#COVID19 Hayati Magufuli alificha taarifa ya Vifo vya Corona at our Risk

😀😀hii kwangu sio kazi mkuu ni mitandao ya kijamii nnayoitumia kurefresh mind nnapokuwa free kwa kubadilishana mawazo na watu tofauti siingizi hata mia huku, the same me nnaeza pitisha mwaka sijagusa fb wala insta unless its about the money sinaga muda wa kupoteza
sina ushamba wa teknolojia

Umefunga kazi bwana Fungakazi.

Ama kweli JF raha sana 😁😁.
 
Mambio ya sakafuni ya nini bro? Tulia, pole pole, utaishia ukingoni 😁😁:

View attachment 1984034

Hapo ni wenzio wafuasi kindaki ndaki wa shujaa wako. Hawana noma wala nini.

Hiiiiii bagosha!

Au nasema uongo ndugu MISULI?
Korona imekaa kisiasa zaidi. Kijijini kwangu sijawahi kumuona mgonjwa wa korona.
Huu ugonjwa unafanyiwa promo hadi kero!
 
Kijini kwangu sijawahi kumwona mgonjwa wa kifaduro, degedege, kipindupindu, kipanda uso, kichocho, donda koo, goiter, nk, wala wa nguvu za kiume.

Magonjwa hatari mitaani wala vijijini.

Nenda hospitali kama vipi usiache pia kujivinjari Mortuary.
 
Unatatizo kubwa sana.
Kabla ya korona huko hospital kulikuwa hakuna wagonjwa? Au ni lini mortuary kulikosa maiti?
huu ugonjwa mnaufanyia promo sana!
 
Ile hali ya kila kifo kuhusishwa na corona ndio kitu ambacho ulikuwa unataka iwe? na huo kwako ndio ukweli ambao unaona Magu alikuwa akiuficha?

Nakumbuka Ummy mwalimu alipokuwa akitangaza vifo, utamsikia akisema "Marehemu alikuwa na maradhi mengine pia" Ilifika muda maradhi mengine yalipumzika kuwa chanzo cha vifo.
Hivi ni nani mwenye mamlaka ya kutangaza chanzo cha maradhi au kifo cha mgonjwa?

Nakukubaliana na wewe kwamba si vyema kuhusisha kila kifo kilichotokea wakati wa mlipuko kilisababishwa na corona.

Lakini, je yale maradhi tuliyokuwa tunaambiwa kwamba ni "changamoto ya upumuaji" ilikuwa ni ugonjwa gani hasa wakati kitabibu hakuna "ugonjwa" unaitwa hivyo? Je, corona si changamoto ya upumuaji? Je, binadamu anapougua au kufariki hakuna haja ya kujua chanzo cha maradhi au kifo chake? Huoni kuita chanzo cha maradhi au kifo ni "changamoto ya upumumuaji" ninkuficha chanzo halisi cha ugonjwa?

Kifua kikuu, pumu na nimonia ni moja ya magonjwa yanayosababisha changamoto ya upumuaji. Je, umeshawahi kusikia wagonjwa wamefurika wodini kutokana na magonjwa haya?

Hujiulizi kwanini yale maradhi ya "changamoto ya upumuaji" yalitokea kwa "mlipuko" na kupelekea wagonjwa kujaa kwenye wodi hospitalini? Kwanini ile changamoto ya upumuaji haikuwa ni kutokana na corona?

Je, corona haijawahi kuua mtu/watu hapa nchini? Je, ulishawahi kumsikia Magufuli akisema kuna mtu/watu walikufa kwa corona hapa Tanzania?
 
Kuhusu kujua chanzo cha kifo hebu msikilize kwanza huyo Doctor.
 
Unatatizo kubwa sana.
Kabla ya korona huko hospital kulikuwa hakuna wagonjwa? Au ni lini mortuary kulikosa maiti?
huu ugonjwa mnaufanyia promo sana!

Ungemalizia kabisa:

1. Kabla ya korona huko hospital kulikuwa hakuna wagonjwa wa Corona?
2. Au lini mortuary kuliko maiti za Corona?

Hata hivyo huko tulishatoka. Sasa hivi tunakoelekea ni Jair Bolsonaro kama kiasi yetu ilivyo kuwa tokea mwaka jana:

Corona: Orodha ya wahanga, sampuli

Ninyi tulieni, mtatusikia.
 
Angeweka orodha ya waliokufa kwa Covid wewe ungenufaikaje na takwimu hiyo kama sio kutishana tu?

Kuna watanzania mnapoteza muda sana kwenye kufuatilia mambo yasiyo na ulazika, JPM alisema Covid ipo watu chukueni tahadhari lakini bado mnatafuta sababu oooh mbona hatangazi wanaokufa? Ivi vyombo vya habari kazi yake ni kutangaza vifo vya Covid tu??

Kazi ya Rais iwe ni kutisha watu tu? Sote tutakufa issue ni kutangulia tu
Hivi ni kweli kwamba kujua/kutangaza chanzo cha maradhi au kifo cha binadamu hakuna maana yoyote? Kama ni hivyo maabara ni za kazi gani kwenye vituo vya kutolea huduma za afya?

Ni hivi ndugu, msingi wa JPM kukataza kutolewa habari kuhusu vifo violivyotakona na corona si kuwaondolea watu hofu. Maguli alikusudia kuonesha ulimwengu kuwa yeye ni kiongozi mwamba, mwenye akili kuliko wote duniani na halazimishwi kufuata taratibu au miongozo ya kimataifa katika kuyaendea mambo kuhusu raia wake. Bali aliamin yeye au taifa lake wanakabiliwa na maadui wa kibeneru.

Ukweli ni kwamba alichukulia janga la corona kuwa ni "hujuma" ya mabeberu kwa taifa lake na si changamoto ya kiasili.

Alihisi kufuata miongozo ya afya ya kimataifa katika kukabiliana na janga hili ni "kupelekeshwa" na mabeneru kitu ambacho halikuwa hakitaki. Badala yake akaamua apambane na janga hili kwa njia tofauti. Magufuli hakupinga lockdown peke yake, alipinga watu kuvaa barakoa (alikosoa hadi makasisi waliovaa barakoa kanisani bali yeye mwenyewe hakuwahi kuvaa barakoa) na alipinga kufungwa kwa nyumba za ibada. Zaidi alikosoa na kizuia vipimo vya corona.

Alichotaka yeye ni kuonesha kwamba alikuwa sahihi kwenda kinyume na miongozo ya kitaalam (kimataifa) dhidi na kwamba Tanzania ilikuwa salama.

Hakupenda taarifa juu ua maradhi au vifo vilivyotokana na corona kwani inheonesha kuwa alifeli na kwamba yeye ndiye aliyechangia kusambaa na vifo vya raia kutokana na kupinga miongozo ya kiafya. Kumbuka yeye ni kiongozi mwamba asiyeshindwa mapambano.

Lakini kusingizia kuwaondolea watu hofu ni ulaghai tu ambao unawahusu watu wajinga.

Ni hivyo tu ndugu yangu.
 
Ukipata nafasi itafute hiyo video Youtube.
Nashukuru nimefanikiwa kufungua na kusikiliza hoja za huyu daktari. Nimeokota hoja zifuatazo zinazotetea msimamo wako na ule wa Magufuli kuhusu taarifa za vifo vinavyohusishwa na korona.
  • Si kila anayepimwa na kukutwa na korona hupata maradhi ya korona,
  • Aliyekufa akiwa na korona (died with C19) haimaanishi alikufa kwa korona (died from C19),
  • CDC wanachanganya Vifo vilivyotokana kweli na korona (True positive) na vile ambavyo si kweli hutokana na korona (False positive) kitu ambacho hupelekea kukuzwa kwa idadi ya vifo.
  • Daktari hawezi kujua chanzo cha kifo cha mgonjwa ila Mungu peke yake.
Hoja zake zote msingi wake ni ile fikra ya sayansi na falsafa kwemba “kubainisha chanzo (cause) cha matokeo (effect) si kazi rahisi hata kama kipo”. Ametumia fikra hii kwa makusudi kuwababaisha watu kuhusu taarifa za vifo vinavyohusishwa na korona ili kuonesha kwamba korona si chochote bali ni janga lililokuzwa kuliko uhalisia wake.

Hadi sasa sijui daktari huyu alifikisha muhadhara wake huu mbele ya hadhira ya watu wa taaluma gani. Lakini inashangaza sana kuona ameishia kufikisha hoja zake bila kuruhusu maswali kutoka kwa “mabingwa” wenzie waliokuwa wanamsikiliza. Nachelea kusema alikuwa anahutubia mbele ya hadhira ya watu wasio elewa kuhusu sayansi kama afanyavyo Mch. Gwajima au alijirekodi akiwa peke yake na kurusha mitandaoni.

Kuegemea kwenye hoja za huyu daktari kwamba anayejua chanzo halisi cha kifo cha mgojwa ni Mungu peke yake ni sawa na kusema kwamba hakuna yeyote hapa duniani anayejua ugonjwa unaua kwavile mwili hupatwa na magonjwa zaidi ya moja kwa wakati mmoja. Lakini hoja zake zinatoa msimamo kwamba “hakuna uhalali wa kuhusisha kifo cha mgonjwa aliyekufa akiwa na korona hadi ithibitike kuwa mgonjwa huyo hakuwa na ugonjwa mwingine wowote zaidi ya korona”. Kama huu ndo msimamo wake ingefaa afafanue maswali yafuatayo.

  • Kuna magonjwa zaidi ya milioni moja yanayojulikana na mengine mengi hayajulikani. Je, inawezekana mgonjwa anayeshukiwa kuwa na korona kupimwa na magonjwa mengine yote yanayojulikana ili kujua kama ana korona peke yake?
  • Tunawezaje kutambua kwa yakini kwamba aliyekufa akiwa na korona hakufa kwa ugonjwa huo endapo alikutwa na ugonjwa mwingine zaidi ya korona?
  • Je, korona peke yake haitoshi kuwa chanzo cha kifo (sufficient cause) hadi ichaganyike na ugonjwa/magonjwa mengine?
  • Ikiwa daktari anaweza kubaini chanzo cha ugonjwa na kutoa tiba sahihi na kumponya mgonjwa, kwanini ashindwe kubaini chanzo cha kifo cha mgonjwa?
Wanasayansi na falsafa wanaposema ni vigumu kubainisha chanzo cha matokeo Fulani haimaanishi kwamba ni “marufuku” kusema kitu Fulani ndo chanzo cha matokeo Fulani. Kama kuna hoja, dalili au ushahidi unaoonesha uwepo wa kile kinachoshukiwa kwenye matokeo fulani inatosha kudai kuwa kitu hicho ndo sababu/chanzo ya matokeo husika. Kanuni zifuatazo ndizo zinazowaongoza wataalam wa afya na wanasayansi kudai kwamba kitu fulani (virusi vya korona) ndio chanzo cha matokeo fulani (changamoto ya upumuaji au kifo).

  • principle of inclusivity: Kila mahali palipo na matokeo husika, kile kinachoshukiwa kuwa ni chanzo nacho pia kipo. Hii maana yake kila anayekufa kwa changamoto ya kupumua (matokeo) alikutwa na virusi vya korona (chanzo).
  • Principle of exclusivity: Kila pasipo na matokeo husika, kile kinachoshukiwa kuwa ni chanzo nacho hukosekana. Yaani wenye changamoto ya upumuaji wengi waliopona, hawakukutwa na virusi vya korona.
  • Principle of frequence: Kila mara matokeo yanapojitokeza, kile kinachoshukiwa kuwa ni chanzo nacho hujitokeza. Yaani mara zote inapotokea watu wengi hufa kwa changamoto ya upumuaji ndio kipindi virusi vya korona husambaa kwa jamii.
  • (Principle of correlation): Kuongezeka au kupungua kwa kiwango cha tukio husika kunaendana na kuongezeka au kupungua kwa kiwango cha kile kinachoshukiwa. Yaani kupungua au kuongezeka kwa vifo au maradhi ya changamoto za kupumua kwenye jamii kunaendana na kupungua au kuongezeka kwa maambukizi ya virusi vya korona kwa jamii.
  • Principle of succession: Matokeo hujitokeza baada na si kabla ya uwepo wa kile kinachoshukiwa kuwa ni chanzo. Ikiwa mtu alipoambukizwa virusi vya korana ndipo akaanza kuugua na kisha kufariki basi kifo hicho chanzo chake ni korona.
Kwa kuzingatia kanuni hizi ndipo daktari hupata uwezo wa kubaini chanzo cha ugonjwa na kuchagua tiba sahihi au kudai kuwa mgonjwa amekufa kwa ugonjwa X na sio Y.

Asante sana.
 
Kama hivyo ndivyo ulivyomuelewa basi sawa.
 
Bila shaka umeelewa "ujanja" wa huyu daktari kubabaisha watu kuhusu korona.
Ndio maana nikasema kama hivyo ndivyo wewe ulivyomuelewa basi sawa, kwa sababu ulichofanya ni kwamba ulikuwa unamsikiliza ili upinge na ndio maana unasema alichokieleza huyo Doctor ni ujaja wa kubabaisha watu.
 
Back
Top Bottom