Haya ndiyo mambo ya ajabu niliyowahi kuona na kushuhudia kwa macho yangu, sitoyasahau katika maisha yangu

Haya ndiyo mambo ya ajabu niliyowahi kuona na kushuhudia kwa macho yangu, sitoyasahau katika maisha yangu

white-coffee-cup-with-fire-inside-glass-is-placed-wooden-table_39344-32.jpg
 
Endelea kuamini wenge hivyo ni vitu ambavyo Mimi huwa vinanifikirisha mpaka Sasa
Utaona ni uongo kwa sababu hayajakutokea na hujashuhudia ila Kama umeshuhudia hutokuja na hizo ngonjera sijui hospital sijui malaria.
mbn wengine tunatembea usiku mnene tena njia za makaburin lakini hatuwaoni hao majini na walozi, au wana watokea watu special.

Hao wavunja nazi na wanao oga mabarabarani nitaamini wapo lakini uchawi na majini hivyo vitu havipo.
 
Ninaposema kuwa nimeshuhudia nakuona kwa macho yangu siyo kwamba nimekuja kutunga story ili niwafurahishe hapana

Tena humu Kuna watu wameona mazito kuliko haya ninayoyazungumza kiufupi tu Mimi sinywi pombe wala sivuti bangi hata sigara pia.

Sasa basi Kuna watu walikua wanauliza mwisho wa Yule afsa niliyeua nyoka wake Nini hatima yake.

Kiukweli kwa namna alivyokua anafoka nakuhuzunika nakulalamika sana nililiona hii ni serious ishu,

Niliomba msamaha ukizingatia alikua ni meneja msaidizi niliona kabisa kibarua kitaota nyasi na mwisho wa siku alinielewa akanisihi sana nisipende kuua ua wanyama ambao hawana tatizo na wewe.

Baada ya siku tatu Yule afsa alisafiri kuelekea kijijini kwao aliomba rikizo ya wiki mbili akidai kuwa ana matatizo huko kwao muhimu

Hizo taarifa nilizipata kwa sekretali wake nilipoonda kumuulizia baada yakuona simuoni Tena.

Lakini hakurudi Tena mpaka Mimi nilipomaliza mkataba wangu, na mpaka natoa huu ushuhuda sijui alipo kwa Sasa.

(5) SITOSAHAU NILIPOPIGA PAKA MAWE USIKU BAADA YA SIKU TATU NILIKUTANA NA BABU MMOJA AKANILALAMIKIA KUWA NIMEMVUNJA MIGUU.

Naam, nilikuwa nimepanga chumba morogoro chamwino chini huko panaitwa mtaa wa mgulasi ni uswahilini kwa kweli miaka ya nyuma palikua panatisha sana

Kipindi natafuta chumba dada yangu aliniambia huko siyo pazuri Kuna wahuni wakabaji Mimi niliona Kama ananizingua na kweli kulikua na Mambo ya ajabu ajabu sana kipindi kile.

Nilipata nyumba moja hiyo nyumba ilikua inawapangaji wanne mwenyenyumba alikuwa haishi pale.

Nilikaa wiki moja tu, lakini nilikua nakeleka sana na kelele za mapaka yaliyokua yanalia Kama watoto wadogo hasa inapofika mishale ya saa sita usiku, watalia mpaka saa tisa au kumi hivi.

Aisee asikuambie mtu wale paka walikua Kama siyo chini ya sita, wakianza kulia wanalia sauti za binadamu haswa watoto wadogo wanalia kwa kupokezana.

Nilichoshwa na hiyo hali niliwauliza wapangaji wenzangu walinijibu kuwa wao wamezoea kitendo Cha hao paka kuja kulia usiku kucha kwenye ule uwanja wa ile nyumba.

Siku moja niliamua kudeal nao wale paka, niliandaa mawe makubwa yakutosha nikayaweka geto, sikuhiyo sikutaka kufunga mlango niliuegesha tu sikufunga nakomeo niliendelea kusubiri mida yao ili nideal nao.

Kweli ilipofika mida yao walifika wakaanza kulia, nikasema yes muda ndiyo huu, niliwachungulia pale mlangoni nikawapimia nipige wapi.

Kweli nilifungua mlango gafla nikarusha mawe mfululizo, mawe mawili yalienda bure ila Kuna mmoja lilimpiga mpaka likambadili direction kipindi anakimbia na alilia mlio wa kuonyesha kapigwa.

Nilirudi kulala lakini sikusikia Tena makelele siku hiyo, kesho yake wapangaji wakawa wananisifia kwa kuwapiga wale paka.

Baada ya siku tatu kupita, asubuhi nilikua nawahi mishmishe, nilisalimiana na baby mmoja kipofu aliyekuwa anaishi nyumba ya nne kutoka niliyokuwa nimepanga.

Yule babu nikipofu huwa anashinda nyumbani tu na ni nadra sana kumuona maana Mara nyingi hushinda ndani.

Nilipomsalimia akaniita nakuniambia "kijana ile siku ulivyorusha mawe uliniumiza mguu wangu"

Kiukweli nilishikwa na butwaa, Yule babu hakuendelea Tena kuzungumza na wala hakusubiri nimjibu alinibia tu "kijana wewe nenda kwenye mihangaiko yako"

Niliondoka pale nikiwa Sina Imani kabisa nakuona Kama Yule babu Kuna kibaya atakuja kunifanyia.

Zilipita siku Kama tatu hivi nilimuona mwenyenyumba pamoja na balozi au mjumbe wa nyumba kumi jioni walikuja wakaniambia nihame na mwenyenyumba alinirudishia pesa yangu wakanipa siku mbili za kutafuta chumba.

Nilipouliza kwa nini mnanihamisha, mwenyenyumba alidai kuwa anataka kuishi yeye na hiyo ni dharura sitakiwi kukaidi amri.

Niliona isiwe kesi niliamua kuhama lakini mpaka nahama Yale manyau yalikua hayalii kabisa sijui kilichojiri baada yakuhama maana sikutaka Tena kuishi chamwino nilihamia kihonda.
 
Broo haya ni Mambo niliyoyaona Mimi aisee, Sasa sitoweza kulazimisha uamini

Mimi ninaimani Kuna watu wapo humu wameona makubwa kuliko haya ninayoyasimulia humu.
 
Ngoja nitakuletea na shuhuda yangu tulipompeleka brother kwa madaktari bingwa wakamfanyia vipimo nakusema hakuna anacho umwa.

Lakini yeye kila inapofika usiku kucha analia vibaya mno nakudai kuwa anachomwa chomwa sindano analia vibaya mno hakuna anayelala.

Tukampeleka hospital akalazwa hali ilikua ni ile ile, mwanzo walizani ni mgonjwa wa akili mchana hakuwa na shida ila ilipofika usiku alianza kulia sana huku akijikunja kunja nakudai kuwa anachomwa sindano zinazompa maumivu makali.

Alikuja dokta mmoja pale alimtazama sana nakusema jamani vipimo vyetu havioni ugonjwa wa namna yoyote jaribuni njia mbadala labda inaweza kutatua tatizo.

Kesho yake asubuhi wazeee walimpeleka wanapopajua wao alikaa kwa muda wa siku tano na walitoa majibu yakua kaacha kulia na kuchomwa chomwa hakuna hasikii Tena kiufupi Hilo tatizo lilikwisha na broo alirudi katika famililia yake nakuendelea na harakati zake.

Hiyo nilishuhudia kwa macho yangu pasipo kusimuliwa na mtu yoyote kuwa madaktari walishindwa kung'amua tatizo na wakatoa ushauri kuwa apelekwe katika tiba mbadala.
Mkuu hicho ulichokiandika kimewatokea wengi na kitaalamu kimepewa jina la 'Chronic psychogenic pain" ni matokeo ya ubongo kutengeneza maumivu ambayo hayapo

Ni mpaka umpate mtaalamu wa maswala ya cognitive behavioral therapy (CBT)

Lakini pia lipo kundi lingine la watu wa "Munchausen syndrome" hawa ni wale ambao wana fake kuumwa
 
ACHA KIHEREHERE
 
Sister yangu alishawahi kutana na hili tatizo (anaona vitu ambavyo havipo)

Mnaweza mkawa naye pamoja afu ghafla akaanza kupiga kelele kuwa "niache, niache" huku akijificha kama ishara ya mtu anayetaka kumchukua bila ridhaa yake.

Anakuwa serious analia na kulia na sometimes katika purukushani unakuta mpaka anaji jeruhi, anasema watu anaowaona wanatisha wana meno marefu na nywele nyingi wanamuambia twende nyumbani

Mara adai kutokewa na watu waliokufa wakisema "twende ambapo tupo sisi"

Makuzi yetu ya kiafrika na uduni wa elimu ulifanya watu wakubali majibu yasio sahihi kuwa ni ushirikina kwa kuyaamini macho na ubongo wetu.

Lakini tulipoenda kwa Doctor ambaye ni mbobezi kwenye maswala ya mental health alitusaidia na sasa hilo tatizo halipo tena

Sayansi inasema muda wote haupaswi kuyaamini macho, masikio na ubongo wako

They can play fool sometimes
Hao madaktari si ndio huwa wanawaambia waende kwa wataalam mambo yakishindikana
 
Dunia Ina Mambo mengi sana na ni rahisi sana kupinga au kubisha Kama hayo Mambo ya ajabu hujayashuhudia na pia ni Bora uwe unasimuliwa tu na usije kukutana nayo maana unaweza ukadhurika ama ukawa hai.

Naam leo nimepata muda nikaona ni Bora nishee haya machache niliyokutana nayo katika huu ulimwengu,

(1) sitosahau nilipokutana na mtu mrefu asiyekuwa na mwisho inasadikika ni jini

Yapata mishale ya saa saba usiku, niliwasha pikipiki yangu kutoka Kambarage kuelekea Matanda kwa wale wenyeji wa Shinyanga wanayaelewa haya maeneo.

Nilikuwa nafanya kazi ya ulinzi kitengo Cha supervising na kupiga patrol kuwaausha walinzi usiku kwa hiyo mishale ya saa saba , saa sita ,saa nane mpaka saa tisa ndyo ilikuWa mida yangu kwenda kuwapatrol walinzi ili kazi za watu ziwe salama.

Nakumbuka nilitoka nyumbani vizuri pale Kambarage nikafika mitaa ya ofisi ya mkuu wa wilaya ili nishike barabara ya kuingia Tanesco Matanda.

Nikawa nakaribia kupita geti la ofisi ya mkuu wa wilaya, Mara gafla nikaona mtu amevaa nguo nyekundu akiwa amesimama katikati ya barabara ninapoelekea Mimi,

Kiukweli haikunishitua nikaendelea kusogea maana ile njia huwa napita sana, nilishawahi kukuta watu wanaogeshana usiku wa manane, Mara watu wanavunja Nazi kwa hiyo nilijua tu huyo aliyevaa nguo nyekundu ni mtu Kama wale ninaowaonaga.

Sasa nilipokuwa naendelea kumkaribia cha ajabu alikuwa anazidi kuwa mrefu na njiani hataki kutoka ilinibidi nipunguze spidi huku nikishusha gia za pikipiki mpaka namba moja hapo nilikuwa nishamkaribia kwa ukaribu na alikuwa ni mrefu kichwa hakionekani hana mwisho.

Sikuamini nilichokiona na ndiyo ilikuwa ni Mara yangu ya kwanza kukutana na kitu kama kile, niliamua kuzima taa na kuziwasha, kitendo cha kuzima nakuwasha tu, lile dubwana lilipotea kama upepo sikuliona tena akili yangu ilibadilika nilikimbiza pikipiki kama mwendawazimu kurudi nyumbani maana sikuendelea na Safari yangu, siku iliyofuata niliumwa sana nililala ndani bila kutoka kwa muda wa siku tano.

(2) NILIUA NYOKA WA MTU, MWENYE NYOKA ALINIFUATA AKAANZA KUNIDAI NYOKA WAKE.

Miaka ya nyuma nilikuwa nafanya kazi katika kiwanda kimoja cha chai huko Iringa kwa majina sitotaja, siku hiyo ilikuwa ni siku ya usafi tulikuwa tunasafisha maeneo ya kiwanda maana siku ya usafi wa mitambo na mazingira kwa ujumla uzalishaji husimama.

Mimi nilikuwa nafyeka majani, lile eneo tulipangiwa wawili lakini mwenzangu kwa muda ule alienda kunywa chai atakaporudi na mimi niende tulipeana zamu.

Kipindi nafyeka gafla nikaona nyoka mwezi anakuja upande wangu, ni mrefu mwembamba, Mimi binafsi nyoka nawajua ni moja Kati ya nyoka wenye sumu kali.

Sikutaka kushangaa ikanibidi nimuue, nilimkata na kwanja tenganisha kichwa na kiwiliwili akafa.

Mara punde alikuja mmoja wa maafisa wakubwa pale kiwandani akihema kama mtu aliye na presha, alinifokea na machozi yakimtoka alisema "kwanini umeua nafsi yangu"

"Huyu ndiyo ananifanya niishi hapa"

Nilishikwa na butwaa sana, maana yule alikuwa ni boss mkubwa nilibaki najiuliza huyu boss na manyoka wapi na wapi.

Na hakuishia hapo aliendelea kunitishia amani akidai nyoka wake arudi na ule ndiyo ilikuwa ni ulinzi wake.

Mimi nilipoona hivyo nikajua kabisa hii ni serious sana nilimuomba msamaha sana nikamwambia sikujua.

Hakika like kitendo cha mtu kusema nimeua nafsi yake kilinistaajabisha sana.

(3) SITOSAHAU NILIPOMKUTA MMASAI AKIONGEA NA CHUNGU NA CHUNGU KILIMJIBU.

Hii nimeshuhudia kwa macho yangu mpaka niliona Kama ninaota, nakumbuka tulikuwa kwenye mitihani ya darasa la saba tena ulikuwa ni muda wa mapumnziko.

Nilikwenda kutafuta darasa moja ambalo lilikuwa lipo mbali na yale tuliyokuwa tunafanyia mtihani nikiwa na lengo la kwenda kupumnzika nitulize akili yangu kidogo.

Nilipokuwa nakaribia kwenye hilo darasa nilianza kusikia sauti ndipo nilipoamua kuchungulia, nikamuona mwanafunzi mwenzangu mmasai, tuliyekuwa nae darasa moja na yeye alikuwa nafanya mtihani wakuhitimu darasa la saba.

Kilichonishangaza alikuwa ameweka chungu pembezoni kabisa ya darasa juu ya dawati kile chungu kilikuwa kinawaka Moto.

Sasa kipindi naendelea kuchungulia alikuwa anaongea peke yake kwa lugha ya kimasai huku akiwa amekunja mikono yake na amenyenyekea kweli mbele ya hicho chungu,

Alipomaliza kuzungumza kile chungu kilimjibu kwa sauti ya kike, kilizungumza kwa lugha ya kimasai pia, niliogopa sana kile kitendo niliinama chini nikasota kwa hatua kama tano hivi nikakimbia sana kuondoka kwenye hilo eneo.

Muda wa mtihani ulipofika masai nae akaja kupiga pepa, tulivyomaliza mitihani sikumuona yule jamaa mpaka sasa ila siku hiyo sikuwa na amani na nilimuogopa sana.

(4)NILISHUHUDIA MAMA WA KISUKUMA AKIIMBA NYIMBO NZURI NA KUMTOA NYOKA TOKA MAFICHONI.

Ukistaajabu ya Musa basi utayaona ya Firauni na wanasema tembea uone mengi na ujifunze.

Nikiwa bwana mdogo nilikwenda kumtembelea shangazi Shinyanga Kijijini baada yakufunga shule.

Siku hiyo nakumbuka ilikuwa ni mchana mishale ya saa 8 mchana tulikuwa tumekaa karibu na mlango tunakula chakula cha mchana.

Mara gafla alipita panya buku kwa spidi ya ajabu sana bila kujali chochote yule panya aliingia ndani maana mlango ulikuwa wazi.

Kabla hatujamaliza kumshangaa panya buku gafla tukashitushwa na bonge la nyoka jeusiii na lenyewe likazama ndani, kumbe lilikuwa linafukuzia kitoweo chake panya buku.

Na sisi baada ya kuona nyoka tukaruka wote kila mtu na njia yake maana wote tulikuwa watoto, tuakaanza kupiga makelele nyoka nyoka nyoka!!

Jirani alikuwepo mama mmoja wa kisukuma alikuja na akatuambia acheni makelele, alimchungulia dirishani Yule nyoka alimuona kajificha kwenye mtungi alituambia nipeni rungu halafu mkae huku.

Alikaa pembezoni na ule mlango alioingilia nyoka, alianza kuimba nyimbo ya kisukuma kwa sauti nzuri sana huku ameshikilia rungu

Aliimba kama dakika tano hivi kisha akatuambia chungulieni hapo dirishani kipindi naimba akikaribia mlangoni mniambie

Kweli yule mama aliendelea kuimba na kadri anavyoimba nyoka alikuwa anasogea taratibu taratibu.

Kilichonishangaza kingine ni pale mama alipokuwa anaacha kuimba na nyoka nae anasimama mpaka yule mama alipoendelea kuimba nyoka nae aliendelea na Safari mpaka alipokuwa amekaa yule mama.

Na ndipo ukawa mwisho wa maisha yake yule nyoka baada ya kukutana na rungu zito alipomkaribia yule mama wa kisukuma.

Nitaendelea kushea kumbukumbu zingine na kama unakumbukumbu za kushea ruksa kushea ili tusome maajabu ya dunia.
Siku moja kuna watu wa Tanesco walikuwa wanapunguza miti iliyo karibu na nyaya zao za umeme walipofika kwenye nyumba moja wakati wanataka kuanza akatoka mama mmoja kwenye nyumba hiyo akawbia mbona mnakata miti yangu bila ridhaa yangu naomba muache wakawa wameacha wakati wanjishauri akaja mama mmoja nadhani ni mkubwa wao akawafokea mbona wamesimama tu wakasema wamekatazwa na mwenye nyumba wasikate akawatukana pale kisha akawaamrisha waikate wakawa wamefanikiwa kuikata wakapanda gari kuendelea na safari hatua chache tu gari ikapata ajari ikapinduka mara kadhaa akafa yule mama hapo hapo wengine walitoka wazima bila hata mchubuko.
Another:
Kuna siku moja nimejilaza gheto kwa rafiki yangu kwenye coach nikiwa bado mwanafunzi kwao na Huyo rafiki yangu kulikuwa na shule ya msingi private tulitumia madarasa yale kujisomea na kukutana wanafunzi wa shule mbali mbali za day advance hapo town,rafiki yetu alikuwa anaishi na mama yake, sikuwa nakawaida ya kulala chali huwa nalala ubavu au kifudifudi siku hiyo nimelala chalk kwenye lile coach nikaota yule mama was rafiki yetu ameniletea papai nikaanza kula knilipo kula mpaka nusu ndio nikagundua sio papai ni kitu kingine kabisa kinachifanana na boga japo kama kina uchungu uchungu yule mama akaanza kucheka nikawa kama najilazimisha kutapika nikiwa kwenye ndoto nimeshituka nimekaa pale kwenye kochi najilazimisha kutapika Sikh mbili mbele yule mama akatutengea nyama ya kuku, dagaa na ugali Luna rafiki yetu ambaye huwa ni mrafi hadi kwenye misiba alikuwa ugali na dagaa tu mimi nilikula na kuku pamoja na wajukuu wa yule mama baadae yule rafiki yangu aliniambia kuku yule alitumika kwa mazindiko.
Another:
Niliota Magufuli amekufa wiki kama moja kabla ya kwenda kanisani mara ya mwisho niliposhtuka moyo ukawa unauma kweli sinaga kawaida ya kuota ndoto yenye maana sawa sawa na nilichokiota nikasema haiwezi kuwa kweli hata tetesi za kifo chake zilipoanza niliona tu maneno wakati ule sikumbuki chochote kuhusu ile ndoto nimekuja kukumbuka asubuhi baada ya kile kifo kutangazwa.
 
Ninaposema kuwa nimeshuhudia nakuona kwa macho yangu siyo kwamba nimekuja kutunga story ili niwafurahishe hapana

Tena humu Kuna watu wameona mazito kuliko haya ninayoyazungumza kiufupi tu Mimi sinywi pombe wala sivuti bangi hata sigara pia.

Sasa basi Kuna watu walikua wanauliza mwisho wa Yule afsa niliyeua nyoka wake Nini hatima yake.

Kiukweli kwa namna alivyokua anafoka nakuhuzunika nakulalamika sana nililiona hii ni serious ishu,

Niliomba msamaha ukizingatia alikua ni meneja msaidizi niliona kabisa kibarua kitaota nyasi na mwisho wa siku alinielewa akanisihi sana nisipende kuua ua wanyama ambao hawana tatizo na wewe.

Baada ya siku tatu Yule afsa alisafiri kuelekea kijijini kwao aliomba rikizo ya wiki mbili akidai kuwa ana matatizo huko kwao muhimu

Hizo taarifa nilizipata kwa sekretali wake nilipoonda kumuulizia baada yakuona simuoni Tena.

Lakini hakurudi Tena mpaka Mimi nilipomaliza mkataba wangu, na mpaka natoa huu ushuhuda sijui alipo kwa Sasa.

(5) SITOSAHAU NILIPOPIGA PAKA MAWE USIKU BAADA YA SIKU TATU NILIKUTANA NA BABU MMOJA AKANILALAMIKIA KUWA NIMEMVUNJA MIGUU.

Naam, nilikuwa nimepanga chumba morogoro chamwino chini huko panaitwa mtaa wa mgulasi ni uswahilini kwa kweli miaka ya nyuma palikua panatisha sana

Kipindi natafuta chumba dada yangu aliniambia huko siyo pazuri Kuna wahuni wakabaji Mimi niliona Kama ananizingua na kweli kulikua na Mambo ya ajabu ajabu sana kipindi kile.

Nilipata nyumba moja hiyo nyumba ilikua inawapangaji wanne mwenyenyumba alikuwa haishi pale.

Nilikaa wiki moja tu, lakini nilikua nakeleka sana na kelele za mapaka yaliyokua yanalia Kama watoto wadogo hasa inapofika mishale ya saa sita usiku, watalia mpaka saa tisa au kumi hivi.

Aisee asikuambie mtu wale paka walikua Kama siyo chini ya sita, wakianza kulia wanalia sauti za binadamu haswa watoto wadogo wanalia kwa kupokezana.

Nilichoshwa na hiyo hali niliwauliza wapangaji wenzangu walinijibu kuwa wao wamezoea kitendo Cha hao paka kuja kulia usiku kucha kwenye ule uwanja wa ile nyumba.

Siku moja niliamua kudeal nao wale paka, niliandaa mawe makubwa yakutosha nikayaweka geto, sikuhiyo sikutaka kufunga mlango niliuegesha tu sikufunga nakomeo niliendelea kusubiri mida yao ili nideal nao.

Kweli ilipofika mida yao walifika wakaanza kulia, nikasema yes muda ndiyo huu, niliwachungulia pale mlangoni nikawapimia nipige wapi.

Kweli nilifungua mlango gafla nikarusha mawe mfululizo, mawe mawili yalienda bure ila Kuna mmoja lilimpiga mpaka likambadili direction kipindi anakimbia na alilia mlio wa kuonyesha kapigwa.

Nilirudi kulala lakini sikusikia Tena makelele siku hiyo, kesho yake wapangaji wakawa wananisifia kwa kuwapiga wale paka.

Baada ya siku tatu kupita, asubuhi nilikua nawahi mishmishe, nilisalimiana na baby mmoja kipofu aliyekuwa anaishi nyumba ya nne kutoka niliyokuwa nimepanga.

Yule babu nikipofu huwa anashinda nyumbani tu na ni nadra sana kumuona maana Mara nyingi hushinda ndani.

Nilipomsalimia akaniita nakuniambia "kijana ile siku ulivyorusha mawe uliniumiza mguu wangu"

Kiukweli nilishikwa na butwaa, Yule babu hakuendelea Tena kuzungumza na wala hakusubiri nimjibu alinibia tu "kijana wewe nenda kwenye mihangaiko yako"

Niliondoka pale nikiwa Sina Imani kabisa nakuona Kama Yule babu Kuna kibaya atakuja kunifanyia.

Zilipita siku Kama tatu hivi nilimuona mwenyenyumba pamoja na balozi au mjumbe wa nyumba kumi jioni walikuja wakaniambia nihame na mwenyenyumba alinirudishia pesa yangu wakanipa siku mbili za kutafuta chumba.

Nilipouliza kwa nini mnanihamisha, mwenyenyumba alidai kuwa anataka kuishi yeye na hiyo ni dharura sitakiwi kukaidi amri.

Niliona isiwe kesi niliamua kuhama lakini mpaka nahama Yale manyau yalikua hayalii kabisa sijui kilichojiri baada yakuhama maana sikutaka Tena kuishi chamwino nilihamia kihonda.
Nilipokuwa mtoto nilikuwa najiuliza vipofu huota ndoto?

Na kama wanaota ndoto huona nini wakati hawana macho?

Nilipokuwa mtu mzima nilipata jibu kuwa,

Mtu ni ROHO, anayo NAFSI na anaishi ndani ya MWILI.

Mtu anayeishi ndani ya MWILI ana viungo vyote kamili,

Upofu, ulemavu nk ni mapungufu ya nje,

Waeza muona mtu mchana ni mlemavu anajivuta chini, usiku anaparamia mabati ya watu usiamini.

Anyway.

Yule mtu aliyekujia akilalamika umemuulia nyoka yake ambaye Yeye aliita ni NAFSI yake,

Hakuwa mtu kamili,

Alikuwa SPY wa Giza, ajikuja kiwandani kutimiza mission alotumwa na wakuu wake wa Giza.

Alikuzuga kuwa anaenda kijijini wakati ndo alikuwa anarudi kwao kuzimu, nyoka alikuwa ndo mtu halisi, while yule mtu alikuwa kivuli Cha NYOKA.

Kuna watu wengi tunaishi nao, tunafanya KAZI nao, wengine tunasafiri nao, Si watu,

Ni nusu mtu, nusu Pepo.

Mungu Ameweka Malaika zake kutulinda bt ni wengi mno ktk JAMII.

Amen
 
(7) SITOSAHAU TULIVYOKIMBIZWA KWA PANGA NA MZEE MMOJA WA MAKAMO BAADA YAKUCHUKUA PESA ZAKE ZA CHUMA ULETE.

hizi siyo stori za kutunga nahadithia vitu halisi nilivyoviona kwa macho nakuvishuhudia na wala siyo stori zakusadikika.

hii ilitokea dar es salaam sehemu moja panaitwa kitunda kipindi hicho miaka ya 2004 hivi pale kitunda ilikua bado kabisa ni bushi kiufupi palikua hapajachangamka

Mimi na mwenzangu tulikua tunatabia ya kwenda kuwinda mabondeni ukivuka barabara ya ng'ombe unapita kwenye bonde moja walikua wanafuga sana nguruwe panaitwa kwa mama Tyson.

Tulikua tunavuka pale Kisha tunaelekea kwenye poli la jeshi kwa wanaolijua hili eneo nafikiri watakumbuka namna gani pale mwelekeo wa jeshini kulivyokua na kichaka.

Tulikua na akili za kitoto, tulikua tunakwenda kuwinda ndege, nakuchuma matunda fulaani yanaitwa mabungo.

Sasa bwana katika pita pita vichakani niliona chungu kikiwa kimefunikwa na kitambaa cheupe na chini pia kimewekewa kitambaa cheupe lakin kwenye shingo ya chungu kimezungushiwa hirizi zilizovikwa Kama cheni.

Nilimuita mwenzangu, alikuja akaona Kisha tukatoka kwa kukukimbia kwenye lile eneo mwenzangu alikua ni muoga alisema ule ni uchawi.

Tulifika mbele tulikaa Kisha tukatafakari mule ndani Kuna Nini???
Kila mmoja wetu alitaka kujua kwenye lile chungu Kuna kitu gani??

Basi tukashauriana tutafute mti mkubwa twende kwenye eneo la tukio tukifika pale tuusukume ule mtungi uliokuwa umefichwa kichakani ili tujue ni Nini kipo ndani yake.

Tulipofika eneo la tukio, mwenzangu alikataa kushika ule mti ilinibidi nishike Mimi nakuanza kusukuma ule mtungi kwa kutumia mti mrefu.

Mtungi ulikua mzito kuanguka na kila nilipokua nautikisa nasikia sauti ya mlio Kama vyuma vinagongana ndani yake, basi nilifanikiwa kuuangusha chini, na tukaona chenchi nyingi sana zinamwagika mia mia hamsini hamsini na shilingi kumi pamoja na ishirini ishirini.

Tulitazamana na rafiki yangu kwanza, Kisha tukazifuata zile hela maana yalikua ni machenchi mengi, nilivua fulana langu tukaziweka zile chenchi Kisha kile chungu tukakiweka Kama kilivyokua tukaondoka eneo lile.

Zile pesa tulikwenda kuzificha sehemu kwa kuhofia wazazi wakituona na hizo pesa lazima wangehoji tu, tulitafuta sehemu tukazificha tukawa tunatumia kidogo kidogo ikawa ni Siri ya watu wawili

Ile pesa tuliitumia ikaisha baada ya wiki Kama mbili, kwa sababu tunajua ni wapi tulizipata tuliamua kurudi Tena Safari hii hakuna mwenye uoga.

Na tulipofika eneo la tukio kweli tukakikuta chungu kipo vile vile hatukutaka hata kuchukua mti Kama ulivyokua mwanzo , tulifika tukafungua chungu tukakuta chenchi lakini Safari hii hazikujaa Kama mwanzo tukazibeba tukatokomea kusikojulikana.

Nakumbuka hata shuguli zetu zakuwinda katika lile poli laki jeshi zilisimama baada yakua tunakuta pesa za bure tunabeba Kama zetu wala mwenyew hafahamiki ni Nani.

Sasa baada yakukaa wiki moja rafiki yangu akanipitia tena, twende tukachukue pesa kwenye chungu,

Tulipofika katika lile eneo Kama kawaida yetu akili zinawaza pesa tu na hakuna kingine.
Tukiwa tunajiandaa kufungua chungu Mara gafla tulishitushwa na sauti ya kiume iliyokua inatokea kichakani Tena akija huku anakimbia kuja eneo letu ambapo chungu kipo.

Alisema "nilikua nawasubiri kwa muda mrefu kumbe ni nyie wapumbavu'

Alikua ameshika panga ni mzee wa makamo alikua amevaa kibarakashea aise tulipo muona anakuja kasi huku kashika panga na sisi tulitimua mbio kila mtu na njia yake hata sikukumbuka rafiki yangu alipitia wapi maana ilikua ni kila mtu akijaribu kuokoa nafsi.

Jiioni nilikwenda kumtembelea rafiki yangu nikamkuta kwao na yeye alikua ana wasiwasi labda mim nilidhurika, basi hatukwenda Tena tangia hapo ila nilisimulia juu ya zile pesa watu wakubwa walisema ni chuma ulete ya huyo mzee zile pesa zilikua zinajaa pale ni Kama ndiyo benki yake ile.

KITU KAMA HIKI NILIKUTANA NACHO MOROGORO KWENYE MASHAMBA YA SUA.

nilikua natoka chamwino kuelekea kisanga kwa miguu wakati ule nilikua naishi chamwino, nakumbuka nilikua Sina hata mia mbovu mfukoni yakupanda daladala na ndiyo maana niliamua kupita shortcut kupitia mashamba ya SUA.

Katika kupita pita kwangu humo mashambani nilipita kwenye mti mkubwa ule mti ulikua upo katikati lile eneo lilikuwa halijalimwa kwa muda mrefu.

Nilipita kwenye ule mti nilishangaa kuona sinia kubwa la shaba limewekewa kitambaa cheupe na chini Kuna kitambaa chekundu.

Halafu juu ya kitambaa cheupe Kuna shilingi mia tano tano nyingi sana za Silva, ni nyingi kweli kweli na pembeni kulikua na kuku mweupe Yule kuku hakjafungwa lakini yupo kama mgonjwa mwenye mdondo na kulikua na udi umewashwa unaelekea mwisho mwisho.

Kiukweli nilipiga hesabu Sina hela mfukoni na hela naziona Kama hivyo nyingi kweli kweli,

Nilifika mpaka kwenye sinia nikazichota kwa mikono miwili Kisha niliendelea na Safari yangu nilizifanyia matumizi ya yangu hakuna lililonipata na pia nilikua jasiri maana nilikumbuka tukio la chungu kule poli la jeshi hatukuzurika.
 
Siku moja kuna watu wa Tanesco walikuwa wanapunguza miti iliyo karibu na nyaya zao za umeme walipofika kwenye nyumba moja wakati wanataka kuanza akatoka mama mmoja kwenye nyumba hiyo akawbia mbona mnakata miti yangu bila ridhaa yangu naomba muache wakawa wameacha wakati wanjishauri akaja mama mmoja nadhani ni mkubwa wao akawafokea mbona wamesimama tu wakasema wamekatazwa na mwenye nyumba wasikate akawatukana pale kisha akawaamrisha waikate wakawa wamefanikiwa kuikata wakapanda gari kuendelea na safari hatua chache tu gari ikapata ajari ikapinduka mara kadhaa akafa yule mama hapo hapo wengine walitoka wazima bila hata mchubuko.
Another:
Kuna siku moja nimejilaza gheto kwa rafiki yangu kwenye coach nikiwa bado mwanafunzi kwao na Huyo rafiki yangu kulikuwa na shule ya msingi private tulitumia madarasa yale kujisomea na kukutana wanafunzi wa shule mbali mbali za day advance hapo town,rafiki yetu alikuwa anaishi na mama yake, sikuwa nakawaida ya kulala chali huwa nalala ubavu au kifudifudi siku hiyo nimelala chalk kwenye lile coach nikaota yule mama was rafiki yetu ameniletea papai nikaanza kula knilipo kula mpaka nusu ndio nikagundua sio papai ni kitu kingine kabisa kinachifanana na boga japo kama kina uchungu uchungu yule mama akaanza kucheka nikawa kama najilazimisha kutapika nikiwa kwenye ndoto nimeshituka nimekaa pale kwenye kochi najilazimisha kutapika Sikh mbili mbele yule mama akatutengea nyama ya kuku, dagaa na ugali Luna rafiki yetu ambaye huwa ni mrafi hadi kwenye misiba alikuwa ugali na dagaa tu mimi nilikula na kuku pamoja na wajukuu wa yule mama baadae yule rafiki yangu aliniambia kuku yule alitumika kwa mazindiko.
Another:
Niliota Magufuli amekufa wiki kama moja kabla ya kwenda kanisani mara ya mwisho niliposhtuka moyo ukawa unauma kweli sinaga kawaida ya kuota ndoto yenye maana sawa sawa na nilichokiota nikasema haiwezi kuwa kweli hata tetesi za kifo chake zilipoanza niliona tu maneno wakati ule sikumbuki chochote kuhusu ile ndoto nimekuja kukumbuka asubuhi baada ya kile kifo kutangazwa.
Dah mzee haya mambo yapo katika hii dunia
 
Back
Top Bottom