Sielewagi kila mara Yanga kuhusishwa na kuhonga/ kutoa rushwa ili ishinde.
1. Je, Yanga haina timu nzuri, na hvyo haijiamini??
2. Je, kama mpk mtu baki anajua, bodi ya ligi haijui na kuichukulia hatua Yanga..???
3. Yanga wanahela nyingi kiasi cha kununua kila mechi mpaka bodi ya Ligi…?? ( Hii ni kwa sababu kila inapotokea wameshinda, watu husema Yanga wamenunua mechi..!!)
4. Timu zingine ni maskini kiasi gani na hawataki ubingwa/ushindi kiasi gani mpaka wakubali kununuliwa na Yanga..??
5. Ubingwa wa Simba mara 4 mfululizo haukuhusisha kununua gimu yoyote..??
6. Ubingwa wa Yanga mara 2 mfululizo ulitokea kwa sababu alinunua mechi nyingi au ni juhudi za wachezaji…??
7. Simba alishawahi kutaka kununuliwa akakataa?? Na kama alikataa kwanini asiripoti bodi ya ligi..??
8. Kama ameweza kununua TIMU ZINGINE ZOTE, kwanini asiwe bingwa MIAKA YOTE mpk akaruhusu Simba akachukua ubingwa mfululizo..??
Nway, hayo ni maswali machache kati ya mengi kuhusiana na hiyo tuhuma ya Yanga kununua matches kila siku. Na nadhani watuhumu wengi hawana UHAKIKA THABITI wa tuhuma wanazotoa zaidi ya kuongea wakiongozwa na ushabiki na upenzi wa timu zao wanazoshabikia.