Haya ndiyo mambo ya ajabu niliyowahi kuona na kushuhudia kwa macho yangu, sitoyasahau katika maisha yangu

Aliponea hospital?
Yes, hiyo ilikuwa ni miaka 15 iliyopita na mwaka 2018 alipata tatizo lingine linalofanana kama hilo

Hilo tatizo lilikuwa kama ni ukichaa, watu wakasema amelogwa, mume wake ikabidi ampeleke kwa kanisani aombewe.

Baadaye zikarudi taarifa mchungaji kapigwa na kiti cha plastic halafu kuna uharibifu aliufanya. Ikabidi uongozi wa kanisa umfunge kwenye chumba ambacho yuko pele yake.

Halafu mikono wakaifunga kwenye bomba la chuma, sisi tunaenda kumuona tunakuta ile kamba imemchuna mikono mpaka damu kwasababu alikuwa anahangaika kujitoa kwenye ile kamba.

Niliingiwa na hasira kwa jinsi nilivyomuona Sister ila nilijizuia ikabidi niombe kumchukua Sister kumpeleka hospitali.

Huko alikutwa na Malaria ya kichwa akapewa dripu za kutosha akaandikiwa na dawa

Ambapo mpaka saizi bado yupo kwenye dose ya hizo dawa
 
Is she alright?
Ina maana mpaka mda huu dada hajapona? maisha haya acheni tu
 

Kweli mzee
 
Is she alright?
Ina maana mpaka mda huu dada hajapona? maisha haya acheni tu
Tatizo lililomuanza miaka 15 iliyopita alipona completely

2018 aliugua Malaria ambayo ilipanda kichwani na kumfanya awe kama chizi.

Maana hadi wodi za machizi amekaa

Alipotibiwa alipewa na dawa ambazo alikuwa anameza vidonge 20 kwa siku

Na sharti alilopewa ni kuwa asi-skip dose hata siku moja kwani kufanya hivyo kunaweza sababisha ugonjwa umrudie tena.

At that time alikuwa anakunywa dawa ila yupo vizuri kila kitu kipo katika utimamu wake, hicho ndio kilichomfanya aanze kuona uvivu kunywa dawa.

Kwa hiyo baada ya ku skip dose ni kweli ugonjwa ulimrudia tena, na ndio hapo akaanza upya na saizi kaanza kupunguziwa idadi ya vidonge naskia anameza vitatu kwa siku badala ya 20 kama ilivyokuwa zamani.
 
Ni kweli, huyu jamaa alikua na wenge zake tu πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Upo sahihi kwa maoni yako.
 
Pole mkuu
 
Bibi kadhihirisha kuwa na sauti ya kumtoa nyoka pangoni.

Ila dunia ina mengi mno.
 
Ngoja nitakuletea na shuhuda yangu tulipompeleka brother kwa madaktari bingwa wakamfanyia vipimo nakusema hakuna anacho umwa.

Lakini yeye kila inapofika usiku kucha analia vibaya mno nakudai kuwa anachomwa chomwa sindano analia vibaya mno hakuna anayelala.

Tukampeleka hospital akalazwa hali ilikua ni ile ile, mwanzo walizani ni mgonjwa wa akili mchana hakuwa na shida ila ilipofika usiku alianza kulia sana huku akijikunja kunja nakudai kuwa anachomwa sindano zinazompa maumivu makali.

Alikuja dokta mmoja pale alimtazama sana nakusema jamani vipimo vyetu havioni ugonjwa wa namna yoyote jaribuni njia mbadala labda inaweza kutatua tatizo.

Kesho yake asubuhi wazeee walimpeleka wanapopajua wao alikaa kwa muda wa siku tano na walitoa majibu yakua kaacha kulia na kuchomwa chomwa hakuna hasikii Tena kiufupi Hilo tatizo lilikwisha na broo alirudi katika famililia yake nakuendelea na harakati zake.

Hiyo nilishuhudia kwa macho yangu pasipo kusimuliwa na mtu yoyote kuwa madaktari walishindwa kung'amua tatizo na wakatoa ushauri kuwa apelekwe katika tiba mbadala.
 
Tajiri anadai nyoka wake πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…