Serikali ina haha kujaribu kuzima mgomo wa Yanga kucheza mechi ya derby iwapo itapangwa tena.
Ukiangalia chanzo ni serikali kujaribu kuisaidia Yanga ishinde ubingwa kirahisi na kwa mbinu nje ya uwanja.
Kitendo cha meneja wa uwanja kugoma kuwafungulia Simba kufanya mazoezi na kusafisha uwanja,akisaidiwa na makomandoo wa yanga,waliolindwa na polisi,ni dhahiri kabisa serikali ilikuwa inajaribu kuisaidia yanga ishinde mechi kirahisi.
Kama vile haitoshi,meneja wa uwanja kwa kuungana na yanga,alipinga maamuzi ya bodi ya ligi ya kuahirisha mechi,akawafungulia mashabiki mageti ya uwanja waingie,kisha akaruhusu timu ya yanga iingie ingawa jana yake alidai hana taarifa kama kuna mechi ya derby( hii ni maajab!)
Serikali hii hii,kule Mwanza,ilituma polisi kuwakamata viongozi wa Simba wakati wakifanya mazoezi kwa sababu za kitoto kabisa.
Yote hii ni kujaribu kuwaharibu kisaikolojia wachezaji wa Simba, ili Simba ipoteze kirahisi Mwanza na yanga waongoze kwa amani.
Timu hii pendwa ya serikali ,ina mashabiki wanaoilaumu Simba kuhusu Fei Toto.
Hata hivyo kwa kuwa hawana akili,wamesahau kuwa mh Rais ndiye aliyewaomba wasishindane na kijana mdogo snayejitafuta bado kwenye soka kama Faisal.Walimsikia mama na wakaruhusu Fei aende Azam.
Leo pamoja na serikali ,TFF na bodi ya ligi kuwabeba hawa jamaa,wamewagomea na wanawatoa kijasho! Na mimi nasema yanga waendelee kukaza hapo hapo