo, akifika kituoni anawakuta wale watu 20 wanamngoja

NNe.. mauwajmabaya zaidi hayakurikodiwa ni yake watu kutiwa katika tanuri z mikate na kunyomwa wakiwa hai, watu kutiwa katika visima vya maji, kule tunaita visima vya ndoo,

na mengineyo
 

Faza; Mimi najua lazima kama umepotelewa ndugu zako lazima upate maumivu kama unayoyaonyesha hapa. POLE. La msingi ukisome kitabu cha Kwakeri Uhuru..... hayo unayoyasema YAMO. Jambo ambalo halimo ni moja tuu.

JEE, ASP walilazimishwa msaada wa kuipindua serikali ya Zenj au huo msaada wao ndio waliomba? Kihistoria inaelekea ASP walikuwa hata wapiga kura wanachukua huko ulikotaja kwa miaka mingi na kuwarudisha baada ya uchaguzi. Utayaona haya kwenye hicho kitabu.

Tanganyika iliombwa msaada wa kijeshi na Msumbiji, Angola, Namibia, nk

Kwahiyo; Faza, kama ASP waliomba msaada, wa kupindua TAFADHALI ANZIA LAWAMA HAPO MITAA YA ZENJ. HUKU BARA NJOO BAADAE MKISHA YAMALIZA
 

Kmbwebwe

u guys are tooo funny

hebu nitafsirie hiI SENTENSI .....................MLITAKA HAO WAARABU WAENDELEE KUWADHULUMU...........kama ulivoitumia katik arisala yako

ulete ushahidi ili tusikuone unabwabwaja tu humu
 
NAUKUUNGA MKONO NDUGU, waache wenye akili za kushikiwa watokwe na mapovu
 

Sawa Sheikh wangu tuko pamoja. Hili la Polisi kuwaambia washukiwa haya tangulieni NAJA limenichekesha sana, huku bara bwana, mahali kama Arusha au kwetu Tarime hukuti mtu ustadh....., haya bwana Pole lakini, tena SERIOUSLY kwa uliowapoteza. M\Mungu awape makazi mema huko waliko. Niliyempa nakala naye alipoteza ndugu. Sio mbaya ukimwandikia hata kama ni PM mention kuwa nime-recommend mfahamiane. Ijumaa Kareem.

cc Gombesugu
 
....inasikitisha..lakini lazima ukweli useme...matokeo ya matumizi ya silaha siku zote huwa hayana heri, na mara zote muhanga wanakuwa ni wanyonge ktk jamii..watoto, wanawake, na vikongwe..hiyo si kwa zanzibar tu, lkn kila mahali ambapo watu waliamua kutumia silaha, hilo limetokea...!lingine ni ukweli kuwa ukoloni haukubaliki...!usultani wa kiarabu ktk eneo hili la afrika ni jambo ambalo lilikuwa halikubaliki na wana waafrika na hata wengine ambao hawana asili ya uafrika lkn wakaweka makazi zanzibar! usultan na uhuru (ambao bado haukutoa haki kwa wengi ) vilikuwa ni ghilba ambazo suala lilikuwa muda ufike ving'olewe...ukoloni ni ukoloni tu...! uwe wa mturuki kwa muarabu, muyahudi kwa mpalestina, mwarabu kwa mwafrika,..ni ukoloni tu..hauwezi kujificha..ubaya mwingine ni fitna inayoambatana na namna /mbinu inayotumika kuutoa.....! lakini mwishowe ukoloni lazima ushindwe na ung'olewe...
 
Wickama


Kwanza nimekupiga LIKE

umenena maneno yanayoingia akilini katika mistari yako


Hicho kitabu cha Dr Harith Al Ghassani, ni maarufu sana na kimejaa ukweli ndani yake

sasa labda unatakiwa ujuwe deep kidogo zaidi ya siasa za znz kabla ya 1964.

Hichi chama ulichokitaja cha ASP, kilizaliwa katika matekeo ya kuungana kwa vyama viwili

1. Shirazi Asociation

2. African Association

wakafanya Afro Shirazi Party (ASP)

Hawa Shirazi Association ndicho chama cha wazanizbari asili,

Hawa African Association ndicho chama cha watanganyika na waafrika wengine waliohamia znz.

Na si marabu alowaita hawa waafrika bali walijiita waafrika wenyewe, hawa ni wale wafanyakazi waliokuja znz kutafuta maisha au waliowafuata wazee wao walokuja znz kutafuta maisha wao wakiwa wadogo.

Nikisema hivi haakuna mtu anayemjuwa mama wa karume, mjomba au kazani zake, hakuna mtu anayemjuwa babu wa ubabani.

watu wa sample hii walikuwa wengi sanaaa siko hizo, znz ilikuwa new york ya afrika mashariki. ndio hawa wakafanya chama chao cha african association, na mila ya chama chao ilikuwa tofauti sana, matusi na vitisho, yaani hiyo haikuwa mila ya kizanzibari. ndio maana siku za kura wakawa wanakwenda kwao tanganyika kulete jamaa zao kupiga kura.

hawa ndio waliokwenda kuchukuwa jeshi la tangika kupindua na ndio maana tunasema mapinduzi ya znz sio halali sababu hayakufanywa na waznzibari wenyewe. ni wanzibara waliokuja kuomba kazi tu znz. kama leo wasomali wafanye mapinduzi uk na wauwe mamilioni ya waingereza nani atakayekubali kwamba hayo ni mapinduzi halali???

sijui upo na mimi???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…