Haya ni baadhi ya matukio muhimu baada ya kupanda mount Kilimanjaro "way back" hakika ilikua safari nzuri na kuvutia sana

Niliona clip sasa sehemu za miamba sjui mawe mvua inanyesha au imekata muda so mrefu na wanarndelea na hiking so sikuelewa na wengine wanapita sehemu ya kukumbatia mwamba hivi ko hali kumbe iko hivyo
Ya, mvua haizuii hiking unless kuna extremely poor visibility, yaani mbele huoni hata mita 1 na chini miguu huioni unakanyaga wapi
Mwamba hiyo route ya Machame sijapita nasikia kuna hiyo wanaita Baranco wall au Kissing rock nafikiri, hapo kupita lazima upambane na hiyo rock
 
Aseeh ko ktk route zako ni ipi favorite one na ugumu gani ulikumbana nao mpl ukasema gari hii basi Tena, vipi kwenye kufurahia utalii napo ulivutiwa na nn zaidi na je msosi mnapika ama ni junk foods mnatumia ??
 
Aseeh ko ktk route zako ni ipi favorite one na ugumu gani ulikumbana nao mpl ukasema gari hii basi Tena, vipi kwenye kufurahia utalii napo ulivutiwa na nn zaidi na je msosi mnapika ama ni junk foods mnatumia ??
Njia inayopendwa na wengi ina starehe, utalii wa kutosha na haiumizi sana ni hiyo ya kupitia Marangu.
Inaitwa coca cola route kwa utani
Wanatumia ascent siku 6-7, descent siku 2-3
Kuna tents na camps za kutosha za kupumzikia( Mandara, Horombo, Kibo) na chakula mnaweza kupika humo kwenye camps
Wale porter wanabeba mizigo ya chakula na takataka mkishuka, hakuna kutupa kitu mlimani

Wanasema Rongai ni rahisi kutoboa ila inabidi uwe fit hasa na ni fupi, tulipanda siku 3 na kushuka siku 1 kushukia Marangu , tulikuwa ma teenager tunawaiga wajeshi, ilikuwa poa na vibe ya wajeda kila mtu alitoboa

Hiyo ya Mawenzi wanasema ni toughest, sijapita ndiyo nataka kuijaribu Dec
Chakula mnaweza kubeba kilichopikwa mnapasha moto mkipumzika
Kwa hali ya kule kuna watu wanalazimishwa kula kama watoto sometimes
 
Umenikumbusha hapo breakfast...unaweza jushungusha kweny hilo jiwe hadi nusu saa..kwa mara ya kwanza kupaona nlidhani hapapitiki ila niliweza papita ila kwa tabu sanaa
 
Pitia na lemosho. ....njia refu kuliko zote nahc
 
Pitia na lemosho. ....njia refu kuliko zote nahc
Yeah, ila siku nyingi na gharama inaongezeka kukaa kule juu nako ingawa ina best experience
Nikiweza kupanda kupitia Machame next time nitajipanga na hiyo
Jamaa yangu amepita route zote na kuzirudia mara kwa mara
 
Ukiweza kutembea kwenye vilima kwa Dar kama maeneo ya Makongo au Goba au ukipata nafasi unapiga camp maeneo ya milimani kama Marangu kupata acclimatization itakusaidia
Wazungu wengi inawasaidia sana hali ya hewa ya kwao licha ya mazoezi
Mwaka huu na mimi nataka nipande. Mimi mazoezi yangu ni kucheza mpira wa miguu tu vipi nitatoboa mpaka summit?
 
Mwaka huu na mimi nataka nipande. Mimi mazoezi yangu ni kucheza mpira wa miguu tu vipi nitatoboa mpaka summit?
Mpira hautoshi. Hauko active muda wote unakuwa na short burst of activity na kutembea au kukimbia kidogo
Lazima ufanye mazoezi ya kutembea umbali mrefu hasa kwenye vilima, hiking au kupanda ngazi kujenga stamina, endurance na sustained cardio fitness
Kule mnatembea tu, mnatembea km 60 mpka 70 kuuzunguka mlima, kwa hatua za taratibu
Kila mtu mpaka wazungu wanajua neno “pole pole”
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…