Haya ni mambo sita (06) ya kujifunza kabla hujaanza kuishi mwenyewe magetoni tafadhali

Haya ni mambo sita (06) ya kujifunza kabla hujaanza kuishi mwenyewe magetoni tafadhali

1️⃣ >Jua kwamba sasa umepata uhuru ambao ukiutumia vibaya basi maisha yako yanaenda kuharibika mara moja. Kuna wengine mmekuwa salama kwa sababu mlikuwa mkiishi kwa wazazi na walezi wenu hivyo sheria zao zimewalinda na mkawa salama . Sasa unaanza kuishi mwenyewe usalama wako ni jukumu lako.


2️⃣ > Heshimu chumba chako. Achana na ile tabia ya kuazimisha kitanda chako kwa rafiki yako au mtu mnaefahamiana nae waje na mtu wake wafanyie mapenzi kwenye kitanda chako. Unachafua kitanda chako kwa roho chafu na ndiyo mwanzo wa mikosi. Kwanini mtu aje afanye uasherati kwenye kitanda chako? Kwani hakuna nyumba za wageni?


3️⃣ >Unahitaji kuwa na tabia itakayoendana na wapangaji wenzako bila kuwakera, kumbuka hapa unaishi na watu tofauti wenye tabia tofauti. Haitakuwa vyema ukaonekana wewe ni msumbufu kwa wenzako, watakuchoka mapema na utahamahama nyumba kila wakati. Hapo siyo kwenu ,usifanye mambo kama upo kwa wazazi wako.


4️⃣ > Ishi vyema na majirani maana hao ndiyo watakubeba usiku ukizidiwa. Inakubidi ujilazimishe tu kwa kila namna uishi nao ukijua kwamba wao ndiyo watakuwa wa kwanza kukusaidia ukipata changamoto.


5️⃣ > Epuka kuwa sehemu ya kuwapiga majungu majirani zako, haitazuia wao kukupiga majungu lakini haimaanishi uingie kwenye vita ya umbea na kusemana Semana na watu wakati una mambo ya msingi ya kufanya.


6️⃣ > Sehemu hiyo wewe ndiyo unalipa kodi lakini angalia pasije kugeuka kaburi la kukuzikia wewe mwenyewe, unaweza ukadhani kwamba sasa upo huru kuleta na kulala na kila kiumbe kinachotembea huko nje. Utakufa kwa magonjwa, watu wanaumwa sana siku hizi. Jali maisha yako.
Ahsante mkuu...wengine ndio tunaanza haya maisha Januari
 
Nakumbuka enzi hizooo nimeingia kuoga daah mkono ukapita kunako sasa ndo tatizo mpaka leo
Mm niliona watu wajinga mbona sisikii raha maana nilitumia sabuni ya mkaa nikaitupa nikaoga nikatoka bafuni sasa kuna demu kaja nifundisha uzee i ashukuriwe sana
 
Back
Top Bottom