Nikifa MkeWangu Asiolewe
JF-Expert Member
- Feb 26, 2024
- 6,944
- 14,351
- Thread starter
- #121
Panafaa sana mkuuUmesimulia vizuri sana mpaka kumpa mtu hamasa ya kwenda kupanda.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Panafaa sana mkuuUmesimulia vizuri sana mpaka kumpa mtu hamasa ya kwenda kupanda.
Duh jumapili nitakuja hanang nipo hapa soera ya kweraKiroba kabisa maana tulikuwa wengi. Halafu sijawahi ona madhara ya mirungi mimi
Duh jumapili nitakuja hanang nipo hapa soera ya kwera
Hongera sana mkuu.Tanzania ni Nchi yetu sote hivyo ni wajibu wa kujivunia vivutio vilivyomo.
Mlima Hanang uliopo Katesh manyara ni mlima wa tatu Kwa urefu hapa Tanzania No1 ukiwa ni Kilimanjaro No2 mlima Meru
Na No3 ni huu mlima Hanang ukiwa na Mita 3417 kama sijakosea.
Nikiwa viunga vya huko niliona Nami nisiishie tu kuuona bila kupanda. Nikiwa na rafiki yangu mmsai tuliazimia kupanda kihuni (Bila kibali) Kwan mwenzangu alikuwa anajua njia za Chocho za kuupanda.
Safari ilikamilika tukiwa tumebeba vitu mhimu Kwa ajiri ya kupanda kwa mara ya kwanza tulipanda kiangazi kwenye mwezi wa8 Hivi na Kwa mara ya pili tulipanda mwezi wa kumi.
VIVUTIO NA MAAJABU YA MLIMA HANANG
Ukiwa mlima Hanang mwanzoni tu Kuna pori la miti asili mbalimbali mizuri sambamba na mirungi.
Japo hairusiwi kukata mti au Jani ama kitu chochote mle hifadhini lakini manyokaa sisi tulichuma mirungi ya kututosha na kuanza kutafuna.
Kuna matunda fln Hivi yanafanana Kwa mbali na dragon fruit pia utayaona msimu wake.
Hali ya hewa ni rafiki sana ukiwa mwanzoni mwa mlima lkn kadiri unavyozidi kupanda juu hubadirika kuwa na unarudi kiasi na miti hupungua kabisa.
Mlima Hanang sio mlima mmoja Kwa jinsi nilivyoona Mimi. Pindi unapopanda unakuwa unaona kileleni ni pale lakini ukifika pale juu unaona mlima mwingine Kwa mbele mrefu kuliko hapo ulipo.
Utaendelea kuona hivyo hivyo zaidi ya milima 9 ama 12 ndo unafika kileleni.
Kuna sehemu unapita Kwa umakini mkubwa sana kwani ikitokea ume umeteleza na kuporomoka sidhani kama utaweza kupona ama kuokolewa.
Ukikaribia kileleni Kuna mapango 3 tofaut na umbali yapo tofauti Yale mapango unaweza kaa ukalala kabisa au hata mvua ikiwakuta kule mnaweza kujihifadhi pasipo shida yoyote Ile.
Mawingu ya mvua daima yatakuwa yanawafunika na hii huambatana na ukungu na vimanyunyu Hivi.
Wingu la mvua ni sawa na ukungu mzito sana mwenzio akiwa mita5 Toka ulipo wewe huwezi muona au utamuona Kwa shida sana. (Picha zote zenye weusi ni Wakati tukiwa ndani ya ukungu mzito wa wingu la mvua)
Miti Ina harufu nzuri sana kule mlimani ya kijani kibichi muda wote vile vile Kuna miti kama Ile Xmass namna unavyouna mti wa Xmass na kule mlimani ni hivyohivyo sema wenyewe hauna Maputo na yule father Xmass 😆
Kule juu Kuna miti fln ukiangalia kana kwamba imekauka lakini ukivunja katawi kadogo unagundua ule mti ni mbichi kabisa Cha ajabu hauna majani yoyote.
Pia utaona mimea fln imekaa kama dodoki la kuogea inatililisha maji ya ubaridi meupe mazuri.
Ukichukua huo mmea na ukakamua nakunywa maji yake yenye ladha nzuri na ya kuvutia mnoo (SIKUJUA kama ni salama ama la japo mwenyeji wangu alinambia hayana shida)
Maji kutoka katika kati ya miamba. Hii pia utaona hasa ukifika sehemu yalipo pango no2-3 utaona maji yakitoka kwenye mwamba.
Kuna nyasi amazing sana huko juu yaani hata ukitaka kulala Haina haja ya kutandika nguo unajilaza vyema kabisaaa kwanza haziwashi yaani full amazing!! 🤩 🤩
Basi ukifika kileleni Sasa hata Katesh huioni Tena utakuwa unaona vijiji vya mbali sana Kwa ukaribu sana Nangwa utaiona nayo Kwa machale sana.
Ukiwa kileleni utaona ziwa la magadi sijui kama lipo karibu na mlima lkn ukiwa juu unaona kana kwamba ukiruka unatua kwenye Ziwa Hilo la magadi (chumvi)
Huu ubao upo Barbara kuu ya Arusha to siginda.
View attachment 3118958
Miti yenye harufu nzuri ya kuvutia Sana. Msukuma Mimi ilibidi niifikishe kwenye nguo zangu walau harufu yake ibakie😹😹View attachment 3118963
Moja ya mapango yaliyomo mlimani huko juu ukifika hapa matumaini ya kutoboa ni makubwa sana.View attachment 3118964
Moja ya sehemu mbaya sana hapa ukiteleza kwisha habar yako.
View attachment 3118971
Hapa ndani ya wingu ama ukunguku mzito sana.View attachment 3118975
Kama unavyoona Kwa mbali ndo Ziwa la magadi wengine huita Ziwa la chumvi.
Maelezo ya ziada.
Mlima huu unapo upanda daima utafuata mwinuko maana hivyo Huwa ni ngumu sana kutoboa ni mlima mkali wenye mteremko mkali kiasi kwamba iwapo jiwe litaporomoka lazima lilete madhara Kuna sehemu unapopanda unapanda kama mbwa yaani unatumia miguu na mikono Yako wiwili😂😂
Japo sio lazima ufanye Hivi lakini wengi hufanya hivyo kuragisiha upandaji.
Ukiwa pale mwanzoni Kuna vitu nilijiuliza sana. Unakuta mtu wa kienyeji kabisa lakini ule mti una jina la kizungu Hadi mirungi nayo Ina majina ya kizungu karibia Kila mti umeitwa majina majina ya watu wakuja ama ya mataifa ya kizungu huko!!
Nilijiuliza hii imekuwaje Hadi na migadogado Ina majina ya kizungu Ili Hali wenyeji wa eneo like wanaijua Kwa majina yake?
Nikakumbuka hata Ziwa Victoria lilinguduliwa na mwanamama aliyeitwa Victory.
Karibuni.
Napenda sana HikingUkiwa unapanda utaona jinsi wingu linatanda juu Kwa Uzuri sana na inakupa hamasa ufike maeneo hayo uingie mawinguniView attachment 3119220
Inakuwaje mkeo asiolewe?View attachment 3119221
Wengi hawakufika kileleni.
Uko sawa mkuu nimeenda google nimeona niwa Saba kabisa karibia milima4 ipo Kilimanjaro huko yte! Ahsantee sanaHongera sana mkuu.
Big up.
Umeshuka nayo vizuri mno!!
Hapo kwenye mlima wa tatu kwa urefu inaweza ikachanganga kidogo.
Kilimanjaro ina vilele vitatu, virefu zaidi, toa shira ambayo sio kirefu sana.
Inabaki Mawenzi na Kibo sijui kwa nini huwa wanavichanganya ila kiuhalisia Kibo ndio Kilimanjaro halisi, ambayo yenyewe pia ina vilele vitatu.
Gilmans, Stella na Uhuru. Uhuru ndio Highest point sasa.
Mawenzi haipandiki kavu kavu
Yeah!Uko sawa mkuu nimeenda google nimeona niwa Saba kabisa karibia milima4 ipo Kilimanjaro huko yte! Ahsantee sana
Nje ya maada mkuu lianzishie Uzi hili😂😂Inakuwaje mkeo asiolewe?
Ahsantee sanaYeah!
Ila hongera sana master.
Ume share kitu kizuri
Naam Kwa hakika hatuwezi lingana katika Mipangilio nipo tiyari kusahihishwa. Nitashukuru sana.Wewe si mzuri katika simulizi, unahitaji muongozo
Ms R tutafika kileleni ? Wengi hawakufika kileleni ujue 😁View attachment 3119221
Wengi hawakufika kileleni.
Kijana kijana kijana,,nimekuita mara tatuMs R tutafika kileleni ? Wengi hawakufika kileleni ujue 😁
Oi Mzee mwenzangu Mpaji Mungu namuuliza Mwanao tutafika kileleni? 🤔🤔🤔
Nini?Kijana kijana kijana,,nimekuita mara tatu
itika vizurNini?
Naaam 🙏itika vizur
Naaam 🙏itika vizur