Hayati Lowassa alivyomponza Kikwete akatimuliwa Msasani kwa kufokewa na Mwalimu Nyerere

Hayati Lowassa alivyomponza Kikwete akatimuliwa Msasani kwa kufokewa na Mwalimu Nyerere

Mwaka 1995 Jakaya Kikwete akijifanya ni masikini na Edward Lowassa akinukia noti,walisindikizana kychukua fomu za kugombea urais,nyuma yao akiwepo king maker Rostam Aziz na Samuel Sitta,
Lowassa aliamua kukodi ndege binafsi chini ya captain Minje baba yake Lilian,walizunguka Tanzania nzima kusaka wadhamini,walikuwa na miaka 42 kwa 45 mtawalia,
Wakajiita Boys II Men.
Aliyekodi ndege ni Lowassa Jk alipewa lift tu,makubaliano ni kuwa yeyote ambaye angepita amteue mwenzake kuwa wqziri mkuu ,na baada ya miaka kumi huyo waziri mkuu agombee urais,hapa ni kama Putin na medinedev wanavyofanyaga.

Taarifa zikamfikia mwalimu Nyerere kuwa kijana Lowassa anagawa pesa kama njugu na amekodi ndege,na akaambiwa anaambatana na mtoto wa rafiki yake marehemu Mrisho Kikwete ,yaani Jakaya .
Mwalimu akamuita Jakaya Msasani ili kumuonya akae mbali na EL,
JK bila kutambua akampa lift EL kwenye gari aina ya Ssang yong Musso mpaka msasani.
Taarifa zikamfikia mwalimu kuwa Jk kaja na EL,mwalimu akajifanya anatoka nje kwa hasira na kumfokea kuwa amechelewa appointnent atoweke haraka mahali hapo kufumba na kufumbua.Jk kwa shingo upande akaondoka bila kujua sababu,
Mwalimu akidhani JK amegundua kosa lake,kumbe wapi,kwenye vikao vya mchujo Jk uso kwa uso tena na mwalimu,na akaulizwa if you brcome a president who gonna be your prime minister,JK akayakoroka kwa kusema Edward Lowassa,mwalimu akamwambia asante kwa kushiriki,jina la JK likakatwa kibabe na akapachikwa Benjamin Mkapa.
Matumizi makubwa ya pesa katika kusaka madaraka yalimponza EL.
.....,....Itaendelea
Kyai kya rangi hiki
 
Sasa kama ni hivyo mbona walikuja kuhitilafiana kiasi kile, mbaya, kwa nini yule hakuonyesha shukurani aliye kutangulia kwa vile alipita kwa nasibu kiasi hiko.
Kimsingi Mwendazake na jeuri yake yote hajawahi tamka hadharani kutofautiana hata matendo japo nahisi alikuwa na wasiwasi wa kwamba yeye ni Rais lakini ni kama system inampa Baadhi ya taarifa Msoga.

Ndio hapo Mwendazake akaanza Kuunda system yake ambayo imeishia njiani 🤣🤣

Refer Kabila vs Thisekedi Huwa napenda kutumia hii mifano
 
Na unaweza kukumbuka Kauli ya JK kwamba mlisema Mimi mpole nimewaletea chuma.

Kiufupi Urais wa JPM ni kama alivyopata Thisekedi baada ya kuona first 11 wamezingua akaona hapa atafute super sub ambae atakuoa chama na atawapelekea moto Wapinzani.

Sema super sub alianza kuita sharubu sana 😆😆😆😆😆😆🤣🤣🤣🤣🤣

Ndio maana Suk gang Huwa hawamkubaki kabisa JK wanahisia aliwakatisha ulaji 😁😁

System ilisema tunamtaka huyu, zike ziara na waziri wa ujenzi na coverage + ulinzia haikuwa kawaida, ziliashiria jambo.

Hata UPM, toka mwanzo ulikuwa na jina kutoka kwa system na sio EL, Mkwere akashupaza shingo akaenda na swaiba wake baadaye ikawa historia nyingine.
 
Nyerere alivyozima hoja ya Serikali tatu chini ya G55 ambayo ilishamshinda Mwinyi na Malecela alikuwa Rais?

Nyerere alivyoratibu kukatwa kwa jina la Malecela na Lowassa 1995 alikuwa ni Chairman wa CCM?
Baada ya Jk kumshinda Mkapa na Msuya kabla matokeo kutangazwa akaibuka na hoja ya kura zirudiwe kati ya Mkapa na Jk alikuwa Chairma wa Ccm?

Vijana wengi hamuwezi kujua nguvu aliyokuwa nayo Kambarage hadi anaondoka Duniani

JKs wote wawili walikuwa na katabia flani hivi

wanaweza wakalia hadharani kumbe wanacheka na wanaweza wakacheka hadharani kumbe wanalia
Tabia za watu wa system hizo,humuoni Mkaonda anavyoigiza huko makanisani analia sijui Machozi na blaa blaa kama hizo za kumanipulate wenye akili ndogo.
 
Mengi sana...na yapo yaliyomuumiza sana lakini akavumilia na hakuwa na kisasi. Jakaya ni mstahimilivu sana. Amepitia mengi na ameyatatua kwa busara.
Na ndio maana Huwa anamsifi Samia kwa kifua.Kimsingi Urais unahitaji mtu mwenye akili ya mbali na stable wa hisia sio unapayuka kienyeji enyeji kama yule Jamaa mwingine 😆😆
 
Yes hii kauli Magufuli alishaisema sana.
Huyo ni mfuasi wa kikwete huwa anamfanya kikwete kama dude fulani la kutisha wakati ukweli ni kwamba hakuna raisi wa ovyo kumzidi kikwete na huyu wa leo...magufuli alishawahi kuongea kuwa anamshukuru kikwete kwa kumwachia uraisi na anamshukuru mno mkapa kwa kumfanya kuwa raisi
 
System ilisema tunamtaka huyu, zike ziara na waziri wa ujenzi na coverage + ulinzia haikuwa kawaida, ziliashiria jambo.

Hata UPM, toka mwanzo ulikuwa na jina kutoka kwa system na sio EL, Mkwere akashupaza shingo akaenda na swaiba wake baadaye ikawa historia nyingine.
Tusichosane, system zipo duniani SI Nchi maskini Kama Tanzania.... Hapa ni wizi wa kura tu...... Ujinga tu
 
Na unaweza kukumbuka Kauli ya JK kwamba mlisema Mimi mpole nimewaletea chuma.

Kiufupi Urais wa JPM ni kama alivyopata Thisekedi baada ya kuona first 11 wamezingua akaona hapa atafute super sub ambae atakuoa chama na atawapelekea moto Wapinzani.

Sema super sub alianza kuita sharubu sana 😆😆😆😆😆😆🤣🤣🤣🤣🤣

Ndio maana Suk gang Huwa hawamkubaki kabisa JK wanahisia aliwakatisha ulaji 😁😁
Hizo ni kauli tu unadhani mwanasiasa atakosa cha kuongea kwa kinywa chake magufuli alimshukuru mzee mkapa kwa kumfanya kuwa raisi unadhani kauli hiyo inamaana gani?
 
Acha uongo, Freeman Mbowe na Lema hawakuwa wabunge 2005-2010..

Sasa huko walikoshadadia ni wapi??
Kushadadia ni kuwa Wabunge ?

au wakati unasoma tayari ulikuwa na mawazo yako kichwani ?

Wakati Lowassa na Rostam wanatangazwa rasmi viwanja vya Mwembe Yanga kama mafisadi Papa, Chairman wa Chadema alikuwa Kikwete?

Kamati kuu ya Chadema iliyoridhia ku upload orodha ya Mafisadi Papa na Jina la Lowassa likiwemo iliongozwa na Salma Kikwete ?

Tanzania Daima gazeti binafsi la Freeman lilipokuwa linashadadia ufisadi wa Rostam na Lowassa ulikuwa bado akili hazijakomaa ?
 
Hizo ni kauli tu unadhani mwanasiasa atakosa cha kuongea kwa kinywa chake magufuli alimshukuru mzee mkapa kwa kumfanya kuwa raisi unadhani kauli hiyo inamaana gani?
Lazima amshukuru Kwa ndio alimuibua na kimfanya aonekane ila JK ndio alimpa Urais kama super sub in case of anything na ikawa
 
Kushadadia ni kuwa Wabunge ?

au wakati unasoma tayari ulikuwa na mawazo yako kichwani ?

Wakati Lowassa na Rostam wanatangazwa rasmi viwanja vya Mwembe Yanga kama mafisadi Papa, Chairman wa Chadema alikuwa Kikwete?

Kamati kuu ya Chadema iliyoridhia ku upload orodha ya Mafisadi Papa na Jina la Lowassa likiwemo iliongozwa na Salma Kikwete ?

Tanzania Daima gazeti binafsi la Freeman lilipokuwa linashadadia ufisadi wa Rostam na Lowassa ulikuwa bado akili hazijakomaa ?
Mbona unajibu kwa jazba?
 
Mwaka 1995 Jakaya Kikwete akijifanya ni masikini na Edward Lowassa akinukia noti,walisindikizana kychukua fomu za kugombea urais,nyuma yao akiwepo king maker Rostam Aziz na Samuel Sitta,
Lowassa aliamua kukodi ndege binafsi chini ya captain Minje baba yake Lilian,walizunguka Tanzania nzima kusaka wadhamini,walikuwa na miaka 42 kwa 45 mtawalia,
Wakajiita Boys II Men.
Aliyekodi ndege ni Lowassa Jk alipewa lift tu,makubaliano ni kuwa yeyote ambaye angepita amteue mwenzake kuwa wqziri mkuu ,na baada ya miaka kumi huyo waziri mkuu agombee urais,hapa ni kama Putin na medinedev wanavyofanyaga.

Taarifa zikamfikia mwalimu Nyerere kuwa kijana Lowassa anagawa pesa kama njugu na amekodi ndege,na akaambiwa anaambatana na mtoto wa rafiki yake marehemu Mrisho Kikwete ,yaani Jakaya .
Mwalimu akamuita Jakaya Msasani ili kumuonya akae mbali na EL,
JK bila kutambua akampa lift EL kwenye gari aina ya Ssang yong Musso mpaka msasani.
Taarifa zikamfikia mwalimu kuwa Jk kaja na EL,mwalimu akajifanya anatoka nje kwa hasira na kumfokea kuwa amechelewa appointnent atoweke haraka mahali hapo kufumba na kufumbua.Jk kwa shingo upande akaondoka bila kujua sababu,
Mwalimu akidhani JK amegundua kosa lake,kumbe wapi,kwenye vikao vya mchujo Jk uso kwa uso tena na mwalimu,na akaulizwa if you brcome a president who gonna be your prime minister,JK akayakoroka kwa kusema Edward Lowassa,mwalimu akamwambia asante kwa kushiriki,jina la JK likakatwa kibabe na akapachikwa Benjamin Mkapa.
Matumizi makubwa ya pesa katika kusaka madaraka yalimponza EL.
.....,....Itaendelea
We mwongo, JK aliingia mpk 3 bora
 
Mwambieni JK atuandikie Kitabu kabla ya Kufa tujifunze mbinu za medani za Vitengo.

Pili asije kukosea kutuondolea Samia [emoji16][emoji16]
Kitabu kimeshaandikwa muds mrefu huko Jijini New York ila mara kwa mara anaahirisha kukizindua kwa sababu kadhaa wa kadhaa na hasa sababu za kisiasa

Uongozi Institute walihusika kwa namna fulani kufanya review
 
Huu uongo wa kitoto sana.BMW alikuwa ni kipenzi cha mwalimu kwa urais wa JMT baada ya Dr Salim,hiyo sababu dhahania haiwezi kutosha kumuondoa BMW moyoni mwa mchonga
Wakati Edo na JK wanaangaika kutafuta wazamini huko,kumbe Mwalimu alisha make up his mind kwa Ben, ni kama uchaguzi wa 2015 Ben nae alifanya kama Mwalimu alivyo fanya 95!!
 
Uhusika wa kikwete kwenye Richmond ni upi?
kumzuia Dr Ibrahim Msabah aliekuwa Waziri wa Nishati na Mbunge wa Kibaha ku approve advance payment ya 10 Billion kwa Kampuni feki ya Richmond ambayo ilikuwa ya mwisho kwenye Procurement process lakini Management ya Tanesco ikalazimishwa kwa Vimemo iwape Tender

baada ya kupewa Tender wakataka walipwe advance payment hiyo wakati haikuwemo kwny terms of contract

ndipo Mh.Rais akastukia kitu akatumia weledi wake wa kimedani akajua Watu aliowaamini wameanza kumzunguka.

Media zikaanza ku report hiyo kashfa nae akaridhia uchunguzi huru kwa Bunge kuchunguza

Report kabambe ya Uchunguzi ya Dr Harrison Mwakyembe, akisaidiwa na Eng. Stella Manyanya kama Makamu Mwenyekiti pamoja na Wajumbe kina Lucas Selelii Mbunge wa Nzega wa wakati huo wakafanya kazi kubwa na ya kizalendo

matokeo kuletwa Bungeni ikabidi ijadiliwe then watuhumiwa ambao ni Wabunge wajibu hoja

Hoja za Utetezi zilipoanza alisimama Peter Serukamba Mbunge wa Kigoma Mjini kumtetea Lowassa

lowassa akamuomba Spila Sitta amzuie Serukamba na badala yake akatangaza kujiuzulu akafuatia Karamagi then Msabaha

Rostam akiwa Katibu wa Uchumi wakati huo akabadilishwa baada ya muda mfupi

JK hakuwafanyia figisu lolote zaid ya kuwatoa kwny Serikali yake na nongwa ikaanzia hapo
 
Back
Top Bottom