Hayati Dkt. Magufuli ndiye Rais aliyefaa kuiongoza Tanzania

CHADEMA na Msogagang wakiona Jina JPM hata wakiwa chooni hutoka haraka kukabiliana na Uzi huo.

Haya ukiwauliza Kama Jiwe hakufaa,Nani Sasa angefafaa basi anayejali demokrasia?
Wataseme Mbowe🤣🤣🤣🤣
Mwenyekiti wa maisha.
 
Alikuwa hafai uraisi yule labda uwaziri angekuwa bado yupo hii nchi sijui ingeenda wapi?
 

Hoja dhaifu sana:-

1. Kila mtu ana haki ya kuishi ,Mchungaji akipoteza kondoo mmoja atawaacha wale 99 na kwenda kumtafuta mmoja ,hii ina maana gani? Roho moja iliyopotea ina thamani kubwa kuzidi hata hao 99 walioko hai maana kila mtu ana haki ya kuishi ,Enzi za Jiwe roho nyingi zilipotea kwenye uso wa dunia na watu wasiojulikana ,wapi Kanguye? Wapi Gwanda? Wapi Rwajabe? Wapi Ben saa8? Nani aliyemmininia risasi 38 Lissu?

2.Sasa unamtolea mfano january? january anakaa Prime area ambapo hawapati madhira ya umeme kukatika maana wakubwa wengi wanakaa huko,umeme ulikuwa unakatika sana hata enzi za jiwe! Umeme haupaswi kukatika unless kuna fault ,sasa unataka kuniambia kipindi cha JIWE kulikuwa hakuna Fault?

3.Majengo mengi yapo kwenye hifadhi ya barabara hata ikulu ,NBC HQ ,New Africa ,Southern Sun ,Holiday Inn ,Aghakhan ,Mwalim House,PPF Tower ,Peugeot House ,Barclay HQ mbona hayabomolewi?
 
Kinachoniuma roho wahindi wameanza kuibuka tena aloo,jamaa aliwapiga pin kwa kweli.

Sasa hivi wataanza tena kutuibia na kuweka mapesa wanayovuna kwenye acc zao nje ya nchi,sijui kama nssf watatupelekea tena hela zetu maweee twafwaa.
Mpaka unaibiwa wewe unakuwa wapi?. Mentality za uvivu na ulalamishi.
 
Magufuri kashakufa homeboy hebu tupe mda na sisi tupumzike kidogo.Kwani Magufuri kaanza siasa mda gani na kabla ya kuwa rais alikuwa katika siasa kipindi gani? Mtu kahudumu kwenye siasa kwa miaka zaidi ya 20, kwahiyo unataka kusema kipindi hicho matatizo haya uliyotaja hayakuepo?ukweli ni kwamba yalikuwepo na hakuna chochote alichokuwa akifanya zaidi tu aliweza kusimamia ujenzi wa barabara mbovu basi.

Kingine matatizo ya wananchi anayetatua ni rais?kama ndio,basi kuna swali jingine la kizushi.Kwani rais ndio anayekata maji na umeme?The fact is,the president does lead the country.They(he/she) are not there to fix any mans' ignorance.Citizens need to fix their own problems.Kwahiyo mambo ya sijui umeme umekatika wananchi ndio inabidi kuwajibika kwa maana ndio uchaguzi walioufanya
 
Mama tunae hadi 2030.
 
Acha Wenge, Mbona hausemi siku hizi watu wasiojulikana hawapo?

Enzi za Magu umeme ulikuwa unakatika tu labda wewe ulikuwa unakaa line ya ikulu.

Jengo la Taneco alibomoa ili iweje? Mbona hausemi alikuwa na Roho Mbaya?
Nenda Lindi wapo wasiojulikana
 
Kwani wanavyoiba nyie mnakuwa wapi?,
Kusema wahindi wanatuibia ni akili za kimaskini. Wanayo nidhamu ya utendaji kazi. Mswahili akipata pesa anakwenda disco na kuanza kurusha pesa hewani kama Diamond.

Wakati huo anao ndugu wengi tu wamezungukwa na umaskini wa kutupwa.
 
Kusema wahindi wanatuibia ni akili za kimaskini. Wanayo nidhamu ya utendaji kazi. Mswahili akipata pesa anakwenda disco na kuanza kurusha pesa hewani kama Diamond.

Wakati huo anao ndugu wengi tu wamezungukwa na umaskini wa kutupwa.
Sijakuelewa gabachori,mi nazungumzia ukwepaji Wa kodi Wa wahindi, kwani huko disco unaloendaga hukutanagi na wahindi wakijirusha?.
 
Sijakuelewa gabachori,mi nazungumzia ukwepaji Wa kodi Wa wahindi, kwani huko disco unaloendaga hukutanagi na wahindi wakijirusha?.
Mpaka wakwepe kodi maana yake ujinga unaanzia kwetu sisi waswahili. Jiulize na utafakari kwa kina.
 
Mpaka wakwepe kodi maana yake ujinga unaanzia kwetu sisi waswahili. Jiulize na utafakari kwa kina.
Usituonee sisi waswahili boss hayo malalamiko unayapeleka kwenye idara ya sirikali ukamshinda gabachori kesu zaidi ya wewe kugeuziwa kipande.

Laumu serikali na mamlaka zake.
 
Kule Afrika kusini makaburu wamefanya makubwa kuliko hayo lakini kwa ukatili wao walikataliwa sio tu na wananchi wa Afrika kusini bali dunia nzima kwahiyo hata hapa kwetu mtu mwenye chembechembe za ukaburu hatumtaki hata angefanya maendeleo gani.
Lakini kwa matatizo ya sasa ya maji kwa Dar na Pwani ni kutokana kupungua kwa kina cha maji kwenye mto Ruvu ambao ndio tegemeo la Dawasa katika upatikanaji wa maji wanayosambaza kwa wananchi wanaowahudumia je sasa unataka wakakojoe huko kwenye mto ili kina kiongezeke? Na swala la umeme waziri tayari ametoa ufafanuzi kwamba kwa muda mrefu kutokana na nidhamu ya woga TANESCO hawajakarabati miundombinu yao na hiyo sasa ndio inasababisha umeme kukatika kwa sababu imeanza kuchoka hivyo nao hivi sasa wameanza kukarabati miundombinu yao ya kuzalisha na kusambaza umeme na bila shaka kazi ikikamilika hali ya umeme itarudi kuwa ya kawaida.
 
Tutolee ukichaa wako hapa. Mungu kamchukua kwasababu zake. Rais wa hovyo kuwahi kutokea Tanzania.
 
endelea na ndoto
 
Kama kuna watu wanatufanya Tanzania tudharauliwe ni pamoja na wewe Hziyech22. Utawala wa Magufuli ulikuwa ni utawala usiozingatia utawala bora, utawala wa sheria, kubana uhuru wa kujieleza na uuaji kupitia kundi la WASIOJULIKANA.

Magufuli alikuwa MWONGO sana na ndiyo maana akawapata na kuwashawishi watu kama wewe mtoa mada ambao hamna vyanzo vingine vya taarifa zaidi ya TBC1.

HATUTAKI kuingozwa na KICHAA tena.
 
Tulia basi mkuu. Magufuli si yupo huko aliko na huko kuna Watanzania wametangulia mbele ya Haki? Basi atakuwa anawaongoza huko...!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…