Hayati Lowassa alivyomponza Kikwete akatimuliwa Msasani kwa kufokewa na Mwalimu Nyerere

 
Kweli urafiki wa wanga haudumu, nani angeamini wanamtandao wangepishana pakubwa mwaka 2015?.....yote yamebaki historia Sasa.

Tungoje mitandao mipya kuelekea 2025.
 
Ongezea na mkapa akaja kuwa fisadi papa
Kwa hiyo Nyerere Hana haki ya kutambua nani malaika na Nani shetani
Interesting. Ukisoma mada kama hii unaona kuwa CCM kweli ni chanzo cha matatizo ya nchi hii. Nyerere baada ya kuacha katiba mbovu na mfumo m’bovu wa uongozi bado aliweka mkono kuchagua na kuendorse mafisadi kuwa viongozi.

Tena huyo BWM aliyemuita “Mr. Clean” alimliza mapema kabisa kwa kuuza NBC kwa “makaburu” kwa bei chee yeye akiwa hai na kushuhudia. Malalamiko yake kupinga mnada ule yalipuuzwa kabisa. Alipofariki tu biashara ya asset za serikali ikapamba moto bila hata vigezo vya haja. Viwanda vikaishia kuwa magodown. Wanunuzi wengi wakiwa madalali wa real estate badala ya wawekezaji makini.

Leo hii ukiambiwa Lowasa alikataliwa kwa sababu ya kuwa na hela nyingi au fisadi, unajiuliza huu ni mzaha au nini? Kiongozi gani wa CCM baada ya Nyerere ana rekodi safi ya kujivunia ya kutokuwa mwizi au fisadi? Angalau AH Mwinyi Nyerere alimtambua kiasi lakini bado akamgonga na “kiongozi unaweza wewe binafsi kuwa msafi. Lakini sharti uwe na uwezo wa kuwaambia ndugu na rafiki zako kwa kauli isiyo na shaka kuwa Ikulu ni mahali patakatifu”.
 
Mzee Mohamed Said unazo hizi taarifa ?
 
Aisee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahaha asante kwa hii kumbukizi mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi na hii report ya Mwakyembe ndio ilipelekea kupewa sumu sio

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilicho gundua kuna kitu kimemkwaza jk , kwenye msiba wa El, jk anaona kuna watu wanamchafua Huku wakimsifu El , bila kujua El ni jambazi Tu 😂.

Jk kwangu ni kiongozi Bora kabisa, alijali wananchi, shida ni mtandao ndio ulikuwa ukimtia aibu
 
Salute
 
Sho...
Nimesoma hayo hapo juu kuhusu Prof. Malima na ningependa na mimi niseme machache niyajuayo kuhusu Prof. Malima.

Katika Bunge mwezi June 1994 Prof. Malima akiwa Waziri wa Fedha alileta mswada kuwa misamaha yote ya kodi iwe chini ya Waziri wa Fedha badala ya kuiachia iwe katika mamlaka nyingi tofauti.

Maadui zake ndani ya Bunge wakalalamika kuwa Prof. Malima alikuwa anataka kujijengea himaya.

(Kwa nini Prof. Malima alikuwa na maadui ni mada ya kujitegemea).

Hata hivyo fikra zilitulia na mantiki ikatawala kuwa hilo ni jambo jema na mswada ule ukapita.

Baada ya mwezi mmoja kupita wakati Prof. Malima yuko nje ya nchi Baraza la Mawaziri likaitishwa kwa shinikizo la Waziri Mkuu John Malecela akiungwa mkono na mawaziri wanne wakongwe nia ikiwa kugeuza suala la misamaha ya kodi uliopitishwa mwezi mmoja tu uliopita.

Prof. Malima aliporejea nchini na kukuta kuwa uamuzi wa Bunge kuhusu misamaha ya kodi umepinduliwa na Bunge, Prof. Malima alimtahadharisha Rais Ali Hassan Mwinyi kuhusu matokeo ya kwenda kinyume na maamuzi ya Bunge na matakwa ya wahisani.

Rais akaitisha Baraza la Mawaziri lililokaa kwa siku nne.

Prof. Malima alihimili hoja zote kutoka kwa maadui zake katika serikali akitetea uamuzi wa Bunge.

Baada ya siku nne Baraza la Mawaziri lilirejea nyuma katika uamuzi wa Bunge.

Maadui zake waliumia sana na chuki yao dhidi yake ikazidi.

Hayo yote ya kuwa Prof. Malima alikuwa fisadi si kweli.

Prof. Malima hakuwa na mali nimemuona kwa karibu sana nyumbani kwake jirani na Victoria na nimeiona nyumba yake Kisarawe siku ya mazishi yake.

Prof. Malima hakuwa na mali na kama alivyokuwa akipenda kusema katika uhai wake, ‘’Hakula cha mtu.’’

Ametajwa hapa Kikwete kuwa alipewa nafasi ya Waziri wa Fedha badala ya Prof. Malima lakini mwandishi kaishia hapo tu.

Inataka ushughulishe bongo lako ujiulize kwa nini Kikwete?

Yapo mengi.

Kwa nini hakuyasema mengine na ni muhimu katika historia ya Prof. Malima?

Hakuyasema inawezekana kwa kuwa hayajui.


 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…