Hayati Magufuli alifanikiwa kutengeneza kundi lililomuamini na kumtii mithili ya wafia Dini


Hivi ndivyo vitendo vya Magufuli na jeshi lake

 

Kwako JIwe atakuwa mzuri pengine ukilamba asali huku ukijipendekeza

Kiukweli yule mnyama , tunamshukuru Mungu ameondoka.

Hivi ni baadhi ya vitendo vyake na jeshi lake walivyotufanyia. Hatusahau milele

 
Nchi ilizizima Kwa furaha alipokufa watu mabaa yalifunguliwa upyaaaaa na yaliyobakiza wanywaji wawili kufumba na kufumbua kukawa na wateja kama wote Arusha mbeya dar acha kabisa Arusha ngombe na mbuzi walichakaa!
Ma-boda boda yaka randa randa huku na huko..... shangwe nderemo na vifijo.... nyama na bia zikaadimika ghafla, bei zikapanda...Dar wa mama wakacheza "MDUNDIKO"...
 
Kama MBOWE tu, wote sasa hivi mnaimba wimbo mmoja na CCM.

Asali tamu itakuwa ya Tabora siyo ile sukari guru ya kutengeneza.
 
Msiwe mnanikumbusha huyu mtu tafadhali😭
 
Toka umejiunga na JF kazi ya ni kuimba na kuabudu juu ya mbowe.. kwako wewe mbowe hana kosa, hana pungufu.

Mbowe kwako ni malaika, hata kama ni uchawa wa kwako umezidi braza.
Lipi la uongo kuhusu Magufuli uliloliona nimeandika
 
Mtampaka sana matope,ila he will always stand out as o morally superb individual.Tunajua kwamba ninyi wote mnaompaka matope Hayati JPM ni mijizi and very evil individuals.Kila wakati mnazungumza hewa tu,you have virtually failed to substantiate his theft or what you are talking about.Sikuona hata siku moja kwamba Hayati Magufuli alijijengea mazingira ya kuabudiwa.

As to his alleged theft,tumewaomba wanaodai JPM alikuwa mwizi,watuonyeshe mahoteli makubwa aliyojenga nje au ndani ya nchi,majumba ya kifahari aliyojenga nje au hata ndani ya nchi,mashamba makubwa aliyo nayo,biashara kubwa alizonazo popote,watoto aliotajirisha kwa kutumia nafasi yake nk.nk.mmeshindwa.Kwa kuwa wameshindwa Mimi nasemabplease,please,please fungeni makanwa yenu,Watanzania hawawaelewi you look stupid.
 
Ninyi watu mwashangaza sana mmemuita Tundu Lissu kapewa chake na vibuyu vya asali akalambe huko Ubelgiji kwisha habari yake.

Ninyi mlobaki hapa Tanzania mmepewa chenu na vibuyu vikubwa vya asali ambavyo mtavilamba hadi 2025 mmebakia hamna hata cha kusema kimyaa.

Haya yote mnokuja kuandika hapa ni baada ya pale unapokuwa walamba asali yako maana ndo masharti ya asali hizo.

Upinzani hamna Tanzania wote ninyi ni waigizaji.
 
Jikite kwenye mada badala ya kutafuta mengine
 
 
1. Hayati John Magufuli hakuwa na kundi lolote ndani ya CCM isipokuwa alikuwa na kundi la waloigiza kuwa wamuunga mkono lakini wote ni wanafiki. Wale wachache walomwelewa na kujaribu kufuata maono yake mifano yake ni michache mmoja wao ni Suleiman Jaffo ambae ni direct chaguo la JPM.

2. Kwenye kutukana wazee hiyo ni ngumu kuelezea kwani ni hao walokuwa wamewekwa pembeni ambao leo hii wamerudishwa na twashuhudia wakifanya mambo ya ajabu katika wizara na taasisi walizopo. Vipio mbona husema pale ambapo walikuwa wakimsema JPM na hata baadae Nape kwenda Ikulu kuomba radhi?

3. Musiba nadhani alikuwa ni mhamasishaji tu au mtu ambae aliamua kwa utashi wake kuwa mfuasi wa JPM na sidhani kama hayati JPM mwenyewe alikuwa akifahamu kuhusu anoyafanya Musiba mitandaoni au hao sehemu ya watu wa TISS na mambo yao mengi tu.

4. Hata media ya Tanzania wengi bado ni "chequebook journalists" na si waandishi makini wa habari ndo maana ni rahisi sana kwa wao kufuata upepo bila kuzingatia misingi ya uandishi wa habari ambayo ni:

1. Kuhabarisha
2. Kuelimisha
3. Kuburudisha.

Tukionacho au kushuhudia safari hii au sasa hivi ni uandishi wa kutegemea umeambiwa/elekezwa uandike nini na wafuata amri kutoka kwa mtoa asali. Yaani sehemu kubwa ya media ya Tanzania nayo yasemekana wana vibuyu vya asali.

5. Kama kiongozi yoyote yule ni lazima apate wafuasi wa kile anokiamini na kukitekeleza. Sasa JPM aliamini katika uthubutu na maono yake ya Tanzania mpya. Ni katika hilo tuliweza kuona mambo mengi yakifanyika au kutekelezwa na yote yapo leo hii wakati mengine waloachiwa kuyamalizia badio wahangaika.

6. Kuhusu kwamba JPM hakuwa na ushawishi wowote majukwaani hilo ni kichekesho kwani hadi leo hii watanzania wengi na hata raia wa nchi zingine duniani waloanza kujitambua baada ya kumsikiliza akiwa majukwaani, leo hii wamehifadhi video zake za hotuba alokuwa akizitoa ili baadae vizazi vijavyo viweze kuambiwa kuwa alikuwepo raisi aliethubutu kufanya haya na yale lakini hakuchukua muda kukaa madarakani.

Mwisho, hayati JPM bado akumbukwa na hata weye mleta mada ni mmoja wa wale wanomkumbuka kwani ni aibu kwa mambo yote ambayo yalipotea wakati wa utawala wake sasa yote yamerudi.

Ni kweli alikuwa na mapungufu yake lakini hata yeye alisema kwamba tutamkumbuka kwa mazuri na si mabaya yake.

Tumkumbuke kwa mazuri.
 
wadanganye wajinga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…