Haya ndiyo mambo ya ajabu niliyowahi kuona na kushuhudia kwa macho yangu, sitoyasahau katika maisha yangu

Haya ndiyo mambo ya ajabu niliyowahi kuona na kushuhudia kwa macho yangu, sitoyasahau katika maisha yangu

Huko alikutwa na Malaria ya kichwa akapewa dripu za kutosha akaandikiwa na dawa

Ambapo mpaka saizi bado yupo kwenye dose ya hizo dawa
malaria ikipanda kichwani basi unakuwa kichaa kabisa. Na kichaa kinakuwa permanent pale mgonjwa atakapochelewa matibabu
 
Kuna magonjwa yanawaattack watu very rarely sasa kutokujua huko(kukosa elimu) kunapelekea watu kudhani ni ushirikina kumbe sio.Miaka minne nyuma nilianza kusikia sauti za ajabu masikioni pia mlio wa kengele yani imagine kengele inalia masikioni mwako wawezo kuhisi umerogwa kumbe ni ugonjwa unaitwa tinnitus sasa magonjwa kama haya ni very rare kuyasikia lakini yapo.
Hakuna mtu anayepinga sayansi lakini Kuna muda sayansi inagonga mwamba mzee.

Mfano mzuri Kuna mzee mmoja wa tiba za asili yeye anatibu watu wenye matatizo ya mifupa bodaboda wamejaa sana kwake.

Kuna mtu alihangaika sana hospitali lakini alikwenda kuponea pale Sasa hapo tunasema sayansi imegonga mwamba

Hakuna mtu anayepinga sayansi.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Sister yangu alishawahi kutana na hili tatizo (anaona vitu ambavyo havipo)

Mnaweza mkawa naye pamoja afu ghafla akaanza kupiga kelele kuwa "niache, niache" huku akijificha kama ishara ya mtu anayetaka kumchukua bila ridhaa yake.

Anakuwa serious analia na kulia na sometimes katika purukushani unakuta mpaka anaji jeruhi, anasema watu anaowaona wanatisha wana meno marefu na nywele nyingi wanamuambia twende nyumbani

Mara adai kutokewa na watu waliokufa wakisema "twende ambapo tupo sisi"

Makuzi yetu ya kiafrika na uduni wa elimu ulifanya watu wakubali majibu yasio sahihi kuwa ni ushirikina kwa kuyaamini macho na ubongo wetu.

Lakini tulipoenda kwa Doctor ambaye ni mbobezi kwenye maswala ya mental health alitusaidia na sasa hilo tatizo halipo tena

Sayansi inasema muda wote haupaswi kuyaamini macho, masikio na ubongo wako

They can play fool sometimes
Visual and auditory hallucinations ukiongeza na delusion ni schizophrenia hiyo
 
Dunia Ina Mambo mengi sana na ni rahisi sana kupinga au kubisha Kama hayo Mambo ya ajabu hujayashuhudia na pia ni Bora uwe unasimuliwa tu na usije kukutana nayo maana unaweza ukadhurika ama ukawa hai.

Naam leo nimepata muda nikaona ni Bora nishee haya machache niliyokutana nayo katika huu ulimwengu,


(1) sitosahau nilipokutana na mtu mrefu asiyekuwa na mwisho inasadikika ni jini

Yapata mishale ya saa saba usiku, niliwasha pikipiki yangu kutoka Kambarage kuelekea Matanda kwa wale wenyeji wa Shinyanga wanayaelewa haya maeneo.

Nilikuwa nafanya kazi ya ulinzi kitengo Cha supervising na kupiga patrol kuwaausha walinzi usiku kwa hiyo mishale ya saa saba , saa sita ,saa nane mpaka saa tisa ndyo ilikuWa mida yangu kwenda kuwapatrol walinzi ili kazi za watu ziwe salama.

Nakumbuka nilitoka nyumbani vizuri pale Kambarage nikafika mitaa ya ofisi ya mkuu wa wilaya ili nishike barabara ya kuingia Tanesco Matanda.

Nikawa nakaribia kupita geti la ofisi ya mkuu wa wilaya, Mara gafla nikaona mtu amevaa nguo nyekundu akiwa amesimama katikati ya barabara ninapoelekea Mimi,

Kiukweli haikunishitua nikaendelea kusogea maana ile njia huwa napita sana, nilishawahi kukuta watu wanaogeshana usiku wa manane, Mara watu wanavunja Nazi kwa hiyo nilijua tu huyo aliyevaa nguo nyekundu ni mtu Kama wale ninaowaonaga.

Sasa nilipokuwa naendelea kumkaribia cha ajabu alikuwa anazidi kuwa mrefu na njiani hataki kutoka ilinibidi nipunguze spidi huku nikishusha gia za pikipiki mpaka namba moja hapo nilikuwa nishamkaribia kwa ukaribu na alikuwa ni mrefu kichwa hakionekani hana mwisho.

Sikuamini nilichokiona na ndiyo ilikuwa ni Mara yangu ya kwanza kukutana na kitu kama kile, niliamua kuzima taa na kuziwasha, kitendo cha kuzima nakuwasha tu, lile dubwana lilipotea kama upepo sikuliona tena akili yangu ilibadilika nilikimbiza pikipiki kama mwendawazimu kurudi nyumbani maana sikuendelea na Safari yangu, siku iliyofuata niliumwa sana nililala ndani bila kutoka kwa muda wa siku tano.


(2) NILIUA NYOKA WA MTU, MWENYE NYOKA ALINIFUATA AKAANZA KUNIDAI NYOKA WAKE.

Miaka ya nyuma nilikuwa nafanya kazi katika kiwanda kimoja cha chai huko Iringa kwa majina sitotaja, siku hiyo ilikuwa ni siku ya usafi tulikuwa tunasafisha maeneo ya kiwanda maana siku ya usafi wa mitambo na mazingira kwa ujumla uzalishaji husimama.

Mimi nilikuwa nafyeka majani, lile eneo tulipangiwa wawili lakini mwenzangu kwa muda ule alienda kunywa chai atakaporudi na mimi niende tulipeana zamu.

Kipindi nafyeka gafla nikaona nyoka mwezi anakuja upande wangu, ni mrefu mwembamba, Mimi binafsi nyoka nawajua ni moja Kati ya nyoka wenye sumu kali.

Sikutaka kushangaa ikanibidi nimuue, nilimkata na kwanja tenganisha kichwa na kiwiliwili akafa.

Mara punde alikuja mmoja wa maafisa wakubwa pale kiwandani akihema kama mtu aliye na presha, alinifokea na machozi yakimtoka alisema "kwanini umeua nafsi yangu"

"Huyu ndiyo ananifanya niishi hapa"

Nilishikwa na butwaa sana, maana yule alikuwa ni boss mkubwa nilibaki najiuliza huyu boss na manyoka wapi na wapi.

Na hakuishia hapo aliendelea kunitishia amani akidai nyoka wake arudi na ule ndiyo ilikuwa ni ulinzi wake.

Mimi nilipoona hivyo nikajua kabisa hii ni serious sana nilimuomba msamaha sana nikamwambia sikujua.

Hakika like kitendo cha mtu kusema nimeua nafsi yake kilinistaajabisha sana.


(3) SITOSAHAU NILIPOMKUTA MMASAI AKIONGEA NA CHUNGU NA CHUNGU KILIMJIBU.

Hii nimeshuhudia kwa macho yangu mpaka niliona Kama ninaota, nakumbuka tulikuwa kwenye mitihani ya darasa la saba tena ulikuwa ni muda wa mapumnziko.

Nilikwenda kutafuta darasa moja ambalo lilikuwa lipo mbali na yale tuliyokuwa tunafanyia mtihani nikiwa na lengo la kwenda kupumnzika nitulize akili yangu kidogo.

Nilipokuwa nakaribia kwenye hilo darasa nilianza kusikia sauti ndipo nilipoamua kuchungulia, nikamuona mwanafunzi mwenzangu mmasai, tuliyekuwa nae darasa moja na yeye alikuwa nafanya mtihani wakuhitimu darasa la saba.

Kilichonishangaza alikuwa ameweka chungu pembezoni kabisa ya darasa juu ya dawati kile chungu kilikuwa kinawaka Moto.

Sasa kipindi naendelea kuchungulia alikuwa anaongea peke yake kwa lugha ya kimasai huku akiwa amekunja mikono yake na amenyenyekea kweli mbele ya hicho chungu,

Alipomaliza kuzungumza kile chungu kilimjibu kwa sauti ya kike, kilizungumza kwa lugha ya kimasai pia, niliogopa sana kile kitendo niliinama chini nikasota kwa hatua kama tano hivi nikakimbia sana kuondoka kwenye hilo eneo.

Muda wa mtihani ulipofika masai nae akaja kupiga pepa, tulivyomaliza mitihani sikumuona yule jamaa mpaka sasa ila siku hiyo sikuwa na amani na nilimuogopa sana.


(4)NILISHUHUDIA MAMA WA KISUKUMA AKIIMBA NYIMBO NZURI NA KUMTOA NYOKA TOKA MAFICHONI.

Ukistaajabu ya Musa basi utayaona ya Firauni na wanasema tembea uone mengi na ujifunze.

Nikiwa bwana mdogo nilikwenda kumtembelea shangazi Shinyanga Kijijini baada yakufunga shule.

Siku hiyo nakumbuka ilikuwa ni mchana mishale ya saa 8 mchana tulikuwa tumekaa karibu na mlango tunakula chakula cha mchana.

Mara gafla alipita panya buku kwa spidi ya ajabu sana bila kujali chochote yule panya aliingia ndani maana mlango ulikuwa wazi.

Kabla hatujamaliza kumshangaa panya buku gafla tukashitushwa na bonge la nyoka jeusiii na lenyewe likazama ndani, kumbe lilikuwa linafukuzia kitoweo chake panya buku.

Na sisi baada ya kuona nyoka tukaruka wote kila mtu na njia yake maana wote tulikuwa watoto, tuakaanza kupiga makelele nyoka nyoka nyoka!!

Jirani alikuwepo mama mmoja wa kisukuma alikuja na akatuambia acheni makelele, alimchungulia dirishani Yule nyoka alimuona kajificha kwenye mtungi alituambia nipeni rungu halafu mkae huku.

Alikaa pembezoni na ule mlango alioingilia nyoka, alianza kuimba nyimbo ya kisukuma kwa sauti nzuri sana huku ameshikilia rungu

Aliimba kama dakika tano hivi kisha akatuambia chungulieni hapo dirishani kipindi naimba akikaribia mlangoni mniambie

Kweli yule mama aliendelea kuimba na kadri anavyoimba nyoka alikuwa anasogea taratibu taratibu.

Kilichonishangaza kingine ni pale mama alipokuwa anaacha kuimba na nyoka nae anasimama mpaka yule mama alipoendelea kuimba nyoka nae aliendelea na Safari mpaka alipokuwa amekaa yule mama.

Na ndipo ukawa mwisho wa maisha yake yule nyoka baada ya kukutana na rungu zito alipomkaribia yule mama wa kisukuma.

Nitaendelea kushea kumbukumbu zingine na kama unakumbukumbu za kushea ruksa kushea ili tusome maajabu ya dunia.
Unachotafuta hapa ni kunadi uganga watu wakufate inbox kama dalali wa waganga
 
Mimi natoa Mikasa ambayo nimekutana nayo na nimeshuhudia kwa macho yangu Kama Kuna mtu anaona kuwa hizi ni stori za kutunga basi shauri yake.

Lakini haya ninayoyazungumza Kuna lakujifunza ndani yake hii dunia ni pana sana nitaendelea kutoa au kushea nilivyoviona katika huu ulimwengu .

Kama Kuna mtu pia yalishawahi kumtokea makubwa zaidi ya haya pia asisite kushea ili tuendeleee kupanua ubongo.

(9) SITOSAHAU NILIVYOKUNJANA MASHATI NA WAOSHA MAITI NDANI YA CHUMBA CHA MAITI.

Hii ilitokea mkoa wa pwani, nilipo mrudisha babu yangu mzaa mama nyumbani kutoka hospital aliuugua kwa muda mrefu tulimuuguza sana mwisho wa siku alikata roho.

Pale mtoto wa kiume nilikua nipo Mimi ndiyo mjukuu mkubwa wengine walikua bado hawajafika kutoka mjini, Sasa ilibidi tuanze kushughulika na mazishi.

Msiba ni wakiislam, maana babu kwenye uhai wake alikua ni muislam nakumbuka alifariki alfajir mpaka saa kumi na mbili hivi saa moja moja nilikwenda kutoa taarifa msikitini.

Naam mchakato ulianza walikuja wazee wa makamo watatu wao kazi yao nikuosha maiti nilielewana nao nikawalipa waanze kazi yao yakuosha pamoja na maandalizi ya ushonaji wa sanda.

Utaratibu uliendelea, maiti ya mzee iliwekwa juu ya kitanda Cha kamba, Hilo zoezi lilikua linafanyika ndani ila chini yakitanda palichimbwa shimo ili Yale maji ya maiti au fuo yamwagigikie chini.

Zoezi lilifanyika Kama utaratibu ulivyo na Mimi sikua mbali nilikua karibu sana na waosha maiti kuhakikisha zoezi linakwenda sawiya.

Sasa basi zoezi lilifanyika Kama lilivyopangwa cha ajabu walipokua wanamuosha mzee pale chini ya shimo walitegesha chombo Kama kibeseni hivi ili kukinga maji ya maiti.

Hilo nililiona lakini sikutaka kuuliza maana wao ndiyo wataalam, ikanibidi niwe mpole kwenye sehemu Kama huwezi kuleta ujuaji na ukiangalia ni wazee wa makamo.

Baada yakukamilisha zoezi lao, waliianda maiti vizuri wakafukia pale chini ya kitanda lakini maji waliyokua wanayakinga waliyaweka kwenye kidumu Cha lita na mengine waliyafukia vizuri kabisa.

Mimi muda huo nilikua nawaangalia nakuwatafakari hawa maji wanataka kupeleka wapi??
Nilijiuliza sana lakini nilijisemea moyoni itafahamika tu.

Walipomaliza shuguli zao, si ndiyo walitaka kutoka nje na Yale maji.
Mimi niliwazuia mlangoni, niliwauliza mnapeleka wapi hayo maji??

Mmoja akajibu tunakwenda kuyaombea, niliwaambia hakitoki kitu hapa toka lini maji ya maiti yakaombewa??

Mzee mwingine alidakia nakusema kijana usijitafutie matatizo tunaomba utupishe tupite!

Kabla sijajibu mzee mmoja alinikunja shati, na Mimi niliona liawalo na liwe tukaanza kukabana ndani ya chumba Cha maiti na nje Kuna watu bahati nzuri kile chumba tulichokuwemo tulikua tumejifungia ndani.

Baada ya hizo purukushani ndiyo mzee mmoja akawaambia wenzake jamani hili la leo lishakua gumu tumuachie hayo maji.

Waliyaacha huku wananikata jicho na waliniambia siku nyingine ukipatwa na matatizo hapa kwenye familia yenu hatuji hata kwa dawa.

Na Mimi niliwaambia sawa.

........................................................................

KWA NINI NILIZUIA YALE MAJI YA MAITI??

nilijua kabisa hawa Kama siyo waganga basi watakua washirikina na Kama siyo washirikina basi watakua wanayataka Yale maji wakayauze.

Nirudi nyuma kidogo Kuna wakati fulani nilikua morogoro masikani tumekaa na washikaji tukipiga stori za hapa na pale.

Alitokea dalali mmoja alituambia kuwa Kuna dili la pesa na dili Hilo Kuna mganga anataka maji ya maiti akafanye Mambo yake lakini dalali hakusema kuwa ni Mambo gani .

Tulicheka nakumpuuza mana hiyo dili ilikuwa ya Moto kwa vijana Kama sisi pale tusingethubutu kabisa kuanza kutafuta maji ya maiti.

Kutoka na mfano Kama huo nilijifunza kuwa maji ya maiti ni dili sana yanatafutwa na waganga kila kukicha au washirikina na kwenda kufanyia Mambo yao huko wanayoyajua.

Ndiyo maana nilikua mkalisana nakufikia hatua kukunjana mashati na wale wazee ndani ya chumba Cha maiti,

Hapa Kuna funzo ni muhimu sana Kama umepatwa na msiba na mtu wako wakaribu basi kuwa karibu sana maana Kuna Mambo ya ajabu hutokea pale msibani anaweza akalifanya hata ndugu yako wakaribu.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom