Hayati Dkt. Magufuli anapohukumiwa kwa kifo chake

Hayati Dkt. Magufuli anapohukumiwa kwa kifo chake

Tunamshukuru Mungu kwa kutuondolea yule kiongozi muovu aliyeko motoni bila damu kumwagika.
Na wewe umejifikiria lini utaondolewa, na unajua unao wanao kuchukia hapo ulipo! Nyani haoni kundule!
 
Shida husomi mada nzima unachagua kisentensi badala ya kungalia yaliyoelezwa ndani, shetani ni yule ambae anatafuta kijisabau badala ya kuangalia nini kinaonglewa. Rudi utazame nilichoongelea siyo kuchua sentensi moja ambayo ukisoma zaidi inaufafanuzi zaidi. Wewe unae jua mbona usomi mada nzima ukaelewa. Shetani ujifanya kujua lakini hajui. Panua akili yako ya kufikiri.
Mkuu jibu nani aloandika vile kwamba kifo ni mpango wa Mungu?

Na usiwakataze watu kufurahia kifo cha wakala wa shetani. Furaha siyo hukumu. Hukumu ataitoa Mungu.

Na pia watu wanaimani tofauti tofauti. Tambua kuna watu hawaamini kama Mungu yupo so please kaa kwa kutulia maana wewe mwenyewe huelewi unachoandika
 
Kwani mwenzetu wewe unasoma maandiko yapi! Si ndio hayo yanayosema auaye kwa upanga atakufa kwa upanga! Si ndio hayo yamesema ole wake amwagae damu zisizokuwa na hatia! Si ndio hayo yaliyosema yaliyofungwa hapa duniani na mbinguni pia! Be serious.
Wewe hauko serious! katika ukristo hakuna kuuwa kwa upanga. Petro alipomkata sikio kwa upanga wale askari waliotumwa kumkamata Yesu, Yesu alimkemea petro na kuchua sikio lilokatwa na kuliuunga kwa yule askari.
Mafundisho ya Kikristo yanasema samehe hata saba mara sabini! Hivyo tafakari unaongelea mafunzo yapi ya dini ipi! Na wapi imeandikwa upanga kwa upanga! Be serious
 
Sasa mbona wew ndiye mwenye chuki, unasema tusihukumu ili hali unasema jamaa atakufa kifo cha ajabu. Wasukuma bhan, hata mkizeeka bado mnakuwa vile, mkipewa madaraka mnakuwa kama Jiwe.
Hiyo si chuki nakupa ukweli, ndo maana nimesema usihukumu. Neno linasema ukihukumu nawe utaukumiwa. Jenga hoja si kuleta lugha za hovyo kwangu. Humu nadani mnadhani ukija kwa matusi utaogopwa. Unavyokuja nami nakuja kihivyo! Pia usiwadharau wasukuma. Ebu nawe weka wazi kabila lako uchambuliwe!
Ondoa chuki za kikabila, huo ni ushetwani!
 
Alikuwa na mamlaka ya kuunda tume ya kijaji kufuatilia matukio haya ambayo yalikuwa na public interest, he never did that, now will you tell us the motive behind! Makosa yapo ya kutenda na kutokutenda yote yaweza kuwa makosa.
Nimeongelea kuhukumu baada yakifo, hayo ungemwambia wakati yuko hai, hayani husu. Elewa mada!
 
Hivi ni wapi kwenye biblia imeandikwa Yusufu alikuwa Waziri Mkuu?
 
Ukisoma maandiko kuna watakatifu walikufa vifo vibaya, kuna waliokata vichwa, kuna waliokaangwa kenye mafuta. Acha kiburi cha uzima wewe uwezi jua kifo chako. Usijisifie kwa ujionavyo wewe! Jiulize Mungu anakuonaje? Hakuna dhambi kubwa wala ndogo! Pia hata kumsema mwenzio si haki mbele za Mungu!
Ndugu yangu wanaofurahia kifo cha Magufuli ni wale wenye Ulemavu wa Teolojia. Wanadhania Mungu yuko kupambana na kuwashikia mijeledi Wakosefu. Mungu hatendi mambo katika Context kama hiyo. Waprotestanti wanadhania ukimuombea mtu mkosefu mabaya Mungu anapokea Sala kama hizo. Magufuli alikufa Kifo cha Kawaida kama wafu wengine na si kutokana na makosa yake. Hata Asingekuwa Raisi na kutenda hayo mabaya bado angekufa tu. Na hata angetanda Mazuri hiyo isingezuia kufa kwake
 
Hakuna sehemu aliyosafishwa, na siko kusafisha, bali naongea wazi hakuna chuki ya marehemu duniani. Kujenga chuki kwa mtu alokufa nadhani ni kutokuwa na akili za kufikiri. Nimeongelea kifo chake na yasemwayo kwa hicho kifo. Sasa nimsafishe kwa nani?

Nyie ndo mtakao kufa vifo vya ajabu na vibaya! Wewe si Mungu kuhukumu!

Sasa nimtetee Magufuli kwani anagombea uRais. Soma uelewe mada chuki zako usikimbie na kuandika tofauti ya mada.

Napenda kukukumbusha utakufa pia, je umetafakari maisha yako?
Magufuli sio wa kutetea popote pale, watu waliteseka na bado mengi hayajulikana.
 
Mkuu jibu nani aloandika vile kwamba kifo ni mpango wa Mungu?

Na usiwakataze watu kufurahia kifo cha wakala wa shetani. Furaha siyo hukumu. Hukumu ataitoa Mungu.

Na pia watu wanaimani tofauti tofauti. Tambua kuna watu hawaamini kama Mungu yupo so please kaa kwa kutulia maana wewe mwenyewe huelewi unachoandika
Nimekwambia soma mada nzima, unataka mimi ndo nikusomee! watu wengine wa ajabu! Pia kutokuwa na dini sio utenda maovu. Zamani watu wengi hawakuwa na dini, lakini walikuwa na hofu ya kuhukumu. Tazama nchi za Ulaya ambazo haziamini hakuna Mungu, uwezi ukakuta mtu ana hukumu mwezie alokufa.
Kwa nature ya binadamu anahofu, hata kama haamini Mungu lakini kuna nguvu nyingine anayo amini.
Na hakuna sheria inayozuia mtu asiongelee kile anachokiamini, mimi naamini juu ya Mungu anaishi, na alie umba mbingu na dunia. Nitamwelezea popote pale, siogopi chochote! Naamini anaukuu wa kuonesha uwezo na nguvu zake!
Hivi unadhani mimi natishwa, au katika mada mtu kuokoteza sentensi na kuanza mashambulizi. Kajipange! Mtu ambae anauelewa usoma mada nzima, si unaokoteleza kaneno ujafikia mwisho unatoa maamuzi. Huo ni uvivu wa kufikiri.
Sijali umwamini Mungu usimwamini au mwingine yoyote, nakueleza kuwa hukumu hutoa Mungu na si binadamu!
 
Hivi ni wapi kwenye biblia imeandikwa Yusufu alikuwa Waziri Mkuu?
Hiyo ni tafsiri tuu kuelezea cheo, Maake yeye ndo alikuwa mtendaji mkuu baada ya mfalme, baada ya hasimu wake kuuwawa na Yusufu kupandishwa cheo kuwa ndo mtendaji Mkuu baada ya Mfalme. Hivyo tafsri, kuwezesha watu kujua cheo chake! Unachotakiwa ni kujiongeza! Si kila neno utafuniwe.
 
Magufuli sio wa kutetea popote pale, watu waliteseka na bado mengi hayajulikana.
Ok, sasa unavyo mhukumu umepata faida gani! Zaidi unamkosea Mungu alie sema usihukumu na we ukaja hukumiwa! Watu mnashindana na marehemu, sijawahi ona akili kama hii nchi yoyote!
Ni kujifariji kusiko na fikra!
 
Kwa hiyo Mungu ndiyo aliagiza mfanye dhuruma kwenye Taifa ikiwemo kupora uchaguzi, kuteka, kutesa na kuua!

Huyo Mungu wenu ni wa kipekee sana.
 
Kuna watu awafai kuwepo kwenye Jamii iliyostaarabika inatakiwa waondolewe vibaka,wezi, wachawi, waganga, dikteta. hili kundi ndo chanzo cha shida zote kwenye Jamii.
Wakala wa shetani anapokufa sisi ufurahi
 
Kifo ni tukio la kiasili. Katika imani kadhaa za kidini zina elezea kifo kilitokea baada ya Adamu na Hawa (Eva) kwenda kinyume na mapenzi ya muumba wao (MUNGU). Ndipo Mungu alitamka kuwa tutakufa, au kurejea katika mavumbi.

Binadamu wa kwanza kufa alikuwa Abeli. Ambaye aliuliwa na kakaye aitwae Kaini. Kaini japo alimuuwa Abeli, bado Mungu alimlinda Kaini na hata akasema atakae muuwa kaini basi atalaaniwa. Hivyo Mungu alimpeleka Kaini nchi ya mbali. Hii yote kumuepusha na kumlinda na mabaya. Mungu alifanya haya yote japo Kaini alikuwa na dhambi ya kumuuwa nduguye.

Mungu utazama tofauti, na macho ya binadamu. Na Mungu ndiye mwenye uweza wa kuhukumu. Siku hizi Tanzania hii kumezuka, tabia ambayo inaonesha watu kufurahia kifo au vifo vya watu wengine. Na kama walikuwa hawampendi huyo mtu au watu; ndo watazusha mengi. Wabaya wake watajifanya wao ni mungu (Mungu), watahukumu, watasema huyu alifanya mabaya ndo maana kafa.

Watajiona wao waliobaki ndo wajanja, hawana makosa au dhambi mbele ya Mungu. Najiuliza hivi kuna mahala popote pale iwe katika misaafu au maandiko yoyote ya kidini na imani zinginezo, pana sema mtu anae kufa mapema au kabla ya wenzie ana dhambi na Mungu kaamua kumkomoa?

Nachojua Mungu alisema tutakufa, hakuna atakaeishi milele hapa duniani. Ndo maana watu ufa wakiwa watoto wachanga, wakiwa vijana, wakiwa wazee, na hata watoto wengine ufia tumboni mwa mama zao kabla ya kuzaliwa.

Tukidai kufa mapema ni kukomolewa na Mungu, ebu tuangalie, hawa mitume wetu, walikufa bado wakiwa vijana, na walikuwa na maadui wengi, hawakupendwa. Yesu kristo aliishi miaka isiyozidi thelathini na tatu. Na alianza kazi ya kuhubiri akiwa na miaka thelathini tu. Vile vile kwa mtume Muhamad S.W.A alikufa mapema. Si hao tu ni wengi!

Hivyo kifo ni asili. Nachoamini kila mtu anakusudi la kuwepo duniani. Na pia ana muda wake wa kuishi. Haijalishi ni miaka mingapi. Muda ukifika Mungu ndo mwamuzi wa yote, uondoke au aseme bado ubaki.

Katika kila jambo Mungu anamakusudi yake. Laweza kuwa baya au zuri, lakini Mungu anatazama tofauti na tunavyotazama sisi wanadamu.

Kikubwa tusijipe kazi ya Mungu ikawa kazi yetu. Tusijipe kuhukumu kwani hukumu ya maisha yetu utolewa na Mungu. Usihukumu usije hukumiwa.

Nimeongea haya yote ni kutokana na watu wengi, wapinzani na wana CCM kuonekana kumhukumu alie kuwa Rais wa Tanzania, J.P. Magufuli na hata kumzodoa kuwa kafa mapema, yako wapi, kuonesha tu Mungu ati kamuondoa kwa mabaya yake. Nilishangaa hata Mchungaji mmoja anajiita mzee wa upako kuongea kama vile nae anaonesha kufa kwa magufuli ni kama adhabu, eti kisa Lowasa hakuchaguliwa Urais na kuwataka watu wakamuombe Msamaha Lowasa.

Mimi niseme kwa maandiko viongozi wote wakuu wa nchi uwekwa na Mungu. Mungu angeamua Lowasa kuwa Rais angekuwa tu. Mchungaji kasahau maandiko anatumia akili za kibinadamu. Kufa kwa Magufuli si kwamba Mungu hakutaka Magufuli awe Rais, la asha. Mungu hutenda kwa wakati wake.

Jiulize katika maandiko tunaambiwa kuwa Yusufu aliuzwa utumwani na nduguze, bado huyo Yusufu akafungwa gerezani. Lakini cha ajabu akaja kuwa ndiye waziri mkuu wa nchi. Hata nduguze walipojihisi atalipiza kisasi kwa kuwafanyia mabaya, aliwaambia. Mlikusudia mabaya kwangu, lakini katika hayo mabaya Mungu alikusudia mema ili nije niwaokoe katika baa la njaa.

Mungu uona mbali zaid ya binadamu. hatujui ni kwanini Mungu aliepusha Lowasa asiwe Rais japo ilitumika njia mbaya au nzuri, lakini Mungu anakuwa na makusudi yake. Mchungaji katafakari neno la Mungu ndo utoe tamko. Hakuna lifanyikalo duniani bila Mungu kuridhia. Mungu huyo aliruhusu Ayubu apate mateso, akaruhusu watoto wake Ayubu kufa na hata mali kuharibika na kupotea lakini alikuwa na kusudi. Kifo cha Magufuli kinakusudi liwe baya au zuri ila watanzania tutajifunza kutokana na hicho kifo siku moja. Kikubwa tusijichukulie mamlaka ya kuhukumu na kusema kafa kwa sababu alikuwa katiri na kadharika. Mbona Mungu alimlinda Kaini japo alikuwa muuwaji?

Hivi kazi yetu ni kuhukumu, kwani tuliobaki hatutakufa? wangapi tumefiwa na ndugu na wazazi, je kutangulia kwao ni kwamba walitenda mabaya Mungu kawahukumu? Kwa uzoefu wa haraka tu mara nyingi watu wema hawadumu? Iwapo hadi sasa unaishi lazima ujiulize, unatakiwa kulifanyia nini Taifa lako la Tanzania, na familia yako. Si kushambulia marehemu, na kujifanya wewe ni mungu unahukumu. Leo hata viongozi wetu utasikia, oooh! Magufuli hakutenda haki, alikuwa kiongozi mbaya, alikuwa muuwaji, alitisha, hakuwa na demokrasia!

Hivi ninyi viongozi mnao sema haya si mlikuwa nae ktk uongozi wa serikali? Kwanini amkumwambia wakati huo akiwa hai kuwa ni kiongozi mbaya.

Nacho jua Magufuli alikubali kukosolewa. Naibu Waziri wa afya kipindi hicho alimkosoa kuhusu matumizi ya kujifukiza. Akamwondoa katika nafasi. Lakini baadae alimrejesha ktk wizara tofauti.

Leo wanao mkosoa magufuli haohao, wanapinga Mhe. Rais Samia kukosolewa. Wakati Rais alidai kuwepo uhuru wa kukosoa. Lakini chama chake na Bunge Wanataka asikosolewe, tumsifie hata kwa yale yasio sifiwa. Wakati wanadai wao ni wanademokrasia. Ukikosoa unahesabika msaliti, Bunge litakuita kwenye Kamati. Chama kitakaa kukuita kikuhoji kwa nini huko kinyume na Rais. Chama kinachoongozwa na mwenyekiti ambae ni Rais alie ruhusu kokosolewa.

Mungu hapendi wafitini na watu waongo, wenye roho za usaliti. Viongozi mjitafakari. Na msijione ninyi hamta kufa. Kifo kipo akijali madaraka yako. Hakuna atakae ishi milele. Kuwepo kwako pengine Mungu anataka utimize mambo fulani. Ghazabu ya Mungu ni kubwa tusihukumu tukaja hukumiwa. Magufuli kaondoka kamaliza yake. Alifanya kwa nafasi yake na kwa staili yake. Watu wote hatufanani.

Tusijione sisi ni bora kwakuwa tu watu wanatuchekea na kutusifia. Tukachekelea na kuota kiburi kuona tuko sahihi na hatukosei! Pamoja na yote Magufuli aliwapenda watanzania. Hakuwahi kusema waondoke wakaishi Burundi.

Leo kauli hiyo inaongewa na kiongozi aliepewa dhamana na watanzania. Viongozi wamejiona wako juu ya sheria, wanauwezo wa kusema chochote. Viongozi wamekuwa na dharau. Wanajiona nchi ni yao. Hata wananchi kulalamika hawaoni haja ya kuomba msamaha.

Hata kiongozi wa nchi hawakanyi anawaacha je naye kafurahishwa na hayo maneno? Je kawatuma?
Harafu hawa hawa ndo wanasema watakuwa wapole na kuwabembeleza wananchi kuliko JPM ambaye kapewa mabaya yote.
Tukumbuke kutangulia kufa si dhambi. Na ukibakia si ujanja wa kufanya kutukana waliotangulia. Bali chukua muda wa kujitafakari.

Mungu alimlinda Kaini japo alikuwa muuwaji wa nduguye. Mungu ndiye mwenye kuhukumu. Na ndiye ajuaye mwisho wa maisha yetu. Jiulize hapo ulipo matendo uyafanyao ktk vificho au wazi, je ni mema? Je wewe ni msafi zaidi ya waliotangulia kufa?

Je, wajua kifo chako kitakuwaje? Lini utakufa? Je utakufa ukiwa na umri gani? Je alie kutangulia kafa akiwa na miaka mingapi?
Si ujanja wala umaarufu kutukana marehemu, au kutafuta umaarufu ati unajilinganisha na marehemu. Huyo kesha maliza wakati wake hayupo tena. Tuache kashfa hatujui kesho yetu. Tanzania ya leo imekuwa na siasa za kujipendekeza, sifa za kijinga, badala ya kufikiria maendeleo ya kweli. Walio tangulia tuwaache, tujenge nchi.
Mwambieni Gwajima amfufuwe, yeye si Askofu wa Ufufuo na uzima?

Tumechoka makelele yenu, Dikteta is died and buried. Fullstop.
 
Ok, sasa unavyo mhukumu umepata faida gani! Zaidi unamkosea Mungu alie sema usihukumu na we ukaja hukumiwa! Watu mnashindana na marehemu, sijawahi ona akili kama hii nchi yoyote!
Ni kujifariji kusiko na fikra!
Tunataka tu iwe fundisho kwa viongozi wetu kwamba wao sio miungu na ipo siku watu watakuwa huru kuongea. Ukijua maovu ya bwana huyu hutamuonea huruma yoyote, aliharibu mno, hayo lazima tuyazungumze akiwa hai au mfu.
 
Nimekwambia soma mada nzima, unataka mimi ndo nikusomee! watu wengine wa ajabu! Pia kutokuwa na dini sio utenda maovu. Zamani watu wengi hawakuwa na dini, lakini walikuwa na hofu ya kuhukumu. Tazama nchi za Ulaya ambazo haziamini hakuna Mungu, uwezi ukakuta mtu ana hukumu mwezie alokufa.
Kwa nature ya binadamu anahofu, hata kama haamini Mungu lakini kuna nguvu nyingine anayo amini.
Na hakuna sheria inayozuia mtu asiongelee kile anachokiamini, mimi naamini juu ya Mungu anaishi, na alie umba mbingu na dunia. Nitamwelezea popote pale, siogopi chochote! Naamini anaukuu wa kuonesha uwezo na nguvu zake!
Hivi unadhani mimi natishwa, au katika mada mtu kuokoteza sentensi na kuanza mashambulizi. Kajipange! Mtu ambae anauelewa usoma mada nzima, si unaokoteleza kaneno ujafikia mwisho unatoa maamuzi. Huo ni uvivu wa kufikiri.
Sijali umwamini Mungu usimwamini au mwingine yoyote, nakueleza kuwa hukumu hutoa Mungu na si binadamu!
Sentensi ipi imeokotezwa mkuu? Wewe ulikuwa unamjibu mtu kuwa Mungu ndo hupanga kifo. Unajichanganya sana kwa maelezo yako.

Huyo shetani bora alivyokufa, kila mtu alifurahi including me. Sijali nitakufaje but atleast nimeshuhudia kafa, yeye hatashuhudia nikifa.
 
Usichukue sentensi moja soma mada nzima uangalie nini kimefafanuliwa ndani. Nimetoa mifano ya Ayubu, na familia yake. Vifo vya watoto wa Ayubu ni shetani alisababisha . Ila Mungui alilidhia. Lakini alimkataza shetani asimuuwe Ayubu.
Ebu so mada yote uelewe !
"Takeni sana kuwa na amani na watu wote na huo utakatifu ambao hakuna atayemuona baba asipokuwa nao" mkuu koleza kwa wino mweusi huo mstari wa kwanza, amani na watu wote. Ilmradi hukuthubutu kufungua mdomo wakati haya yanatendeka acha historia iwe mwalimu.
 
Back
Top Bottom