Haya ni mambo sita (06) ya kujifunza kabla hujaanza kuishi mwenyewe magetoni tafadhali

Haya ni mambo sita (06) ya kujifunza kabla hujaanza kuishi mwenyewe magetoni tafadhali

Mwachiluwi

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2022
Posts
33,977
Reaction score
67,600
1️⃣ >Jua kwamba sasa umepata uhuru ambao ukiutumia vibaya basi maisha yako yanaenda kuharibika mara moja. Kuna wengine mmekuwa salama kwa sababu mlikuwa mkiishi kwa wazazi na walezi wenu hivyo sheria zao zimewalinda na mkawa salama . Sasa unaanza kuishi mwenyewe usalama wako ni jukumu lako.


2️⃣ > Heshimu chumba chako. Achana na ile tabia ya kuazimisha kitanda chako kwa rafiki yako au mtu mnaefahamiana nae waje na mtu wake wafanyie mapenzi kwenye kitanda chako. Unachafua kitanda chako kwa roho chafu na ndiyo mwanzo wa mikosi. Kwanini mtu aje afanye uasherati kwenye kitanda chako? Kwani hakuna nyumba za wageni?


3️⃣ >Unahitaji kuwa na tabia itakayoendana na wapangaji wenzako bila kuwakera, kumbuka hapa unaishi na watu tofauti wenye tabia tofauti. Haitakuwa vyema ukaonekana wewe ni msumbufu kwa wenzako, watakuchoka mapema na utahamahama nyumba kila wakati. Hapo siyo kwenu ,usifanye mambo kama upo kwa wazazi wako.


4️⃣ > Ishi vyema na majirani maana hao ndiyo watakubeba usiku ukizidiwa. Inakubidi ujilazimishe tu kwa kila namna uishi nao ukijua kwamba wao ndiyo watakuwa wa kwanza kukusaidia ukipata changamoto.


5️⃣ > Epuka kuwa sehemu ya kuwapiga majungu majirani zako, haitazuia wao kukupiga majungu lakini haimaanishi uingie kwenye vita ya umbea na kusemana Semana na watu wakati una mambo ya msingi ya kufanya.


6️⃣ > Sehemu hiyo wewe ndiyo unalipa kodi lakini angalia pasije kugeuka kaburi la kukuzikia wewe mwenyewe, unaweza ukadhani kwamba sasa upo huru kuleta na kulala na kila kiumbe kinachotembea huko nje. Utakufa kwa magonjwa, watu wanaumwa sana siku hizi. Jali maisha yako.
 
Screenshot_20251208-103546.jpg
 
Mimi sio kijana wako jiheshimu kijana kusoma shule moja haimaanishi tunalingana,

Nimepita pale lyabii miaka ya 80's mwanzoni mm ni baba yako,
Mimi nilipita miaka 60 wakati shule ukiwa change kabisa. Waalimu kipindi kile walikuwa wazungu.

Kwa hivyo, niombe radhi kwa kunidhalilisha mbele ya hili jukwaa linaloniheshimu.
 
Kwanza wanawake kwanza wana mikosi.Ukijingiza tu huko unakuwa maskin.Bora uishi tu single na ufurahie maisha,mwanaume sio lazima uishi na mwanamke.mimi na miaka 45 na sijawai kuwa na mpenzi na maisha yangu ipo vizr na sina stress.Ama hisia zikikusumbua piga nyeto na mambo itakuwa vizuri.mm napiga nyeto mara saba kwa siku na nnakuwa najitosheleza vzr,bila hata kuhitaji mwanamke.
 
Back
Top Bottom