Petro Masunga
Member
- May 5, 2023
- 7
- 7
Naitazamia nchi ya watu wazima, huku nikiwa na kiasi cha tashwishi. na kujiuliza maswali, kama nchi ya watu wazima tunataka nini? hivi mwelekeo wetu ni upi? kiongozi ni yule, na mwongozwa ni huyu. najaribu kuwaweka kwenye kundi moja, lakini hawawekeki. hivyo niliona kila mmoja akiendelea na njia yake, huku kila mmoja akimtupia mwenziye lawama kwamba (hasikii).
Tuko sawa pamoja, kila mmoja katika njia yake yuko sawa. lakini tumeteleza kidogo ni lazima tujirekebishe, wote kwa pamoja, ili kati ya wawili aweze kuwa mmoja. viongozi wanafanya vitu vya ajabu ajabu, kana kwamba tuliwaazima kutoka ng'ambo, kana kwamba siyo viongozi wa nchi ya watu wazima, wanaingia kwenye mikataba isiyo rafiki kwa nchi, kana kwamba wao siyo raia wa nchi hii, yaani hawana kiasi kabisa. je; sifa ya kiongozi wa nchi ya watu wazima iko wapi kwao? kiukweli ni lazima tubadilike maana kokote kule tuendako duniani, tutabaki raia wa Tanzania, tu. ni lazima muheshimu vyeo mlivyonavyo, muna sistahili kuwa na hivyo vyeo, hivyo msifanye vitu vya ajabu ajabu, kana kwamba hivyo vyeo, mlivipata kwa bahati mbaya.
Vivyo hivyo kwa sisi waongozwa, tunao jiita wananchi, tumeteleza kidogo, lazima tujirekebishe. hatuna sifa za kuwa katika nchi ya watu wazima. mikono yetu ya kuume tumeshikilia, kila aina ya vitu vya ajabu ajabu, huku vitu muhimu na vya msingi, tukiviacha kushoto. hivi nani alikuambia ukienda barabarani kuandamana kwa kutambua nini unacho kiandamania, hautaendelea kuwa mtanzania? ni kwa sababu tuwatumwa wa mihemko na ushabiki usio kuwa na mipaka.
Ndiyo maana hatuna mipango na nchi yetu. Huyu yuko na kazi ya kuajiriwa, ukimuuliza mpango kuhusu kazi ile, atakuambia hana mpango wowote maana shida yake ilikuwa ni kupata kazi, ili apate fedha, ukimuuliza kuhusu atadumu kwa muda gani, atakuambia, kiukweli hajui, maana kazi siyo yake,(ameajiriwa), kwa kutambua kwamba kazi siyo yake, bado hana mpango wa kwamba, niajiriwe kwa kwa miaka mingapi ili na mimi nijiajiri, hana mpango huo hata kidogo, maana baada ya kufutwa kazi pale, ataenda kule na nyaraka zake, kwa ajili ya ile kazi tu, je; hatupo na hawa watu kati yetu?
Maana baada ya umri kumkataa kazini, anakuwa omba omba, ni kwa sababu hakuwa na malengo ya maisha na hiyo kazi, hana sifa ya kuwa raia wa nchi ya watu wazima, shida ya namna hiyo hiyo lakini kinyume chake, kwa ambaye hana kazi, anaweza hakawa anapata vibarua, badala ya kuwa na mpango hai kuhusu fedha anayo pata, yeye kama kula ataila sana hadi iishe, kama ni kujiremba atajiremba sana ili tu iishe halafu kesho tena aende kutafuta vibarua, je; sifa ya raia wa nchi ya watu wazima iko wapi kwake?
Hivyo hebu tuwe na kiasi jamani, na tuzingatie majukumu yetu kama wahandisi wa nchi. Pia natazamia mfumo mzima wa uendeshaji nchi ubadilishwe pamoja na idara zake, ili kusiwepo tofauti kati ya serikali na mwananchi. hivyo kwa sababu nchi ya watu wazima ni nchi ya watu wenye ukwasi na shauku kubwa ya maendeleo. hivyo itafaa sana huo mchakato wa katiba mpya uharakishwe, kwa sababu tunataka kwenda mbele kwa vitendo.
Kwa maana hiyo na katika kutambua uzito wa mchakato huo, mimi ninatoa pendekezo kwamba hiyo katiba iandikwe na iwekwe kwenye app ya umma ambapo hiyo app haitahitaji kuwa na ,mbs, ili kuingia na kuisoma, ili watu waipigie kura. kwa sababu ya wananchi wengi kuwa na simu zenye uwezo wa wavuti hata kama siyo smart phone, ili kuokoa gharama kubwa ya fedha itakayo tumika, nimezingatia hilo, ili kabla ya uchaguzi mkuu ujao. tuwe tayari tushapata katiba mpya. tunapaswa tutazame hatua nyingine mbele, na tuwajibike kama nchi ya watu wazima.
Ahsante.

Upvote
1