Hayati Dkt. Magufuli anapohukumiwa kwa kifo chake

Hivi Mungu hakuwa anajua kuwa Kaini atakuja kumuua Abeli?
 
Huyu ulivuka mipaka hata ya kiuumbaji,unakumbuka kwamba alisema atamuomba mungu angalau ampe kazi ya kuongoza Malaika!
 
Unawezaje kumfananisha Yesu na shetani?

Kama unawafananisha mwambieni na yeye afufuke sasa kama Yesu kisha apae mbinguni kwenda kuwafagiloa malaika.
Yeye kama maandiko anayajua aanze kushusha nondo hapa na sisi tumshushie. Katika mada yake katolea mifano ya mitume wawili waliokufa bado vijana wadogo na wakiwa na maadui wengi. Hajui maisha ya Yesu duniani yalikuja kwa mpango wa Mungu na ilikuwa lazima afe msalabani afufuke na arudi kwa Mungu.

Kamzungumzia mtume Muhamad alikufa bado kijana mdogo na alikuwa na maadui wengi.

Sasa mwambie atetee hoja zake kwa vifungu vya maandiko matakatifu kama ataweza. Unaleta mada za kipuuzi kumtetea mpuuzi.

Alafu anasema viongozi wa nchi huwekwa na Mungu. Mungu hawezi support ujinga alioufanya Magufuli.
 
Huyu ulivuka mipaka hata ya kiuumbaji,unakumbuka kwamba alisema atamuomba mungu angalau ampe kazi ya kuongoza Malaika!
Hukumu utolewa na Mungu na hasa binadamu akiwa kesha toweka katika ulimwengu huu wa nyama
 
wengi wa wanaomponda dr magufuli, hata wao hawajielewi!

unategemea watamuelewa magufuli!

mtu aliyewaambia tunaweza kufanya tuliyoaminishwa hayawezekani!

binafsi huwa nawapuuzia tu

ukijadili nao mtaonekana wote wehu!
 
Sasa mbona unasema kuna watu wamemhukumu, kiazi wewe
Hukumu utolewa na Mungu, si Binadamu!
Mwenye matusi uwa namashaka na malezi aliyoyapata kwa wazazi wake, na udhihirisha namna asivyoelimika kwa upuuzi, na malezi yasiyofaa. Nzi ufuata harufu mbaya. Na inzi ukulia chooni! Na siku zote nzi akiona kinachonuka ufuata akijua ni choo. Hii utokana na malezi ya chooni kwa huyo nzi.
 
Sasa mbona unahukumu. Mkuu huna ukomavu kiimani. Kaa utulie.
Umejuaje binadamu mwenye matusi imetokana na malezi ya wazazi wake? Kumbe hujui hata uliposimamia. Kama upo upande wa Imani kubali matusi mkuu
 
wengi wa wanaomponda dr magufuli, hata wao hawajielewi!

unategemea watamuelewa magufuli!

mtu aliyewaambia tunaweza kufanya tuliyoaminishwa hayawezekani!

binafsi huwa nawapuuzia tu

ukijadili nao mtaonekana wote wehu!
Hawa watu wenye chuki kwa magufuli wanadhani wanaogopwa. Wanakuja na matusi. Acha nile nao sahani moja. Wasidhani tunawaogopa! Wakajiona ndo wenye kusema. Upumbavu utajibiwa kipumbavu! Heri niwe mwehu lakini nibaki nikitetea ninacho kiamini! Nitasema kweli daima fitina kwangu mwiko! Let me enjoy them, nina muda na ninanguvu za kuwajibu!
 
Kwahy ulitakaje ulitaka watu tuhuzunike kwa upumbavu wake?
 
Well narrated Wilderness Voice

Ukweli utabaki kuwa ukweli JPM alikuwa Rais bora na kiatu chake hakuna kitakayeweza kumtosha.

Watanzania tumemkumbuka sana tunalia usiku na mchana,nchi sasa hivi HAIELEWEKI tupo tupo tu kwa kudra za Maulama.

TUSISAHAU KULIOMBEA TAIFA KILA TUSALIPO/TUOMBAPO.
 
Kwa imani tunaamini mfumo wa serikali za hapa duniani ni mfumo ulioigwa kutoka katika serikali kuu ambayo ni ya Mungu

Hapo mwanzo Mungu huyo huyo aliongoza falme mbalimbali za haki kuwasambalatisha wale wote
waliopanga kukwamisha mipango ya Mungu katka mataifa hayo

Pamoja na yote hayo bado wafalme hao wa haki walikufa kwa style tofauti tofauti huku Mungu pekee akibakia na hukumu zao

Lakini binadamu wa leo wamebaki kuwa wajuaji hata kusahau yanayo wahusu na familia zao wamejigeuza miungu watu hata kutoa hukumu huku nao wakisuburi kuhukumiwa

Ukiwa na akili timamu jiulize swali moja tu ni serikali ipi au awamu ipi kwenye uongozi wa nchi hii iliyomaliza uongozi wake bila lawama

wewe ukisifia wengine wataponda tu lazma. huwezi amini hadi leo hii kuna watu wanaamini mwalimu JK
alifanya makosa makubwa kwa taifa hili pamoja na juhudi zote za kulikomboa taifa hili

jiulize ni nani anaefaa unae msifia wewe wenzio wanamlaani

Waacheni wazee wetu wapumzike
 
Hamna mtu anakumbuka kiongozi dhalimu.
 

Dunian hapa wamepita watu wengi sana,

Toka kwa baba yetu Adam na mama yetu Anna wamepita watu wengi sana wema na wabaya,

Mungu kupitia manabii na mitume wake ametuelezea simulizi nyiingi sana za watu waliopita na kufariki na kuzikwa,

Siyo kwamba tulipewa simulizi zile kwa bahati mbaya la hasha,tumepewa simulizi zile ili ziwe funzo kwa sisi vizaz vya sasa na vizaz vijavyo,

Ili wale wanaobakia katika huu ulimwengu waweze kupata mazingatio,

Magufuli kweli kafariki,lakin yapo mazur kafanya na yapo mabaya kafanya,kuelezea maisha yake ni kutaka sisi tunaobakia hapa dunian tupate cha kujifunza kupitia maisha yake,na siyo kama ni kukufuru na kudhihaki kana kwamba sisi hatutakufa,la hasha
 

Nchi haileweki??

Labda kama ni kwenu huko Chato,nchi hiii ilikua almost imecollapse hii,

Unaweza kutupa vigezo gani unavyosimamia kusema kwamba nchi kwa sasa haieleweki kabla hatujaanza kukupa sisi vigezo vyetu??
 
Umeandika vizuri sana, ingawa tutakuelewa wachache sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…