Pre GE2025 Haya ndiyo makosa ambayo BASATA wanamtuhumu Nay wa Mitego kutokana na wimbo wake wa "Nitasema"

Pre GE2025 Haya ndiyo makosa ambayo BASATA wanamtuhumu Nay wa Mitego kutokana na wimbo wake wa "Nitasema"

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,

Ndio walikuwa wanajitapa na uhuru wa kutoa maoni kuongezeka. Kauli za kichochezi inatakiwa kutolewa maana. Huku ni kutufanya mabubu wazi wazi.

======
HATI YA MAKOSA

KOSA LA KWANZA

Kutoa wimbo kwa walaji bila kibali, kinyume na Kanuni ya 25(1) ya Kanuni za Baraza la Sanaa la Taifa, 2018.

MAELEZO YA KOSA

Msanii Emmanuel Elibariki Nay wa Mitego mnamo tarehe 24/09/2024, huku ukijua kwamba ni kinyume na Kanuni, ulitoa wimbo unaoitwa NITASEMA kwa walaji kabla ya kupewa kibali cha kuthibitisha kuwa maudhui yake yamezingatia maadili.

KOSA LA PILI

Kutoa wimbo ambao maudhui yake yanahamasisha uchochezi kinyume na Kanuni 25(6)(d) ya Kanuni za Baraza la Sanaa la Taifa, 2018.

MAELEZO YA KOSA

Msanii Emmanuel Elibariki Nay wa Mitego mnamo tarehe 24/09/2024, huku ukijua kwamba ni kinyume na Kanuni, ulitoa wimbo unaoitwa NITASEMA ambao baadhi ya mashairi yake yanahamasisha vitendo vya uchochezi dhidi ya Serikali kwa madai kwamba Serikali inahusika katika kufanya vitendo vya utekaji na mauaji ya watu.

KOSA LA TATU

Kutoa wimbo ambao maudhui yake yanapotosha jamii, kinyume na Kanuni 25(6)(b) ya Kanuni za Baraza la Sanaa la Taifa, 2018.

MAELEZO YA KOSA

Msanii Emmanuel Elibariki Nay wa Mitego mnamo tarehe 24/09/2024, huku ukijua kwamba ni kinyume na Kanuni ya 25(6)(b), ulitoa wimbo unaoitwa NITASEMA ambao baadhi ya mashairi yake yanapotosha jamii kwa kuiaminisha kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameshindwa kutekeleza majukumu yake hivyo nchi inazama, na kwamba miradi ya maendeleo ilioachwa na mtangulizi wake imetelekezwa.

KOSA LA NNE

Kutoa wimbo ambao maudhui yake ni kukashifu mataifa mengine kinyume na Kanuni 25(6)(h) ya Kanuni za Baraza la Sanaa la Taifa, 2018.

MAELEZO YA KOSA

Msanii Emmanuel Elibariki Nay wa Mitego mnamo tarehe 24/09/2024, huku ukijua kwamba ni kinyume na Kanuni ya 25(6)(h), ulitoa wimbo unaoitwa NITASEMA ambao baadhi ya mashairi yake yanakashifu nchi ya Rwanda na nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa kudai kwamba nchi hizo hazina usalama, jambo ambalo linaweza kusababisha nchi ya Tanzania kuingia kwenye mgogoro wa kidiplomasia na nchi hizo.

E.E. Buganga
Kny: KATIBU MTENDAJI
27/09/2024​

Nakala: Katibu Mtendaji aione kwenye Jalada

Soma Pia:
~
Ney wa Mitego aitwa BASATA kujadili wimbo wake wa ‘Nitasema’
~ Kuelekea 2025 - Wasanii kujiingiza kwenye siasa na kuwa machawa ipi faida yao kama nao wanashiriki kuingiza wananchi shimoni?

Wasanii wengine waliowahi kufungiwa na BASATA soma;
~ Utata: Msanii Roma Mkatoliki na wenzake wakamatwa/tekwa nyara

nay.jpg
nay 1.jpg
UPDATES
- BASATA waufungia wimbo wa Nay 'Nitasema'
 
Katika watu hawajui kuimba ni huyo Ney wa mitego alikosea kila kitu kwanzia kuchagua jina lake la sanaa mwanaume unajiitaje Ney alaf wa mitego!
Aachwe asifungiwe
Ajabu,mwanamuziki kuwa na kithethe
 
Back
Top Bottom