Hayati Dkt. Magufuli anapohukumiwa kwa kifo chake

Kwa taarifa yako mleta mada ni kwamba mara tu baada ya kifo cha mwendakuzimu kutangazwa wanyama wafugwao hasa wale wenye miguu 4 na 2 walikufa Sana kwa kichinjo na watu waligonga supu, mchemsho, nyama choma etc, katika hao waliosherehekea wamo babu zako, wakubwa zako aina mbalimbali, wapo walimu wako na wengine wanaokuzidi elimu, uchumi, busara, uelewa etc.
Sasa hii habari ya wewe kuteseka na kuanza kutaka kuwaelimisha watu kwamba mtu akifa hasemwi vibaya usijisumbue waache watu wafurahie kifo cha mtesi wao, hutoweza kuzuia hili hata mwenyewe alisema "nikifa mnikumbuke kwa mema", sasa mtu kama Lissu amkumbuke mwendakuzimu kwa wema upi? Wake na wazazi wa akina Leopold Lwajabe, Azory Gwanda, Ben saa8, etc nao wamkumbuke kwa wema upi? Yeye aendelee kuungua huko kuzimu kutokana na matendo yake.
Nichukue nafasi hii kukukumbuxha mleta mada kwamba unatakiwa kutenda mema hapa duniani ili ujiwekee akiba yenye mustakabali mwema huko baadae na ukikaidi ukafanana na huyo gaidi utakumbana na dhahama, don't 4get the rule of karma.
 
uzuri maandishi haya hayafi.

usijimalize sana ndugu.
hatubadilishi misimamo mpaka kizazi Cha tatu kutoka sisi kije kijue tulipinga upuuzi wa jiwe Toka akiwa hai mpaka akiwa mfu hatukwepeshi muraaa
Na tuna sababu zetu Kama Ninyi mlivyo na sababu zenu za kumpenda Hivyo tusipangiane!
 
very well my friend karma is bitch!
Niwe muwazi tu mbele ya raia wa Tanzania kwamba kifo Cha yule bwana hata hakikistua mtima wangu maana ni kitu nilichokua naomba kitokee na nilikitarajia Muda wowote maana
Kwa matendo ya yule bwana niliamini Bora atangulie japo nitamfuta ila akiwa wa kwanza yeye moyo wangu utasuuzika kabisa,maana haiwezekani ujaribu kumtoa mwenzako roho kisa siasa
Yaani siasa tu Ndio uwe na roho ya jiwe hapana ndugu zanguni pale tulipigwa!
 
Hutakiwi kuhukumu mwenye kuhukumu ni Mungu pekee ndiyo mada yangu.
 
Wewe hasa umekazana kutetea Nini? Usikumbushe watu na kuwaudhi kuhusu utawala huo MBOVU ulioacha makovu. Tuongee mengine tu tusikumbushane inaleta hasira.
Hatutakiwi kuhukumu mwenye hukumu ni mwenyezi Mungu ndo mada yangu.
 

Mwenye kuhukumu nae atahukumiwa.
 
Hutakiwi kuhukumu mwenye kuhukumu ni Mungu pekee ndiyo mada yangu.
Kwa hiyo wakati mwendakuzimu anapoteza watu, anaua hovyo, marisasi hovyo hovyo aliagana na Mungu au unajipa upofu? Mbona unaongea KINYUME na matendo ya huyo mtakatifu wako ambae pia ni mwendakuzimu?
 
Kwa hiyo wakati mwendakuzimu anapoteza watu, anaua hovyo, marisasi hovyo hovyo aliagana na Mungu au unajipa upofu? Mbona unaongea KINYUME na matendo ya huyo mtakatifu wako ambae pia ni mwendakuzimu?
Ahukumuye nae atahukumiwa! Over!
 
Mtoa mada elewa kwamba kufurahia au kushangilia tatizo linapompata mtu ni hulka ya mwanadamu na kwa muktadha huo ndio maana hata huyo Magufuli unaye mhurumiya leo alikuwa anaamuru wengine wauwawe.

Ndio maana ukisoma Biblia 1 Samuel 25:39 utaona jinsi Daudi alivyoshangilia kifo cha hasimu wake Nabal. Hivyo haya ni mambo ya kawaida kwa wanadamu, ukifariki sio wote watakaohuzunika wala kufurahi.

Huwezi leo ukaniambia mtu kama Lissu aliyepewa ulemavu wa maisha eti ahuzunikie kifo cha Magufuli na hiyo hali ni hivyo hivyo kwa ndugu wa Azory Gwanda na Beny Saanane.

Piga ua sisi ni binadamu tu, hatuwezi kugeuka kuwa malaika. Kindly advise please.
 
Ndiyo maana Corona iliporudi,ilianza na ndugu wa bwana yule alichekelea sana na yeye aki....debe.
Usitukane mamba kabla ya kuvuka mto.
 
hatubadilishi misimamo mpaka kizazi Cha tatu kutoka sisi kije kijue tulipinga upuuzi wa jiwe Toka akiwa hai mpaka akiwa mfu hatukwepeshi muraaa
Na tuna sababu zetu Kama Ninyi mlivyo na sababu zenu za kumpenda Hivyo tusipangiane!

hakuna anayekupangia,wasi wasi wangu ni vitukuu kuja kuona walikuwa na babu mwenye akili za hovyo.
 
hakuna anayekupangia,wasi wasi wangu ni vitukuu kuja kuona walikuwa na babu mwenye akili za hovyo.
labda watakuja kukushangaa wewe ulivyokua mjinga Kwa kua na mahaba na chama chakavu kilichofeli kuitoa nchi Kwenye umaskini uliotopea Kwa wananchi wake Kwa miaka zaidi ya 60 ya uhuru halafu Babu Kama wewe ukawa unatumika na kuhadaiwa Kama toilet paper Kwa kupewa tisheti na kofia ya kijani Ili uwapigie kura
Utashangawa sana!
 
Aliyemtuma Kingai na Mahita kumuua na kumtupa mozes lijenje ndio unayemtetea hapa? Aliye amuru mateso kwa makomandoo Adamoo na Lingwenya ndio unamsemea hapa? Tuache bhana tunajua kushughulika na wasaliti
Ikiwa ni yeye aliyeamrisha watu wateswe na kuuawa laana na adhabu havitamuepuka. Ikiwa ni wateule wake ndio walijiamulia kuteka, kutesa, kuua na kudhulumu kikombe hawatakiepuka na yeye atapata fungu lake kwa kufurahia uovu ule. Na yeyote anayeendeleza ndoto za kikatili na uonevu wakati huu asitaraji kuwa na amani ya nafsi...
Tujitafakari malipo yanaanzia hapahapa duniani...
 
Kuwaacha waliotangulia sio shida. Shida ipo kwenye kuziacha sifa,tabia na matendo waliyoyaacha. Sifa,tabia na matendo yao yanaendelea kuishi haijalishi ni mazuri au ya hovyo.
 
Kujazana sio tija,wengine wanaenda kuhakiki tu kama kweli kafa au ni uzushi tu kama ule wa 2019. Inaonekana wewe ni miongoni mwa wale wanaojidanganya kwamba watu wakijaa kwenye msiba wako basi ndio tiketi ya kwenda mbinguni. Kujaa kwa watu msibani siyo "kujaa kwa Mungu"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…