6 Pack
JF-Expert Member
- Apr 17, 2022
- 2,819
- 5,996
Vipi hali zenu ndugu zangu?
Nimekuwa na maswali kadhaa akilini kwangu, lakini kila nikijaribu kuwauliza wana historia wanashindwa kunipa majibu yanayoeleweka. Anyway ngoja niyalete hapa huenda watapatikana wenye majibu yanayoeleweka.
Kwanza kabla ya kuendelea naomba niseme kwamba mada yangu hii haihusiani na kashfa kwa dini yoyote. Kwahiyo naomba wachangiaji mchangie kulingana na mada inavyotaka mchangie, sio kushambuliani kwa vigezo vya dini nk.
Sasa ndugu zangu tukifuatilia vitabu vya dini zetu kubwa mbili yani uislam na ukristo, vinatuambia kwamba mzee wetu au baba yetu wa imani Ibrahim alikuwa na asili ya Iraq, yani alitokea Iraq na lugha yake kilikuwa ni ki Ibrania hii pia ni lugha iliyokuwa inaongelewa Iraq miaka hiyo.
Historia inasema kwamba baadae Ibrahim alipata watoto wawili ambao ni Isihaka ambae ndio chimbuko la waisrael na Ismael ambae ndio chimbuko la waarabu. Kama nimekosea naomba nisahihishwe.
Sasa swali langu la kwanza kwa upande wa uzao wa Ismael.
Ikiwa Ibrahim ambae ni baba wa Ismael alikuwa mu Iraq na lugha yake kuu ni kiibrania.
a) Je, hii lugha ya kiarabu ilitokea wapi na ilianzishwa na nani?
Ikiwa waarabu wametokana na Ismael mtoto wa Ibrahim
b) Je, kabla ya hapo hiyo ardhi ya arabians ilikuwa inaishi watu wa jamii gani?
Swali la pili ni kwa uzao wa Isihaka
Ikiwa Ibrahim ambae ni baba wa Isihaka alikuwa mu Iraq.
a) Je, hawa waisrael tunaowaona leo kina Netanyahu na wengine ni uzao ule ule wa Isihaka au kuna tofauti? Kama ni wale wale waliotokana na uzao wa Ibrahim.
b) Mbona kirangi na kimuonekano ni kama vile wazungu yani hawafanani kabisa na ndugu zao wa Iraq alipotokea babu yao Ibrahim?
Swali la mwisho ikiwa waarabu na waisrael walitokana na uzao wa Ibrahim.
Je, Wahindi na Wachina huko Asia walitokana na uzao wa nani?