Hayati Dkt. Magufuli anapohukumiwa kwa kifo chake

Hayati Dkt. Magufuli anapohukumiwa kwa kifo chake

Kwa taarifa yako mleta mada ni kwamba mara tu baada ya kifo cha mwendakuzimu kutangazwa wanyama wafugwao hasa wale wenye miguu 4 na 2 walikufa Sana kwa kichinjo na watu waligonga supu, mchemsho, nyama choma etc, katika hao waliosherehekea wamo babu zako, wakubwa zako aina mbalimbali, wapo walimu wako na wengine wanaokuzidi elimu, uchumi, busara, uelewa etc.
Sasa hii habari ya wewe kuteseka na kuanza kutaka kuwaelimisha watu kwamba mtu akifa hasemwi vibaya usijisumbue waache watu wafurahie kifo cha mtesi wao, hutoweza kuzuia hili hata mwenyewe alisema "nikifa mnikumbuke kwa mema", sasa mtu kama Lissu amkumbuke mwendakuzimu kwa wema upi? Wake na wazazi wa akina Leopold Lwajabe, Azory Gwanda, Ben saa8, etc nao wamkumbuke kwa wema upi? Yeye aendelee kuungua huko kuzimu kutokana na matendo yake.
Nichukue nafasi hii kukukumbuxha mleta mada kwamba unatakiwa kutenda mema hapa duniani ili ujiwekee akiba yenye mustakabali mwema huko baadae na ukikaidi ukafanana na huyo gaidi utakumbana na dhahama, don't 4get the rule of karma.
 
uzuri maandishi haya hayafi.

usijimalize sana ndugu.
hatubadilishi misimamo mpaka kizazi Cha tatu kutoka sisi kije kijue tulipinga upuuzi wa jiwe Toka akiwa hai mpaka akiwa mfu hatukwepeshi muraaa
Na tuna sababu zetu Kama Ninyi mlivyo na sababu zenu za kumpenda Hivyo tusipangiane!
 
Kwa taarifa yako mleta mada ni kwamba mara tu baada ya kifo cha mwendakuzimu kutangazwa wanyama wafugwao hasa wale wenye miguu 4 na 2 walikufa Sana kwa kichinjo na watu waligonga supu, mchemsho, nyama choma etc, katika hao waliosherehekea wamo babu zako, wakubwa zako aina mbalimbali, wapo walimu wako na wengine wanaokuzidi elimu, uchumi, busara, uelewa etc.
Sasa hii habari ya wewe kuteseka na kuanza kutaka kuwaelimisha watu kwamba mtu akifa hasemwi vibaya usijisumbue waache watu wafurahie kifo cha mtesi wao, hutoweza kuzuia hili hata mwenyewe alisema "nikifa mnikumbuke kwa mema", sasa mtu kama Lissu amkumbuke mwendakuzimu kwa wema upi? Wake na wazazi wa akina Leopold Lwajabe, Azory Gwanda, Ben saa8, etc nao wamkumbuke kwa wema upi? Yeye aendelee kuungua huko kuzimu kutokana na matendo yake.
Nichukue nafasi hii kukukumbuxha mleta mada kwamba unatakiwa kutenda mema hapa duniani ili ujiwekee akiba yenye mustakabali mwema huko baadae na ukikaidi ukafanana na huyo gaidi utakumbana na dhahama, don't 4get the rule of karma.
very well my friend karma is bitch!
Niwe muwazi tu mbele ya raia wa Tanzania kwamba kifo Cha yule bwana hata hakikistua mtima wangu maana ni kitu nilichokua naomba kitokee na nilikitarajia Muda wowote maana
Kwa matendo ya yule bwana niliamini Bora atangulie japo nitamfuta ila akiwa wa kwanza yeye moyo wangu utasuuzika kabisa,maana haiwezekani ujaribu kumtoa mwenzako roho kisa siasa
Yaani siasa tu Ndio uwe na roho ya jiwe hapana ndugu zanguni pale tulipigwa!
 
Ndio maana tunakuambia umezidiwa na mahaba mpaka sasa unakana hata maneno yako mwenyewe, mchelea mwana kulia hulia yeye, ndilo linalokukuta sasa, ulikuwa na wkati mzuri wa kumkumbusha mahaba wako huu uzi ulioweka leo hapa labda yeye angekusikia, kwa kuwa tulimuasa sana hapa kuwa aache visasi, hakusikia, mbona husemi kuwa kisasi ni Cha Mungu! Sisi hapa hatuhukumu bali tunakumbusha kuwa kama ilivyo wema kuwa ni mbegu ubaya nao ni mbegu lazima iote. Hata hukumbuki andiko juu ya kuikumbusha nyumba ya Yakobo dhambi zao!
Hutakiwi kuhukumu mwenye kuhukumu ni Mungu pekee ndiyo mada yangu.
 
Wewe hasa umekazana kutetea Nini? Usikumbushe watu na kuwaudhi kuhusu utawala huo MBOVU ulioacha makovu. Tuongee mengine tu tusikumbushane inaleta hasira.
Hatutakiwi kuhukumu mwenye hukumu ni mwenyezi Mungu ndo mada yangu.
 
Tatizo alianza kula nyama ya binadamu na kuizoea. Karma ikaona isiwe shida akapewa jeuri dhidi ya kirusi corona nacho kikampumzisha fasta fasta.

On a very serious note. Mleta mada usipoteze muda kuhangaika na wanaosherehekea kifo cha mwendazake. Ni hulka mbaya lakini halisi ya kibinadamu. Ni kama vile watu wanavyochangamkia kumchoma moto kibaka. Binadamu wengi ukiwasababishia maumivu makubwa usitarajie wahuzunike siku ukifikwa na msiba. Na ukishangaa na kulalamika kwanini inakuwa hivyo, wewe ndio utakuwa na matatizo. Wala usijifariji kwa kauli "hata nyinyi mtakufa tu". Sawa, lakini yeye katangulia. Waingereza wana msemo "surviving someone". Lissu amemsurvive mbaya wake. Na kwa mtu aliyekuwa akijimwambafy (ref JK) kila mara, kutangulia "bila kutarajiwa" ni tatizo linalotafsiriwa kama adhabu - kibinadamu.

Kama wewe unaomboleza kifo cha mwendazake jua ni msiba wako binafsi. Usipoteze muda kutafuta ushirika. Kila mmoja wetu ana misiH

Ndio maana tunakuambia umezidiwa na mahaba mpaka sasa unakana hata maneno yako mwenyewe, mchelea mwana kulia hulia yeye, ndilo linalokukuta sasa, ulikuwa na wkati mzuri wa kumkumbusha mahaba wako huu uzi ulioweka leo hapa labda yeye angekusikia, kwa kuwa tulimuasa sana hapa kuwa aache visasi, hakusikia, mbona husemi kuwa kisasi ni Cha Mungu! Sisi hapa hatuhukumu bali tunakumbusha kuwa kama ilivyo wema kuwa ni mbegu ubaya nao ni mbegu lazima iote. Hata hukumbuki andiko juu ya kuikumbusha nyumba ya Yakobo dhambi zao!
Mwenye kuhukumu nae atahukumiwa.
 
Hutakiwi kuhukumu mwenye kuhukumu ni Mungu pekee ndiyo mada yangu.
Kwa hiyo wakati mwendakuzimu anapoteza watu, anaua hovyo, marisasi hovyo hovyo aliagana na Mungu au unajipa upofu? Mbona unaongea KINYUME na matendo ya huyo mtakatifu wako ambae pia ni mwendakuzimu?
 
Kwa hiyo wakati mwendakuzimu anapoteza watu, anaua hovyo, marisasi hovyo hovyo aliagana na Mungu au unajipa upofu? Mbona unaongea KINYUME na matendo ya huyo mtakatifu wako ambae pia ni mwendakuzimu?
Ahukumuye nae atahukumiwa! Over!
 
Mtoa mada elewa kwamba kufurahia au kushangilia tatizo linapompata mtu ni hulka ya mwanadamu na kwa muktadha huo ndio maana hata huyo Magufuli unaye mhurumiya leo alikuwa anaamuru wengine wauwawe.

Ndio maana ukisoma Biblia 1 Samuel 25:39 utaona jinsi Daudi alivyoshangilia kifo cha hasimu wake Nabal. Hivyo haya ni mambo ya kawaida kwa wanadamu, ukifariki sio wote watakaohuzunika wala kufurahi.

Huwezi leo ukaniambia mtu kama Lissu aliyepewa ulemavu wa maisha eti ahuzunikie kifo cha Magufuli na hiyo hali ni hivyo hivyo kwa ndugu wa Azory Gwanda na Beny Saanane.

Piga ua sisi ni binadamu tu, hatuwezi kugeuka kuwa malaika. Kindly advise please.
 
Ndiyo maana Corona iliporudi,ilianza na ndugu wa bwana yule alichekelea sana na yeye aki....debe.
Usitukane mamba kabla ya kuvuka mto.
 
hatubadilishi misimamo mpaka kizazi Cha tatu kutoka sisi kije kijue tulipinga upuuzi wa jiwe Toka akiwa hai mpaka akiwa mfu hatukwepeshi muraaa
Na tuna sababu zetu Kama Ninyi mlivyo na sababu zenu za kumpenda Hivyo tusipangiane!

hakuna anayekupangia,wasi wasi wangu ni vitukuu kuja kuona walikuwa na babu mwenye akili za hovyo.
 
hakuna anayekupangia,wasi wasi wangu ni vitukuu kuja kuona walikuwa na babu mwenye akili za hovyo.
labda watakuja kukushangaa wewe ulivyokua mjinga Kwa kua na mahaba na chama chakavu kilichofeli kuitoa nchi Kwenye umaskini uliotopea Kwa wananchi wake Kwa miaka zaidi ya 60 ya uhuru halafu Babu Kama wewe ukawa unatumika na kuhadaiwa Kama toilet paper Kwa kupewa tisheti na kofia ya kijani Ili uwapigie kura
Utashangawa sana!
 
Aliyemtuma Kingai na Mahita kumuua na kumtupa mozes lijenje ndio unayemtetea hapa? Aliye amuru mateso kwa makomandoo Adamoo na Lingwenya ndio unamsemea hapa? Tuache bhana tunajua kushughulika na wasaliti
Ikiwa ni yeye aliyeamrisha watu wateswe na kuuawa laana na adhabu havitamuepuka. Ikiwa ni wateule wake ndio walijiamulia kuteka, kutesa, kuua na kudhulumu kikombe hawatakiepuka na yeye atapata fungu lake kwa kufurahia uovu ule. Na yeyote anayeendeleza ndoto za kikatili na uonevu wakati huu asitaraji kuwa na amani ya nafsi...
Tujitafakari malipo yanaanzia hapahapa duniani...
 
Kifo ni tukio la kiasili. Katika imani kadhaa za kidini zina elezea kifo kilitokea baada ya Adamu na Hawa (Eva) kwenda kinyume na mapenzi ya muumba wao (MUNGU). Ndipo Mungu alitamka kuwa tutakufa, au kurejea katika mavumbi.

Binadamu wa kwanza kufa alikuwa Abeli. Ambaye aliuliwa na kakaye aitwae Kaini. Kaini japo alimuuwa Abeli, bado Mungu alimlinda Kaini na hata akasema atakae muuwa kaini basi atalaaniwa. Hivyo Mungu alimpeleka Kaini nchi ya mbali. Hii yote kumuepusha na kumlinda na mabaya. Mungu alifanya haya yote japo Kaini alikuwa na dhambi ya kumuuwa nduguye.

Mungu utazama tofauti, na macho ya binadamu. Na Mungu ndiye mwenye uweza wa kuhukumu. Siku hizi Tanzania hii kumezuka, tabia ambayo inaonesha watu kufurahia kifo au vifo vya watu wengine. Na kama walikuwa hawampendi huyo mtu au watu; ndo watazusha mengi. Wabaya wake watajifanya wao ni mungu (Mungu), watahukumu, watasema huyu alifanya mabaya ndo maana kafa.

Watajiona wao waliobaki ndo wajanja, hawana makosa au dhambi mbele ya Mungu. Najiuliza hivi kuna mahala popote pale iwe katika misaafu au maandiko yoyote ya kidini na imani zinginezo, pana sema mtu anae kufa mapema au kabla ya wenzie ana dhambi na Mungu kaamua kumkomoa?

Nachojua Mungu alisema tutakufa, hakuna atakaeishi milele hapa duniani. Ndo maana watu ufa wakiwa watoto wachanga, wakiwa vijana, wakiwa wazee, na hata watoto wengine ufia tumboni mwa mama zao kabla ya kuzaliwa.

Tukidai kufa mapema ni kukomolewa na Mungu, ebu tuangalie, hawa mitume wetu, walikufa bado wakiwa vijana, na walikuwa na maadui wengi, hawakupendwa. Yesu kristo aliishi miaka isiyozidi thelathini na tatu. Na alianza kazi ya kuhubiri akiwa na miaka thelathini tu. Vile vile kwa mtume Muhamad S.W.A alikufa mapema. Si hao tu ni wengi!

Hivyo kifo ni asili. Nachoamini kila mtu anakusudi la kuwepo duniani. Na pia ana muda wake wa kuishi. Haijalishi ni miaka mingapi. Muda ukifika Mungu ndo mwamuzi wa yote, uondoke au aseme bado ubaki.

Katika kila jambo Mungu anamakusudi yake. Laweza kuwa baya au zuri, lakini Mungu anatazama tofauti na tunavyotazama sisi wanadamu.

Kikubwa tusijipe kazi ya Mungu ikawa kazi yetu. Tusijipe kuhukumu kwani hukumu ya maisha yetu utolewa na Mungu. Usihukumu usije hukumiwa.

Nimeongea haya yote ni kutokana na watu wengi, wapinzani na wana CCM kuonekana kumhukumu alie kuwa Rais wa Tanzania, J.P. Magufuli na hata kumzodoa kuwa kafa mapema, yako wapi, kuonesha tu Mungu ati kamuondoa kwa mabaya yake. Nilishangaa hata Mchungaji mmoja anajiita mzee wa upako kuongea kama vile nae anaonesha kufa kwa magufuli ni kama adhabu, eti kisa Lowasa hakuchaguliwa Urais na kuwataka watu wakamuombe Msamaha Lowasa.

Mimi niseme kwa maandiko viongozi wote wakuu wa nchi uwekwa na Mungu. Mungu angeamua Lowasa kuwa Rais angekuwa tu. Mchungaji kasahau maandiko anatumia akili za kibinadamu. Kufa kwa Magufuli si kwamba Mungu hakutaka Magufuli awe Rais, la asha. Mungu hutenda kwa wakati wake.

Jiulize katika maandiko tunaambiwa kuwa Yusufu aliuzwa utumwani na nduguze, bado huyo Yusufu akafungwa gerezani. Lakini cha ajabu akaja kuwa ndiye waziri mkuu wa nchi. Hata nduguze walipojihisi atalipiza kisasi kwa kuwafanyia mabaya, aliwaambia. Mlikusudia mabaya kwangu, lakini katika hayo mabaya Mungu alikusudia mema ili nije niwaokoe katika baa la njaa.

Mungu uona mbali zaid ya binadamu. hatujui ni kwanini Mungu aliepusha Lowasa asiwe Rais japo ilitumika njia mbaya au nzuri, lakini Mungu anakuwa na makusudi yake. Mchungaji katafakari neno la Mungu ndo utoe tamko. Hakuna lifanyikalo duniani bila Mungu kuridhia. Mungu huyo aliruhusu Ayubu apate mateso, akaruhusu watoto wake Ayubu kufa na hata mali kuharibika na kupotea lakini alikuwa na kusudi. Kifo cha Magufuli kinakusudi liwe baya au zuri ila watanzania tutajifunza kutokana na hicho kifo siku moja. Kikubwa tusijichukulie mamlaka ya kuhukumu na kusema kafa kwa sababu alikuwa katiri na kadharika. Mbona Mungu alimlinda Kaini japo alikuwa muuwaji?

Hivi kazi yetu ni kuhukumu, kwani tuliobaki hatutakufa? wangapi tumefiwa na ndugu na wazazi, je kutangulia kwao ni kwamba walitenda mabaya Mungu kawahukumu? Kwa uzoefu wa haraka tu mara nyingi watu wema hawadumu? Iwapo hadi sasa unaishi lazima ujiulize, unatakiwa kulifanyia nini Taifa lako la Tanzania, na familia yako. Si kushambulia marehemu, na kujifanya wewe ni mungu unahukumu. Leo hata viongozi wetu utasikia, oooh! Magufuli hakutenda haki, alikuwa kiongozi mbaya, alikuwa muuwaji, alitisha, hakuwa na demokrasia!

Hivi ninyi viongozi mnao sema haya si mlikuwa nae ktk uongozi wa serikali? Kwanini amkumwambia wakati huo akiwa hai kuwa ni kiongozi mbaya.

Nacho jua Magufuli alikubali kukosolewa. Naibu Waziri wa afya kipindi hicho alimkosoa kuhusu matumizi ya kujifukiza. Akamwondoa katika nafasi. Lakini baadae alimrejesha ktk wizara tofauti.

Leo wanao mkosoa magufuli haohao, wanapinga Mhe. Rais Samia kukosolewa. Wakati Rais alidai kuwepo uhuru wa kukosoa. Lakini chama chake na Bunge Wanataka asikosolewe, tumsifie hata kwa yale yasio sifiwa. Wakati wanadai wao ni wanademokrasia. Ukikosoa unahesabika msaliti, Bunge litakuita kwenye Kamati. Chama kitakaa kukuita kikuhoji kwa nini huko kinyume na Rais. Chama kinachoongozwa na mwenyekiti ambae ni Rais alie ruhusu kokosolewa.

Mungu hapendi wafitini na watu waongo, wenye roho za usaliti. Viongozi mjitafakari. Na msijione ninyi hamta kufa. Kifo kipo akijali madaraka yako. Hakuna atakae ishi milele. Kuwepo kwako pengine Mungu anataka utimize mambo fulani. Ghazabu ya Mungu ni kubwa tusihukumu tukaja hukumiwa. Magufuli kaondoka kamaliza yake. Alifanya kwa nafasi yake na kwa staili yake. Watu wote hatufanani.

Tusijione sisi ni bora kwakuwa tu watu wanatuchekea na kutusifia. Tukachekelea na kuota kiburi kuona tuko sahihi na hatukosei! Pamoja na yote Magufuli aliwapenda watanzania. Hakuwahi kusema waondoke wakaishi Burundi.

Leo kauli hiyo inaongewa na kiongozi aliepewa dhamana na watanzania. Viongozi wamejiona wako juu ya sheria, wanauwezo wa kusema chochote. Viongozi wamekuwa na dharau. Wanajiona nchi ni yao. Hata wananchi kulalamika hawaoni haja ya kuomba msamaha.

Hata kiongozi wa nchi hawakanyi anawaacha je naye kafurahishwa na hayo maneno? Je kawatuma?
Harafu hawa hawa ndo wanasema watakuwa wapole na kuwabembeleza wananchi kuliko JPM ambaye kapewa mabaya yote.
Tukumbuke kutangulia kufa si dhambi. Na ukibakia si ujanja wa kufanya kutukana waliotangulia. Bali chukua muda wa kujitafakari.

Mungu alimlinda Kaini japo alikuwa muuwaji wa nduguye. Mungu ndiye mwenye kuhukumu. Na ndiye ajuaye mwisho wa maisha yetu. Jiulize hapo ulipo matendo uyafanyao ktk vificho au wazi, je ni mema? Je wewe ni msafi zaidi ya waliotangulia kufa?

Je, wajua kifo chako kitakuwaje? Lini utakufa? Je utakufa ukiwa na umri gani? Je alie kutangulia kafa akiwa na miaka mingapi?
Si ujanja wala umaarufu kutukana marehemu, au kutafuta umaarufu ati unajilinganisha na marehemu. Huyo kesha maliza wakati wake hayupo tena. Tuache kashfa hatujui kesho yetu. Tanzania ya leo imekuwa na siasa za kujipendekeza, sifa za kijinga, badala ya kufikiria maendeleo ya kweli. Walio tangulia tuwaache, tujenge nchi.
Kuwaacha waliotangulia sio shida. Shida ipo kwenye kuziacha sifa,tabia na matendo waliyoyaacha. Sifa,tabia na matendo yao yanaendelea kuishi haijalishi ni mazuri au ya hovyo.
 
Sielewi hata unachokiongelea, Hata Yesu alipokufa watu walifurahia! Angalia Biblia watu wengi wema walipokufa maadui zao walishangilia! Mungu wetu haukumu kwa kuangalia watu wanasema nini!
Basi kwanini watu walijazana kwenye kifo chake kama kweli alngekuwa anachukiwa kwa uzushi huo wanao usema ttungeona barabara empty!
Kujazana sio tija,wengine wanaenda kuhakiki tu kama kweli kafa au ni uzushi tu kama ule wa 2019. Inaonekana wewe ni miongoni mwa wale wanaojidanganya kwamba watu wakijaa kwenye msiba wako basi ndio tiketi ya kwenda mbinguni. Kujaa kwa watu msibani siyo "kujaa kwa Mungu"
 
Back
Top Bottom