DaudiAiko
JF-Expert Member
- Dec 2, 2012
- 372
- 310
Wanabodi,
Hivi karibuni, wana CHADEMA kadhaa wakiongozwa na mwenyekiti wao Freeman Mbowe, walifanya mazungumzo na Rais Samia Ikulu katika kuhakikisha kwamba kuna maridhiano kati ya serikali na vyama vya upinzani. Kwa CHADEMA, maelewano haya yanaweza yakawa na manufaa makubwa lakini kwa kundi lingine la watu, hisia za kudanganywa bado zina tawala mioyoni mwao.
Inawezekana kabisa kwamba mwenyekiti wa CCM (Rais Samia) anaelewa kwamba wana CHADEMA wanapitia mengi katika shughuli zao za siasa na ameguswa kwa kiasi kikubwa mpaka kufikia hatua ya kutaka kumaliza tofauti zao kwa njia ya kistaarabu.
Vilevile inawezekana kwamba yaliyo mkuta Freeman Mbowe yamekuwa tishio kwa yeyote anaye amua kuipinga serikali kwa njia yoyote. Inaezekana kweli kuna urafiki, inawezekana kweli kuna uwoga. Kufahamu kama mazungumzo hayo yatazaa matunda, tujaribu kuangalia madai ya wana CHADEMA.
Haya ndio madai yaliyo wasilishwa kwa Rais Samia,
(Video attached).
1. kurejeshwa kwa mchakato wa katiba mpya kabla ya 2025:
Sidhani kama katiba yetu ina vipengele ambavyo vina ruhusu serikali au bunge kuanzisha mchakato wa katiba mpya au vipengele vipya kutokana na mapungufu yaliyopo lakini ni muda muafaka kwa wote wanaodai mabadiliko haya watoe mapendekezo yao. Rais Samia ameweza kukwepa swali hili mara kadhaa kwenye mahojiano na kwasababu hiyo ni vyema kama tungefahamu kama yeye pekee anaweza kuanzisha mchakato huu bila ya kuwa na ridhaa ya wahusika wengine.
2. Kuundwa kwa tume kufuatilia hoja za wana CHADEMA:
Kama chama kikuu cha upinzani sidhani kama shughuli zao za kila siku hazifuatiliwi na serikali. Ila tume iliyoundwa na vyama vya upinzani inaweza ika rasimisha yanayo endelea kwa kuwasilisha changamoto zote.
3. Serikali kuhakikisha kwamba chaguzi zinazo fanyika ni za huru na haki:
Kwanza kabisa, wana CHADEMA wana amini kwamba uchaguzi hauwezi kuwa wa huru na haki kama tume ya uchaguzi sio huru. Ukizingatia umeshindwa kwa asilimia ngapi, hilo linaweza lisiwe kweli. Rais Magufuli akishinda uchaguzi kwa asilimia 88, ameshinda kwasababu amechaguliwa na watanzania walio wengi. Kwa hilo, ni muhimu kwa wana CHADEMA kupata ridhaa ya wananchi walio wengi kabla ya kusingizia au kufuatilia uwepo wa tume ya uchaguzi.
4. Uhuru kwa vyama vya siasa kufanya shughuli za siasa:
Katiba inaruhusu shughuli za siasa kufanywa na vyama vyote. Kipengele 18(1) cha katiba kinaruhusu mtu yoyote kutoa maoni na kutoa habari kwa kutumia chombo chochote. Katiba yetu haina tafsiri ya neno "Uchochezi" bali kila mtu ana haki ya kutoa maoni yake.
5. Kufutwa kwa kesi za siasa na kuachiwa huru kwa wafungwa wote wa siasa:
Kesi haiwezi kufutwa hivi hivi. Katika kutaka hilo lazima tuzingatie kuwa na mahakama iliyo huru. Kama kweli wahusika sio wahalifu basi sheria ifuate mkondo wake.
6. Kufutwa kwa sheria kandamizi nchini:
Swali linakuwa lile lile, sheria kandamizi zipi?
7. Kurejea kwa watu walio uwawa au kupotea kwasababu za siasa:
Kitu kinacho aminika ni kwamba mtu yeyote anayejiunga na upinzani lazima afuatiliwe na serikali. Kwa kudai kurejea kwa watu hawa, moja kwa moja unakuwa umei tuhumu serikali kwa kuwa dhuru kwa njia moja au nyingine. Kama ni kweli, ni muhimu kuhakikisha kwamba mambo kama haya hayajirudii
8. Usalama kwa viongozi wa siasa:
Katika kuweka hali tulivu ya siasa nchini, ni muhimu kwa pande zote mbili kushiriki kwenye siasa safi. Sio sahihi kwa Tundu Lissu na Godbless Lema kuishi nchi zingine kwa kuhofia maisha yao nchini. Tanzania ni yetu sote, tupingane kwa hoja na sio kwa mikuki
9. Kuondolewa bungeni kwa waliokuwa wana CHADEMA:
Dhumuni ya maridhiano ni pamoja na kusisitiza uhumihu wa mazungumzo tunapokuwa na changamoto. Kususia bunge au uchaguzi bila mazungumzo inaashiria kukataa kufanya maridhiano. Vile vile hatua zilizochukuliwa na wana CHADEMA zinaonyesha kwa asilimia mia kwamba hawakubaliani na kuwa na wawakilishi hao bungeni. Sio sawa kwa bunge kuwa ng'ang'ania.
10. Kuzuia ukandamizwaji wa haki na demokrasia:
Kwa hili, tufahamu kwamba haki sio haki ya siasa tu bali haki inahusisha vitu vingine vingi ambavyo havina uhusiano wowote na siasa. Baada ya kufahamu hilo, tukubaliane kwamba Tanzania ni nchi ya amani na wananchi wake wanaishi kwa amani na uhuru. Labda demokrasia, narudia tena, tushindane kwa hoja na sio mikuki