Hayati Magufuli alifanikiwa kutengeneza kundi lililomuamini na kumtii mithili ya wafia Dini

Huwezi kuelewa kama ni mtu unaabudu hela na maslahi binafsi. Wafuasi wa magufuli walikua waomini wa itikadi ya uzalendo, wapenda haki usawa na maendeleo. Kwa hivyo wasingeheshimu mikataba ya kifisadi ya kukandamiza na kunyonya nchi. Pia miongoni mwao walikuepo wasomi waliyojua hakuna mkataba wa kisheria hauna pa kutokea ndio maana wakavunja mikataba ya wapiga dili ambao walipata hasira sana.
 
Alikuwa mtu hatari sana kwa Tanzania yetu na ameharibu nchi kwelikweli!
 
W
Mjinga tu wala hujui maana ya dikteta. Mwenyewe unawaita populist kwa hivyo unajua wanapendwa na wamepigiwa kura kwa wingi. Shida yako kwa aina ya viongozi kama hao kina chavez na magufuli wanaweka maslahi ya umma wa wananchi wao. Wabinafsi, walafi, na wezi dhulumati wa mali ys umma kama wewe lazima wawaite dikteta kufuatisha kiitikio wanachoamrisha wamagharibi.
 
Ushawishi gani aliokuwa nao Magufuli?
 
Kipindi cha utawala wake ilikuwa vigumu kutenganisha mzalendo na mjinga.
Wazalendo ndio waliyompenda, wajinga ndio waliyomchukia. Wajinga walimchukia kwa kufuata mkumbo wa fisadi na wapikaji bila wao kua na sababu kimaslahi kumchukia.
 
Mbowe ameshaju submit kwa mama. Ni mtoto wa.mama period.
 
Sabab ni moja tu. Alikua ni kiongoz wa kwel. Na ndio hicho unachokishangaa. ..
 
Mtu yoyote ambaye hua anaona JPM hakua mtu mzuri, nafanya kuwaza ya kwamba nchi hii hata aongoze YESU au MOHAMMED bado watalaumiwa tu, nchi hii haijawahi kupata Rais mzuri kuzidi JPM, simaanishi wengine hawakufaa isipokua JPM alikua ni Bora kuliko

Na mtu anayemponda utakuta alikuaga ni mwizi wa pesa za umma Kwa namna moja ama nyingine na akakutana na mkono wa chuma wenye kutaka haki kwa wote kama ambavyo alifanya Gaddafi

Gaddafi aliapa kuishi kwenye matenti jangwani mpaka ahakikishe kila mLibya wa mwisho anamiliki nyumba ya kuishi, akaondoa utofauti mkubwa wa kipato na kuondoa Ile hali ya watu wachache kumiliki pesa kuliko Serikali na kusababisha Serikali isitawalike, watu wakafanana kwa kiasi fulani, ila Serikali ikawa na pesa za kutosha na kuweka huduma muhimu karibu zote Kwa Raia wote. Ndivyo JPM alivyokua anaipeleka nchi, lakini majizi machache yalipobanwa ili kutenda haki, yakaanza kulalamika mitandaoni ya kwamba JPM ni dikteta asiyefaa, yakasahau kabisa yalikua yalikwepa Kodi ama kukwapua pesa za Umma.

Binafsi napenda sana Spirit za JPM, Gaddafi, Patrice Lumumba, Saddam Hussein, Putin na wengineo ambao wana uchungu na wananchi

Mtu alishakufa, tena kifo chenye utata kisicho eleweka, lakini bado Kuna watu wanaendelea kugombana na mwili uliolala mauti na kuoza, hii ni aina ya ukichaa kwa watu
 
niliwahi kuwa kwenye hilo kundi la hiyari la kumsifia marehemu. ila baadae nikaacha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…