Haya ni baadhi ya mambo mengine yaliyomo kwenye kitabu cha Erick Kabendera

Haya ni baadhi ya mambo mengine yaliyomo kwenye kitabu cha Erick Kabendera

Endelea kujifariji kuhusu magufuli na uongozi wake! He was our 5th president..No one is going to change that! Huyo kabendera na wew hakuna watu watawakumbuka..!
Kuna watu hapa kwangu hawaendi msalani,shuleni wala kujidai bila mimi.Wataanzaje kumkumbuka asiye na direct impacts kwao?Fikiria upya.
 
Mwisho wa siku, mmeivuruga nchi, mmeuza maliasili za watanganyika na sasa HAMNA mtakachowaambia waumini wa sera za Magu ambao ndio wengi na wasio wanufaika wa MIKOPO ya nchi iendayo chizimkazi kwa gharama za vizazi vyao.

Hakikisheni mnawachanganya kweli kweli ili mfanikiwe hiyo October 2025.

1. Magufuli
2. Lisu vs Mbowe
3. Mapambio
4. Chawa

Ndo sera zenu kuhakikisha MITANO TENA inafanikiwa sio?

Bila hivyo, mtaulizwa, mwamba alifanya, nyie mmeshindwa nini?
Maana ya kuuwa wanafanana. Na wao wanauwa
 
Nilijua mradi wa kumchafua mwamba JPM kupitia serikali hii umekwisha, naona ndo kwanza unakolezwa.

Mambo aliyoyafanya mwamba yanajieleza yenyewe, wadanganyika tunawekwa busy kujadili issue ya Magu huku rasilimali zetu za nchi zikiporwa, ucahguzi wa serikali za mitaa umechezewa, bandari zetu zimegawiwa kwa wageni, wamaasai wa Roliondo wanafurushwa kwenye makazi yao, deni la taifa linapaa kila uchwao, miradi mikubwa ya kimkakati imesimama, watu wanatekwa mchana kweupe na kwenda kuuawa wengine wakiponea chupuchupu na wengine hawajulikani walioko mpaka leo kina Soka na yule kijana wa Mbeya aliyechoma picha yenye sura ya Samia.

Kama taifa adui yetu siyo mtu aliyelala usingizi wa mauti, kama alifanya ubaya wakati wake watajuana na Mungu wake huko aliko nadhani ni wakati wa kuwaambia watawala ukweli tusiwe kept busy na vitu vya kipumbavu ambavyo havina maslahi kwa ustawi wa taifa. Usalama wa taifa kuweni macho na maslahi mapana ya taifa acheni kutetea na kulinda kikundi kidogo cha watu huku taifa likibaki mifupa mitupu, nyinyi ndo mmeapa kulinda maslahi ya taifa hili achananeni na mambo ya vyama vya siasa. Taifa linawategemea sana sema hamjui tu au kama mnajua mmeamua kujizima data.
 
Back
Top Bottom