Ilikua safari nzuri na ya kuvutia sana unforgettable moment.
Nilipanda kama mtalii tulipandika njia ya the Northern circuit 10 day tunashukia mweka gate.
Labda nikupe hints kidogo ya zone za mountain kilimanjaro na actually ukipanda mlima kilimanjaro up to Uhuru peak ni sawa na mtu alietembelea mabara matano tofauti kwa siku chache..
Yeah
Hapa kuna kanda hizo 5 ambazo hupitia unapoanza chini hadi kileleni:
1.Ukanda wa Kilimo/Tambarare (Cultivation Zone): Hii ni sehemu ya chini yenye mashamba ya migomba na kahawa, kijani kibichi, na joto la kawaida.
2.Ukanda wa Msitu wa Mvua (Rainforest Zone): Msitu mnene wenye miti mirefu, unyevunyevu, na wanyama mbalimbali.
3.Ukanda wa Mbuga na Vichaka (Heather and Moorland Zone): Joto hupungua, miti hupotea na kubaki vichaka maalum na maua ya mlima.
4.Ukanda wa Jangwa la Mlima (Alpine Desert Zone): Sehemu kame yenye mawe na mchanga, haina mimea mingi, joto la mchana ni kali na usiku hupungua sana.
5..Ukanda wa Theluji/Arctic (Arctic Summit Zone): Kilele cha juu kabisa (Uhuru Peak) kikiwa na theluji na barafu, hali ya hewa ni ya baridi kali sana.