Hicho kitu kibaya ni kipi asichosema?! Sana sana kuna wakati alipoulizwa kuhusu bifu lao alitaja sababu za kijinga kabisa... suala la kufutiana sauti kwenye wimbo!!
Hakuna lolote zaidi ya mambo ya kipumbavu! Si ajabu hapo kaenda kwa mganda wa kienyeji kaambiwa nyota yako imechukuliwa na mpinzani wako! Sasa kama sio upumbavu tuite nini!
Muziki duniani kote umebadilika! Muziki duniani kote siku hizi watu wanatoa ngoma back to back kwa sababu ule upuuzi wa zamani kwamba eti ngoma mzuri inaishi, hivi sasa huo upuuzi hauna nafasi!!
Huo upuuzi hauna nafasi kwa sababu siku hizi media za kusikiliza ngoma zipo nyingi, na matokeo yake, ngoma ikitoka kwa siku unaweza kuisikia hata mara mia na ushee... ukipanda daladala utaisikia, ukipanda UBA utaisikia, kwa Dar kila uchochoro utakaopita, utaisikia kwa njia mbali mbali! Matokeo yake, ngoma hata ikiwa kali vipi, baada ya muda mfupi itachosha tu kutokana na kuisikia mara kwa mara!
Kutokana na hilo, ili watu wasipotee, ndo hapo linapokuja suala la back to back! Kiba na akili zake za kizamani anaamini akitoa ngoma moja, mwaka mzima ita-trend tu! Ikiwa tofauti, ndo pale wajinga hukimbilia kwa waganga wa kienyeji na kuambiwa wamerogwa kumbe mchawi wao ni ujinga wao wenyewe!!!